Quantcast
Channel: BONGOWEEKEND
Viewing all 1902 articles
Browse latest View live

WAGOMBEA SITA URAIS WA TFF USO KWA USO TBC1

$
0
0

‘Wagombea sita wa Urais TFF uso kwa uso kwenye kipindi maalum leo Ijumaa saa 3 usiku, mbashara ndani ya TBC 1 na TSN online.’ KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) kesho Ijumaa (Agosti 11, 2017)wameandaa kipindi maalum kwa wagombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kitakachofanyika mjini Dodoma kuanzia majira ya saa 3 usiku. Kipindi hicho maalumu kitarushwa mubashara kupitia TBC pamoja na ‘TSN Online’ kitawakutanisha wagombea urais; Ally Mayay, Fredrick Mwakalebela, Wallece Karia, Shija Richard, Iman Madega na Emmanuel Kimbe ikiwa ni saa chache kabla ya siku ya uchaguzi yaani kesho kutwa Jumamosi.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya kipindi hicho, Enock Bwigane alisema kuwa ili mpira wa miguu uendelee kukua nchini TBC na TSN iliona ni vyema ikawakutanisha wagombea kwenye jukwaa moja ili waweze kuwaambia wananchi ni kwa njia gani wataweza kuinua soka la Tanzania kama wakipewa dhamana hiyo.

Alisema, “Kuna takribani wapiga kura 130, wagombea urais ni sita lakini mmoja ndiye atakayeshinda na kuongoza shirikisho hilo kwa miaka minne kabla ya uchaguzi mwingine hivyo tumeona haja ya kuwakutanisha na kuwawezesha wananchi waweze kuwafahamu... “…Naamini fursa ya kuwakutanisha na kuwapa nafasi ya kuwaeleza watanzania sera na mipango yao ya kuboresha soka ni jambo la msingi na ni haki yao ukizingatia kuwa leo ndiyo siku ya mwisho ya kampeni,” alisema Bwigane.

Naye Katibu wa kamati hiyo, Alfred Lasteck alisema kuwa TSN ikishirikiana na TBC inatambua nini watanzania wanataka kufahamu kuhusu mpira wa miguu na ndiyo maana imepanga kuwakutanisha wagombea ili waweze kuzungumza na umma kabla ya uchaguzi hapo kesho.

“Kuna zaidi ya Watanzania milioni 50 ambao wangependa kufahamu ni nini kitasaidia soka la Tanzania ili liweze kuendelea kutoka lilipo sasa hadi kufikia mafanikio.

“Hivyo ni nafasi ya kipekee kwa kila mtanzania kufuatilia matangazo mubashara yatakayorushwa na TBC1 pamoja na TSN Online kipindi kile ambacho wagombea wote wa Urais watakapokuwa wakielezea mipango yao kuhusu mpira wa miguu nchini,” alisema Lasteck.


MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE AZINDUA MADARASA SITA KATA YA PERA

$
0
0

MBUNGE wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,amewahimiza wananchi kujenga tabia ya kujitolea katika shughuli za kimaendeleo pasipo kuachia serikali/halmashauri na wahisani pekee.

Aidha amesema ofisi yake na halmashauri wataendelea kuunga mkono juhudi za wafadhili na wadau wanaojitokeza kushirikiana nao kutatua changamoto zinazowakabili jimboni hapo ikiwemo elimu.

Ridhiwani alitoa rai hiyo, wakati wa uzinduzi wa majengo ya madarasa sita na ofisi moja ya walimu katika shule ya msingi Pakistan Utete iliyopo kata ya Pera,Chalinze wilayani Bagamoyo,yaliyokarabatiwa kwa ufadhili wa marafiki wa Pakistan,kwa gharama ya sh.milioni.30.

Alisema baadhi ya wafadhili wanasaidia endapo wanaona jamii husika ikichukua juhudi na kufikia hatua mbalimbali .

Aliwataka wananchi wa Chalinze kushirikiana na serikali,halmashauri na wafadhili wanaojitokeza ili kukamilisha miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao.

“Ajenda kubwa tuliyonayo ni kuboresha na kutatua changamoto katika sekta ya elimu” “Pamoja na shughuli zinazofanywa na wahisani lakini haina budi wananchi mkajitolea katika shughuli za maendeleo ili tukienda kuomba msaada kwa wafadhili waweze kukubali kirahisi kwa kuona hatua ambazo zimeanza kuchukuliwa “alisema Ridhiwani.

Ridhiwani alisema wakati marafiki wa Pakistan wakiwezesha ukarabati huo,lakini halmashauri ya Chalinze imeshatenga fedha kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo nane katika shule ya Pakistan Utete. Hata hivyo,mbunge huyo alieleza kwamba,pia wanajenga matundu ya vyoo katika shule ya msingi Mbala sanjali na madarasa mawili ya shule ya msingi Makombe.

Ridhiwani alieleza,ujenzi wa matundu ya vyoo utasaidia kuondoa kero ya uchafu wa mazingira ambapo baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakijisaidia ovyo maporini ,vichakani .
“Kwasasa kilichobakia ni usimamizi katika hatua ya ujenzi unaoendelea kwenye shule hizo ”alisema Ridhiwani.

Akizungumzia msaada walioupata kutoka kwa marafiki wa Pakistan,Ridhiwani aliomba ushirikiano ulioonyeshwa usiishie hapo .
Alimpongeza mwenyekiti wa kitongoji Hussein Mramba na diwani wa kata ya Pera kwa jitihada walizozichukua kusukuma jambo hilo.
Ridhiwani hakusita kumuomba balozi wa Pakistan nchini Tanzania,Amir Khan ,kuwasaidia ujenzi wa jengo la kulaza wagonjwa na mashine za kupima magonjwa katika kituo cha afya Chalinze.

Akizindua majengo hayo,balozi wa Pakistan nchini Khan,alisema amefurahishwa na ushirikiano uliopo baina ya nchi hiyo na Tanzania,na alishauri kuwepo na mahusiano kati ya wabunge wa Pakistan na Tanzania.

“Nilipoambiwa kuja shuleni hapa ni km 120 kutoka Dar es salaam nikaona nije kutembea na kuona kilichofanyika,Nawapongeza kwa kuanzisha ujenzi huu ili watoto wapate elimu”alisema Khan.

Alisema ili watoto hao wasome vizuri ni vyema kukajengwa uzio katika shule hiyo ili kuweka usalama zaidi hivyo wanatasaidia kuujenga. Balozi huyo,aliahidi na kukubali ombi la kusaidia mashine na vifaa vya kituo hicho cha afya lakini kwasasa wanachotakiwa kufanya ni kuandika maombi ya msaada huo.

KILIMO CHENYE TIJA BILA YA KUWA NA SOKO LA UHAKIKA NI KAZI BURE KWA MKULIMA

$
0
0


 Mkuu wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Selemani Mzee, akizungumza na maofisa ugani wakati akifungua mafunzo ya namna ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi leo ambayo yaliandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). Kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa wilaya hiyo, Winfrid Tamba, Mtafiti Bestina Daniel kutoka COSTEC na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa wilaya hiyo, Kanzumari Malilo.


 Ofisa Tawala wa wilaya hiyo, Benaya Kapinga akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa wilaya hiyo, Selemani Mzee (kushoto) kuzungumza na maofisa ugani. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Masasi, Juma Satmah.
 Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Masasi, Juma Satmah, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Watafiti watoa mada wakisubiri kutoa mada zao. Kutoka kulia ni Dk. Nicholaus Nyange, Benadetha Kimata na Dk. Dk.Emmarold Mneney.
 Mshauri wa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Mkoa wa Mtwara, Ally Linjenje, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
 Mtafiti kutoka Costech, Bestina Daniel akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo kwa maofisa ugani.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wa wilaya hiyo, Kanzumari Malilo, akishukuru COSTECH kwa kuwapelekea mafunzo maofisa ugani wa wilaya hiyo.
 Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Mafunzo yakiendelea.
 Mwenzeshaji wa mafunzo hayo Kutoka OFAB Dk.Emmarold Mneney, akitoa mada.
 Muonekano wa chumba cha mafunzo hayo.
 Viongozi wa Wilaya hiyo wakiwa kwenye mafunzo hayo.
 Ofisa Ugani, Saidi Mnangona kutoka Kata ya Chigugu, akiuliza swali.
 Ofisa Ugani, Jacob Mbuya kutoka Kata ya Chikunja, akiuliza swali

Ofisa Kilimo, Lothi Philipo Mollel kutoka Kata ya Chiungutwa, akiuliza swali.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi na Jamii ya Viazi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Mtwara Naliendele, Benadetha Kimata, akitoa mada
Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa matumizi ya kilimo, Dk.Nicholaus Nyange, akitoa mada.

Na Dotto Mwaibale, Masasi

MKUU  wa Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Selemani Mzee amesema kilimo chenye tija kitakuwa na maana iwapo kutakuwa na masoko ya uhakika ya kuuza mazao  kinyume ya hapo itakuwa kazi bure kwa wakulima.

Hayo ameyasema wilayani hapa leo  wakati akifungua mafunzo ya namna ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). 

Mzee alisema bila ya kuwa na masoko ya kununua mazao ya wakulima itakuwa ni kazi bure hivyo ni vema kilimo chenye tija kikaenda sanjari na kupatikana kwa masoko hayo.

Mzee alisema wakulima wa Masasi wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kulima kwa kutumia nguvu nyingi lakini anavuna kidogo pamoja na matatizo ya masoko. Alisema teknolojia ya kilimo ndio itakayomkomboa kwani atalima eneo dogo na kuvuna mazao mengi.

Katika hatua nyingine Mzee aliwataka maofisa ugani wilayani mwake kuhakikisha  wanawasaidia wakulima kulima mahindi ya  WEMA ambayo yanahamasishwa na watafiti wa masuala ya kilimo kutokana na kustahimili ukame.

“Ninachowaomba tujipange kuwasaidia wakulima wetu namna ya kupata masoko ya mazao yao, watatumia teknolojia je wakishapata mazao mengi watauza wapi? Lakini pia tuwasaidie akishavuna mazao yake atahifadhi vipi? alihoji Mzee.

Alisema kwamba mbinu za kilimo cha teknolojia ambayo inahamaishwa na wanasayansi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ndio tiba pekee ya kuachana na kilimo kisicho na tija.

“Nawaagiza kwamba mkitoka hapa, mkawahamasishe wakulima wenu angalau walime hata nusu ekari ya mahindi haya yanayohamasishwa kutumiwa na watafiti wetu. Nafahamu kwamba wakipata mazao mengi lazima msimu ujao wataongeza eneo la kulima,” alisema Mzee.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka pia maofisa ugani hao kuhakikisha kwamba licha ya kulima mazao hayo, lakini pia wakahamasishe wakulima kutumia mbegu za mihogo hasa kiroba ambayo inahamasishwa na watafiti wa Kituo cha Utafiti Naliendele Mtwara.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Masasi, Juma Satmah alisema kuwa kundi hilo la wataalam wa kilimo ni muhimu sana kwa maendeleo ya wilaya hiyo kwa kuwa ndio wahamasishaji wakubwa wa kilimo ingawa mara nyingi limekuwa likisahaulika.


Mwenzeshaji wa mafunzo hayo kutoka Kutoka OFAB Dk.Emmarold Mneney aliwaambia washirikiwa mafunzo hayo kuwa bioteknolojia katika kilimo itasaidia kuepukana na magonjwa, wadudu waharibifu na pia inasaidia mazao kukabiliana na ukame.

Alisema kuna teknolojia ya uzalishaji wa mbegu kwa kutumia tishu ambayo kwa sasa imesaidia kupata mbegu nzuri za muhogo, korosho na nanasi na kudhibiti wadudu waharibifu kama  mahindi ambazo zinajulikana kama WEMA.

Alisema teknolojia nyingine ambayo imebuniwa na watafiti ni kupata mbegu kwa njia ya uhandisi jeni (GMO). Alisema kwa sasa watafiti wanaendelea kufanya utafiti wa mihogo na mahindi ili waangalie ukanzani wa mazao hayo dhidi ya magonjwa, ukame na uharibifu wa wadudu.

Mtafiti Bestina Daniel kutoka COSTECH alisema kupitia Jukwaa la bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini wameona waendeshe mafunzo kwa wakagani ambao ndio nguzo ya kilimo ili  kuwakumbusha majukumu yao na kuwapatia  mbinu malimbali za kilimo kwa kuwa wanategemewa na wakulima. 

Aidha aliongeza kuwa mafunzo hayo ya siku moja kwa maofisa  ugani hao yamelenga kuwapatia mbinu bora za uzalishaji wa mazao ya korosho, mahindi na Mihogo na nafasi ya matumizi ya bioteknolojia katika kusaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima na kuongeza uzalishaji.

Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi kwa nyakati tofauti aliwajulisha washiriki wa mafunzo hayo kuwa wakulima wa Tanzania hawajabahatika kulima zao lolote lililofanyiwa uhandisi jeni.

" Hadi sasa, hakuna mkulima wa Tanzania aliyewahi au anayelima mazao ya Uhandisi jeni (GMO), na sio kulima tu hata wale wanaofuga, hakuna mfugaji mwenye mnyama wa GMO Tanzania." alisema Nyinondi.

Akifafanua kauli yake Philbert Nyinondi alisema watu wengi kwa kutofahamu au kwa makusudi wanawachanganya wakulima hasa wale wanaotumia mbegu za chotara na kuwaambia ndo GMO.

"Tumefikia upotoshaji wa kiwango cha juu sana kwenye jamii. Mtu akiona kitu bora au kilichoboreshwa mfano maembe makubwa, mananasi makubwa, mimea inayokuwa kwa muda mfupi na hata kuku wa kisasa huitwa GMO. Ukweli ni kwamba labda Serikali yetu iamua wakulima wa Tanzania wafaidi teknolojia hii mapema zaidi. Vinginevo, kwa kasi ya watafiti wetu, tunaweza kuwa na zao la kwanza la GMO kwa mkulima kuanzia mwaka 2022" alisema Nyinondi.  

Alitanabaisha kuwa upatikanaji wa mazao GMO hata hiyo mwaka 2022  utategemea matokeo ya utafiti unaendelea nchini, tathimini zitakazofanywa na Taasisi ya serikali kama kamati ya kusimamia matumizi salama ya bioteknolojia NBC, 

Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Mamlaka wa Uthibiti wa Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na wepesi wa kampuni za mbegu zenye usajili Tanzani kuzalisha mbegu za kutosha kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima.


UVCCM YAWATAKA WFANYAKAZI WA UMMA KUTENGANISHA SIASA NA MAENDELEO

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Viongozi Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akionyesha ilani ilani ya CCM mwaka 2015-2020 na maelekezo ya namna ya utekelezaji wakati akizungumza na Viongozi Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba Ndg Abdallah Rashid Ali akielezea namna Ofisi ya Mkuu wa Wilaya inavyotekeleza ilani ya CCM mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

Na Mathias Canal, Kusini Pemba

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa kauli moja Umewataka watumishi wa Umma kote nchini Kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015-2020 kwa kutenganisha Siasa na shughuli za maendeleo. 

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 15, 2017 na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Ndg Shaka Hamdu Shaka (MNEC) alipokuwa akizungumza na Viongozi Mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Mara baada ya kuzuru katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.

Shaka ametilia mkazo zaidi kwa kuwataka Watumishi wa Serikali kutenganisha siasa na Majukumu ya kazi kwa Wananchi ili kuwaletea maendeleo pasina kuwabagua kwa dini, kabila ama utofauti wa itikadi za vyama vya kisiasa.

Alisema kuwa litakuwa Jambo la aibu tena lisilovumilika kwa Viongozi wa Umma kushughulika na Mambo ya siasa kwani hizo Ni kazi za vyama vya siasa ambavyo hata vyama vya siasa vina mipaka katika kufanya siasa.

Shaka Alisema kuwa watumishi wa Umma wamepewa dhamana kubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli hivyo Ni matarajio ya Chama Cha Mapinduzi CCM na Serikali, watumishi wote Kusimamia na kuwajibika ili Kutekeleza imara ilani kwa utayari.

Alisema kuwa ilani ya CCM imeielekeza Serikali kufanya Mambo mengi ya Maendeleo ambayo kwa asilimia kubwa tayari yameanza kutekelezwa kwa usimamizi mzuri wa Rais Magufuli.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo chini ya CCM hivyo kila kiongozi aliyeajiriwa na Serikali Ana jukumu moja kubwa la Kutekeleza ilani kwa umakini mkubwa kwa maslahi mapana ya Taifa.

"Kama kuna mtumishi asiyefanya hivyo basi ni wazi kuwa hastahili kuendelea kuwa kwenye nafasi yake"

"Tunakuwa na mipango mingi lakini utekelezaji wake unasuasua kwa kisingizio Cha bajeti ndugu zangu ifike Wakati tuwe na bajeti inayotekelezwa na itekelezwe kwa umakini, uangalifu na weledi Mkubwa" Alisema Shaka

Alisema kuwa watumishi wa serikalini wanapaswa kubainisha vyema Mipango ya muda mfupi na muda mrefu kwa manufaa ya Wananchi pasina kuwabagua zaidi ni kukubali kuwa wawajibikaji wazuri.

Katika Hatua nyingine UVCCM Taifa imempongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Dkt Ali Mohed Shein kwa maendeleo endelevu aliyoyafanya katika kipindi Chake tangu amekuwa Rais wa Zanzibar kwa kuimarisha Huduma za uwanja wa Ndege, uchumi wa Pemba umeimarika, fursa za uwekezaji sio Kama kipindi kilichopita.

Umoja huo umesisitiza kuwa Ni vyema wasaidizi wa Rais kumsaidia kwa vitendo sio maneno kwani Ni Lazima Viongozi kuwa na uthubutu na uwajibikaji.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ANAIWAKILISHA NCHI KWENYE MKUTANO WA SKAUTI DUNIANI

$
0
0

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anahudhuria Mkutano Mkuu wa Skauti wa Dunia ambao unafanyika jijini Baku, Azerbaijan.  Akiikisha Chama Cha Skauti Tanzania akiwa na wajumbe wengine watano.

IKUNGI CUP YAZINDULIWA RASMI

$
0
0


SERIKALI imekuwa ikifanya jitihada za dhati katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, Nyumba za walimu, Maabara, Matundu ya vyoo na mabweni.

Ili kunusuru kadhia hiyo imeelezwa kuwa moja ya mikakati ni pamoja na wakuu wa Wilaya kuwashirikisha wananchi pamoja na wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto na hatimaye kuwafanya wanafunzi wawe na furaha na amani. 

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa miguu yanayojulikana kama “IKUNGI ELIMU CUP 2017” itakayofanyika katika vijiji vyote 101 vilivyopo katika wilaya ya Ikungi.

Mashindano hayo yaliyoanza leo Agosti 19, 2017 katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Ikungi yanataraji kufika ukomo siku ya Jumanne Septemba 19, 2017 kwa matazamio ya kuwafikia zaidi ya wanachi 5000 katika Wilaya hiyo.

Dkt Lutambi alisema kuwa Mashindano hayo yenye kauli mbiu isemayo “CHANGIA, BORESHA ELIMU IKUNGI” yamebeba mtazamo chanya wa elimu wenye manufaa kwa wananchi katika kizazi cha sasa kuelimika na kizazi kijacho.

Alitumia nafasi hiyo pia kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu huku akiwaeleza wananchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli alichagua mtu muhimu kumuwakilisha katika Wilaya hiyo kwani ubunifu wake katika utendaji una manufaa makubwa kwa wananchi na jamii kwa ujumla.

Awali akisoma taarifa ya uzinduzi wa Mashindano hayo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa mashindano hayo ambayo yatakuwa yanalenga kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali kuchangia vitu mbalimbali kwa ajili ya kuboresha changamoto zinazoikabili sekta ya elimu katika Wilaya ya Ikungi ikiwemo upungufu wa nyumba za walimu, maabara ya masomo ya sayansi kwa shule za sekondari, Madarasa kwa shule za msingi pamoja na vifaa vya kujifunzia.

Sambamba na mashindano hayo ya mpira wa miguu lakini pia umezinduliwa ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya masomo ya Sayansi ambazo zipo katika hatua za msingi kwa muda mrefu.

Aidha, zimetolewa zawadi kwa wanafunzi waliopata daraja la kwanza (Division One) katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka huu 2017 na walimu wao ikiwa ni ahadi iliytolwa na mkuu wa wilaya hiyo.

Mhe Mtaturu aliahidi kutoa shilingi laki moja kwa kila mwanafunzi atakayepata Daraja la Kwanza na shilingi milioni moja kwa walimu kwa wanafunzi 10 watakaopata Daraja la Kwanza.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi akihutubia mamia ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa miguu ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017”
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi akihutubia mamia ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa Mashindano ya Mpira wa miguu ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017”
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisoma taarifa ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017” mbele ya Mgeni rasmi ambayeni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambi wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa Miguu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akibeba tofali lililofyatuliwa na Mgeni rasmi ambayeni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angeline Lutambiwakati wa ufunguzi wa mashindano ya mpira wa Miguu ya “IKUNGI ELIMU CUP 2017”
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Singida Ndg Jimson Mhagama akibeba tofali lililofyatuliwa wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturuakifyatua matofali wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi akifyatua matofali wakati wa ufunguzi wa zoezi la ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa maabara na madarasa.
Kikosi cha Timu ya Ikungi United
 Kikosi cha Timu ya Puma Combine kilichoshinda goli 3 kwa 2 dhidi ya Ikungi United
Moja ya wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita kwa kupata Daraja la kwanza akipokea shilingi 100,000 ikiwa ni ahadi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu
Matofali ambayo yamefyatuliwa na wadau wakati wa ufunguzi wa ufyatuaji matofali Wilayani Ikungi


Mipira iliyotolewa kwa jili ya timu zote washiriki wa “Ikungi Elimu Cup 2017”


TANZANIA RATED BEST SAFARI COUNTRY 2017

$
0
0
THE NETHERLANDS – SafariBookings.com has conducted an in-depth analysis of reviews from safari tourists and acclaimed Africa experts to determine the continent’s best country for safaris. And the winner? Tanzania came out on top – the country is the clear winner and has been awarded our best safari country for 2017.
More than 2,500 reviews were used in this comprehensive research. Contributions came from safari-goers all over the world. And 22 reputable guidebook authors – working for Lonely Planet, Rough Guides, Frommer’s, Bradt and Footprint, who make-up the SafariBookings expert panel – also contributed reviews.

BONDIA SELEMANI SIMBA HAPANIA KUTOA KICHAPO KWA MABONDIA KUANZIA AGOST 26 VIJANA

$
0
0


 

Na Mwandishi Wetu


BONDIA wa ngumi za kulipwa kutoka Singida Selemani Simba 'Singida Unaited' amendelea na mazoezi ya kujifua kwa ajili ya mpambano wake wa Agost 26 utakaofanyika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni ambapo atapambana na Kallage Ramadhani bondia anaenolewa na kocha mkongwe katika ngumi Rajabu Mkamba

Akizungumzia mpambano wake Simba amesema kuwa amekuja Dar kwa ajiri ya kupambana na kuwapiga mabondia wote watakaopambana nae wakati wowote ule bondia huyo mpaka sasa kashapigana mapambano mawili kati ya hayo mawili kashinda moja na kudundwa moja

akizungumzia matarajio yake katika masumbwi amesema anatamani kufika mbali zaidi kama Ibrahimu Class 'King Class Mawe' walivyofanikiwa kufika mbali na mpaka sasa kuwa bingwa wa Dunia

katika mpamano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya ubingwa kati ya bondia Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' na Baina Mazola 'Simba Mazola'

mapambano mengine ya siku hiyo ni sajo bosco Jr atakumbana na juma rashidi mdobinaIssa Nampepecha ataoneshana umwamba na Abbas Mwamba wakati Karim Ramadhani ataoneshana kazi na Yohana Dhobian na Keisii Amali atakuchiana ngumi na Hashimu Chisola na Said Wigo atazipiga na Chicho Ramadhani

Mapambano haya yote yatasimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC ambayo yenye dhamana ya kuendesha mchezo wa ndondi za kulipwa nchini


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alv

erez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi

SERIKALI YATOA UFAFANUZI UJIO WA BOMBADIER

MABONDIA BAINA MAZOLA NA FRANSIC MIYEYUSHO WAZIDI KUTAMBIANA KUMALIZA UBISHI AGOST 26 VIJANA KINONDONI

$
0
0


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Baina Mazola 'Simba Mazola' na Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' wamendelea kutambiana kwa ajili ya mpambano wao ujao utakaofanyika Agost 26 katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mpambano wa raundi nane uzito wa kg 57

Wakiongea kwa nyakati tofauti kambi hizo zimejimba kila mmoja kumpiga mwenzake raundi za awali

Kwa upande wa Miyeyusho amejigamba kuwa katika mabondia wa Mabibo wanaofundishwa na kocha Cristopher Mzazi akuna anae msumbua ata mmoja hii ni pambano la kisasi ukumbuke kuwa Mzazi ana mabondia wengi na mimi ndie ninae mwalibia mara ya kwanza nilimvunja mbavu bondia wake Ramadhani Shauli akakaa mbali na mchezo wa ngumi mwaka mzima wakaniletea bondia mwingine Nassibu Ramadhani nae nikafanya hivyo hivyo sasa wamemleta huyu Mazola nita akikisha  navunja mbavu kama nilivyo wafanyia wenzake wawili

Kwa upande wa Mazola nae ametamba kumsambalatisha mpinzani wake raundi za mwanzo kwani ana jipya ukumbuke mchezo wa ngumi sio sawa na michezo mingine umri ukienda biashara imekwisha sasa naenda kumstafisha ngumi rasmi yule babu hivyo wapenzi waje kwa wingi siku hiyo ili waone ninavyo mwachisha ngumi

nae mratibu wa mpambano huo kaizirege Dragon Kaizum amesema mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi wakati bondia kutoka Singida Selemani Simba 'Singida Unaited' atakumbana na Kallage Ramadhani na Sajo Bosco atapambana na Juma Rashidi Issa Nampepecha ataoneshana umwamba na Abbas Mwamba wakati Karim Ramadhani ataoneshana kazi na Yohana Dhobian na Keisii Amali atakuchiana ngumi na Hashimu Chisola na Said Wigo atazipiga na Chicho Ramadhani

Mapambano haya yote yatasimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC ambayo yenye dhamana ya kuendesha mchezo wa ndondi za kulipwa nchini


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi

KINANA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI TANO ZA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akiwa katika mazungumzo na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, alipokutana nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), akiwa na Mabalozi wa nchi tano za Ukombozi Kusini mwa Afrika, wanaoziwakilisha nchini zao hapa nchini, baada ya mazungumzo nao katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Mabalozi hao ni wa nchi za Zimbambwe, Zambia, Namibia, Msumbiji na Afrika Kusini. 
PICHA: BASHIR NKOROMO. KWA PICHA ZAIDI ZA KIKAO HICHO/>BOFYA HAPA 

JANUARI MAKAMBA AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA DIASPIORA ZANZIBAR

$
0
0
Na Mathias Canal, Zanzibar

Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) limefunguliwa jana tarehe 4 Agosti 2017 kwa kuwashirikisha washiriki wapatao 350, ambapo miongoni mwao wanadiaspora wamehudhuria zaidi ya 200 na watendaji kutoka taasisi za Serikali zote mbili wakiwa ni 150.

Diaspora wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini katika sekta ya kuimarisha na kuanzisha viwanda ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba (MB)  alipomuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi litakalodumu kwa siku mbili Agosti 23 na 24, 2017 katika ukumbi wa Sea Cliff Hotel uliopo katika kijiji cha Kama Wilaya ya Magharibi A.

Mhe Makamba alisema kuwa kwa sasa Demokrasia imeimarika nchini kutokana na serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kukubaliana kwa kauli moja kuimarisha usalama wa wananchi ili kurahisisha uimara wa uwajibikaji wa ujenzi wa Taifa.

Alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakabili Diaspora ikiwemo ucheleweshwaji wa uwekezaji sambamba na kutokuwepo sera ya utambuzi dhidi yao lakini changamoto hizo zinaendelea kutatuliwa na hatimaye kumalizika kabisa.

Changamoto zingine ilikuwa ni pamoja na kuwepo kwa uraia wa nchi mbili ambapo Mhe Makamba alisema kuwa serikali inalifanyia kazi jambo hilo kwani halipo katika uhalisia kwa sasa kwa kutokuwepo kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ili Diaspora waweze kutumia fursa ya uwekezaji nchini kwa urahisi huku akiwasihi kutumia fursa muhimu za uwekezaji katika Nyanja zote kwani faida itakuwa kwa Diaspora wenyewe, watanzania waishio nchini na Taifa kwa ujumla wake.

Alisema kuwa Diaspora ni kiungo muhimu katika kuchangia sehemu kubwa ya maendeleo endelevu katika nchi zao za asili kwa kuchangia katika uhamishaji wa rasilimali, ujuzi na mawazo na hatimaye kupelekea nchi yao kunufaika na uchumi wa kidunia unaoonekana kukua siku hadi siku.

Alisema kuwa fedha zinazotumiwa na Diaspora katika nchi wanazoishi ni miongoni mwa vyanzo vinavyosababisha ukuaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi, fedha hizo zitakapotumika vizuri kwa uwekezaji katika biashara na vitega uchumi ndio huwa chanzo na kichocheo cha ukuaji jadidifu wa pato na uchumi wa nchi zinazopokea fedha hizo.

Aidha, Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeweka msisitizo na juhudi za kukusanya mapato ili kukuza uchumi wa Tanzania na uwezo wa serikali kujiendesha.
Mhe Mkamba aliwasihi Diaspora kufuata kanuni,taratibu na sheria katika nchi wanazoishi ili kuendelea kuiweka Tanzania katika sifa nzuri ya kuwa na wananchi wenye kufuata sheria na taratibu.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeratibu Kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi Ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) kwa minajili ya kuwaweka pamoja watanzania hao ili kujadili kwa pamoja namna ya kutumia fursa za uwekezaji.
Kongamano hilo ni mwendelezo wa makongamano matatu ya awali yaliyofanyika mwaka 2014 na 2015 Jijini Dar es Salam na mwaka 2016 lililofanyika Mjini Zanzibar.

Lengo kuu la makongamano hayo ni kwa Serikali na wanadiaspora kukutana, kubadilishana mawazo na kuwashajihisha wanadiaspora kuwekeza nchini kwao kwa maslahi yao na kwa ustawi wa uchumi wa taifa lao.

Kongamano hili la nne la Diaspora limebebwa na dhamira ya “Uzalendo kwa Maendeleo” chini ya kauli mbiu isemayo “Mtu Kwao, Ndio Ngao”

Katika hatua nyingine washiriki wote wamepata fursa ya kujadili kwa pamoja namna bora ya kuboresha umoja huo wa watanzania waishio nje ya nchi sambamba na kutoa maoni yao kwa serikali kwa dhamira ya kuwa na Umoja na ushirikiano bora kati yao na serikali.

Pia walitembelea shamba la BIG BODY SPICE linalolima mazao mbalimbali ya
viungo ikiwemo mazao ya Pilipilimanga, Mdalasini, Kahawa, Hiliki, Vanila,
Mdoriani, Kakao, Karafuu, Tangawizi, Mrangirangi na Mkungumanga.



Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayeshughulikia Mazingira Mhe Januari Makamba MB) akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Baadhi Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo
Mkurugenzi Mpya wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Ndg Geofrey Mwambe akizungumza wakati wa Kongamano la nne la watanzania waishio ughaibuni linalofanyika Sea Cleaf Hotel Mjini Zanzibar
Washiriki wa Kongamano la nne la Watanzania waishio ughaibuni (4th Tanzania Diaspora Conference) wakifatilia Mjadala wa ufunguzi wa kongamano hilo

Dkt Hamed Hikmany (Katikati) akiongoza mada kuhusu Ushauri wa uwekezaji kwa siku zijazo mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

Mhe Hassan Khamis (Katikati) akiongoza mada kuhusu Jukumu la jumuiya ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi katika uwekezaji sambamba na Diaspora na nchi yao katika maendeleo endelevu mara baada ya ufunguzi wa kongamano la nne la watanzania waishio nje ya nchi lililofanyika jana Agosti 23, 2017 Sea Cliff Hotel Mjini zanzibar

MABONDIA KIVU ABDI NA CHESA BULI KUPAMBANA OCKTOBA 20 MANYARA PARK

MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA KESHO VIJANA KINONDONI

$
0
0


Mabondia Baina Mazola kushoto akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao jumamoso Agost 26 katika ukumbi wa Vijana Kinondoni Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mratibu wa mpambano wa masumbwi kaizirege Dragon Kaizum katikati akiwatambulisha mabondia mbele ya wahandishi wa habari kushoto ni Baina Mazola na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa agost 26 jumamosi hii litakalofanyika katika ukumbi wa vijana kinondoni Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Selemani Simba akipama uzito kwa ajili ya mpambano wake na Kallage Hassani utakaofanyika jumamosi ya agost 26 katika ukumbi wa vijana kinondoni Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Kallage Hassani kushoto akituniashiana misuli na Selemani Simba 'Singida United' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho agost 26  katika ukumbi wa Vijana Kinondoni Picha na SUPER D BOXING NEWS


Mabondia Kallage Hassani kushoto akituniashiana misuli na Selemani Simba 'Singida United' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho agost 26  katika ukumbi wa Vijana Kinondoni Picha na SUPER D BOXING NEWS



Mabondia Cosmas Cheka Kushoto akitambiana na Haidal Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho Agost 26 katika ukumbi wa Vijana Kinondoni 
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Baina Mazola 'Simba Mazola' na Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' wamepia uzito kwa ajili ya mpambano wao  utakaofanyika jumamosi Agost 26 katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mpambano wa raundi nane uzito wa kg 57

Wakiongea kwa nyakati tofauti kambi hizo zimejigamba kila mmoja kumpiga mwenzake raundi za awali

Kwa upande wa Miyeyusho amejigamba kuwa katika mabondia wa Mabibo wanaofundishwa na kocha Cristopher Mzazi akuna anae msumbua ata mmoja hii ni pambano la kisasi ukumbuke kuwa Mzazi ana mabondia wengi na mimi ndie ninae mwalibia


Kwa upande wa Mazola nae ametamba kumsambalatisha mpinzani wake raundi za mwanzo kwani ana jipya ukumbuke mchezo wa ngumi sio sawa na michezo mingine umri ukienda biashara imekwisha sasa naenda kumstafisha ngumi rasmi yule babu hivyo wapenzi waje kwa wingi siku hiyo ili waone ninavyo mwachisha ngumi

nae mratibu wa mpambano huo kaizirege Dragon Kaizum amesema mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi wakati bondia kutoka Singida Selemani Simba 'Singida Unaited' atakumbana na Kallage Ramadhani na Sajo Bosco atapambana na Juma Rashidi Issa Nampepecha ataoneshana umwamba na Abbas Mwamba wakati Karim Ramadhani ataoneshana kazi na Yohana Dhobian na Keisii Amali atakuchiana ngumi na Hashimu Chisola na Said Wigo atazipiga na Chicho Ramadhani

Mapambano haya yote yatasimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC ambayo yenye dhamana ya kuendesha mchezo wa ndondi za kulipwa nchini


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi

DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam Agosti 25, 2017. Wahandisi wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya kuibuka  wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama "Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE". Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani), amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo, kutembelea mashuleni ili kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili wapende kujisomea masomo ya sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye waje kushika nafasi kama walizo nazo wao.
Dkt. Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, wakati akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa tuzo na Makamu nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi wanawake Tanzania “Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition, (TAWECE), ambalo huenda sambamba na maonesho ya shughuli za kihandisi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
“Niwapongeze sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini niwaase, mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia kwenu, wanaweza kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo baadaye kufanya kazi za kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Dkt. Mwinuka alisema, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Shirika kwani inajenga picha (image) nzuri mbele ya jamii kuonyesha juhudi zetu za kuwahudumia wateja wetu. Alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye hafla hiyo fupi, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, alisema Wahandisi wanawake kutoka TANESCO, walionyesha umahiri wao katika kuelezea teknolojia ya usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre), inayotumia kuboresha huduma wanazozitoa katika jamii.
“Lakini pia si hivyo tu, tulionyesha uboreshaji wa huduma tunazozitoa kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya kisasa kupitia mfumo wa fiber ambao upitishaji taarifa mbalimbali kama vile mawasiliano na picha na hii inawezesha mfumo kuliona tatizo la mteja mara tu linapotokea na kuwezesha TANESCO kuchukua hatua haraka bila mteja kupata usumbufu.” Alisema Mhandisi Lutenganya.
Katika Kongamano hilo la mwaka huu lililofanyika Julai 28, (2017), kulikuwa na makundi matatu ya washiriki, ambayo ni shule za Sekondari, taasisi za elimu ya juu na mashirika ya umma ambapo waandaaji waliangalia uandaaji, uelewa wa washiriki pamoja na teknolojia ilivyotumika.
TANESCO ina wahandisi wanawake 55, na kuifanya taasisi ya kwanza nchini kuwa na idadi kubwa na wahandisi wanawake.
Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, alisema ni wajibu wa wanawake kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yao na kuachana na dhana ya woga.
“Fanyeni kazi kwa bidii na maarifa, na niwaambie, utendaji kazi wako ndio utamvutia MD afikie uamuzi wa kukupandisha cheo na sio jambo linguine lolote lile, mimi nitastaafu hivi karibuni, ninawaeleza haya kwavile ninajua umuhimu wa kujituma katika kazi na kujiamini.” Alisema Mhandisi Ngahyoma.Alionyesha kufurahishwa kwake, na angependa idadi ya wanawake viongozi katika Shirika hilo inaongezeka na kufikia sio asilimia 50 tu bali asilimia 75.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akiwa na Dkt. Mwinuka wakati akionyesha tuzo hiyo.

 Dkt. Mwinuka, akiwapongeza baadhi ya wahandisi hao.
 Dkt. Mwinuka akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.
 Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, akizungumza.

 Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
  Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.

MAHAKAMA KUSOGEZA MAFUNZO KWA WADAU WAKE

WAZIRI MWIGULU ATOA MWEZI MMOJA JWA BODAHODA KUNUNUA KOFIA NGUMU

$
0
0

****
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza waendesha bodaboda wote nchini kuhakikisha kuwa wanakuwa na kofia ngumu ‘Helmet’ ndani ya mwezi mmoja baada ya hapo hatua kali zitachukuliwa.

(PICHA NA HABARI ZIMEANDALIWA NA KADAMA MALUNDE)


ANGALIA PICHA ZA MATUKIO 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza na waendesha bodaboda na baiskeli 'daladala' leo mjini Shinyanga.Kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule.Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akiwasisitiza waendesha bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza.
Waendesha bodaboda na baiskeli mjini Shinyanga wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza na waendesha bodaboda na baiskeli.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akieleza namna jeshi la polisi linafanya ili kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Masanzu akisisitiza jambo wakati kikao hicho.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini,Mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akizungumza katika kikao hicho.
Kikao kinaendelea.
Mmoja wa waendesha akiuliza swali kwa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho.
Mkazi wa Shinyanga Mjini akieleza shida yake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba baada ya kikao kufungwa.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

BONDIA IDDI MKWELA ASEMA KAMOTE NA MFAUME MFAUME WANANIKIMBIA

$
0
0


Na Mwandishi Wetu


BONDIA Idd Mkwela baada ya kumsambalatisha bila ya huruma bondia Adam Ngange hivi karibuni amekuwa katika wakati mgumu wa kupata mapambano zaidi kwa kuwa mabondia wa nchini kwa sasa wanamkimbia

mana mpaka sasa nimepewa ofa ya kupambana na mabondia wawili tofauti ambao wananiogopa na naisi wameingia mitini kwa kipigo nilichotoa kwa Ngange

Mkwela alikwenda mbali zaidi na kuwataja mabondia Allan Kamote kutoka Tanga na bondia anaetamba kwa sasa Mfaume Mfaume kuwa wananikimbia kwa kuwa kazi yangu ninayo onesha nikiwa ulingoni ni zaidi yao hivyo nawaonya wakae wakijua siku nikikutana nao ama zao ama zangu

Mkwela anaenolewa na Sako Mwaisege 'Dungu' nae ametilia mkwazo kwa kuwataka mabondia hawo ambao kwa sasa awana tambo mbele ya mkwela kwani Mkwela ni moto wa kuotea mbali ata hivyo izo kazi zilikuja katika kambi yetu mara gafla tukasikia zimepeperuka yani wametukimbia

hata hivyo atuchoki tunaendelea kufanya mazoezi najua ipo siku wataingia katika anga zetu kwani awana ujanja wa kunikwepa bali wanachelewesha kupigana na sisi

Kocha Mwaisege aliongeza kwa kusema kuwa Mkwela katika viwango vya ubora nchini Tanzania kupitia mtandao wa Boxrec anashikilia namba mbili baada ya bingwa wa Dunia wa GBC  Ibrahimu Class 'King Class Mawe' hivyo najua watakuja tu kwa kuwa mimi ndio nipo juu zaidi yao

ukimwangalia Kamote yeye ni namba kumi na mbili hivyo nimempita mbali sana ana ujanja na sasa amechoka ngumi zimekwisha na sasa ni zamu yangu mimi kutamba akuna wa kuuzima moto wangu katika uzito wa lightweight kg 61  mimi ndie mtawala wa uzito huo hivyo wajipange sana vinginevyo wabadilishe uzito ili kujiepusha na kipigo nitakacho wapa alimaliza kusema Mkwela

DC KIBAHA ATOA MWEZI MMOJA WAVAMIZI WA MSITU WA DUTUMI KUONDOKA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama  ametoa mwezi mmoja kwa wavamizi wa eneo la hifadhi ya msitu wa Dutumi kuondoka mara moja ifikapo Oktoba 4 mwaka huu.

DC Assumpter amesema hayo baada ya kwenda kuutembelea msitu huo eneo la Tengefu la hifadhi lililopo katika Mkoa wa Pwani baada ya kupata taarifa kuwa kuna watu ambao wamevamia na wameweka makazi katika eneo hilo isivyo rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari  katika eneo hilo DC Assumpter  amesema kuwa ndani ya msitu huo kuna watu kutoka katika mikoa mbalimbali jumla ya wananchi 3,000 ambao wanaishi ndani ya msitu huo huku wakifanya uharibifu wa kukata miti hovyo na kuichoma kwa lengo la kufanya biashara ya kuchoma mkaa bila ya kuwa na vibali halali kutoka serikalini.
 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza na wakazi waliovamia eneo la hifadhi ya msitu wa Dutumi mara baada ya kukagua msitu huo na kukuta uharibifu mkubwa ndani ya Msitu huo.
 Mkuu wa Wilaya Assumpter akimshika mtoto mmoja wapo anayeishi  na wazazi wake kwenye kambi ya watu wanaokata misitu na kuchoma mkaa , hapo alikuwa akiwauliza wazazi hao kuwa hawawatendei haki watoto wao kwani ndani ya kambi hizo hakuna mahitaji muhimu kama hispitali, shule, maji safi  pamoja na malazi yenye hadhi ya kuishi binaadamu
Sehemu ya msitu wa Dutumi ambao umefyekwa miti yote mikubwa na wananchi waliovamia msitu huo


GROUP LA WHATSAPP LA AFYA YANGU LATOA MSAADA KWA WAJAWAZITO MLANDIZI MKOANI PWANI

$
0
0
 Msimamizi Mkuu wa Kundi la WhatsAPP la AFYA YANGU, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale (kushoto), akimkabidhi Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, vifaa vya kujifungulia wajawazito vilivyotolewa na kundi hilo kwa Kituo cha Afya cha Mlandizi jana. Kulia ni Mwanachama wa kundi hilo, Mudeme Elly.

 Msimamizi Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale (katikati), akitoa maelezo wakati akikabidhi msaada huo.
 Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya cha Mlandizi, Sahib Katyene, akitoa maelezo wakati akipokea msaada huo.
 Diwani wa Mlandizi, Euphrasia Kadala, akitoa shukurani 
baada ya kupokea msaada huo.
 Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, akizungumza wakati akipokea msaada huo.
 Wauguzi wa kituo hicho cha afya wakipiga makofi wakati wakipokea msaada huo.
 Vifaa hivyo vikipokelewa.



 Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, akimkabidhi vifaa hivyo Mganga wa Kituo hicho.
 Wauguzi wakipokea vifaa hivyo.



 Baadhi ya majengo ya kituo hicho cha afya.
 Picha ya pamoja.
 Vifaa vikipelekwa kuhifadhiwa.
 Ni furaha tupu baada ya kupokea msaada huo.
Waandishi wa habari wakibadilishana mawazo na Msimamizi Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulela.

Na Dotto Mwaibale, Kibaha

KUNDI la WathAssp la Afya yangu limetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 900,000 kwa ajili ya kujifungulia wajawazito kwa Kituo cha Afya cha Mlandizi mkoani Pwani.

Vifaa hivyo vilivyopokelewa na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa vilikabidhiwa katika kituo hicho huku tukio hilo likishuhudiwa na Diwani wa Mlandizi, Euphrasia Kadala na wauguzi wa hospitali hiyo.

Akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo Mbunge Jumaa alisema msaada huo umefika kwa wakati muafaka na utasaidia wajawazito katika hospitali hiyo.

"Msaada huu tulioupokea leo hii utawasaidia wajawazito wanaofika kujifungua katika kituo hiki tuna washukuru sana" alisema Jumaa.

Alisema yeye yupo katika makundi ya WathAssap 36 lakini hajawahi kuona yakitoa msaada kwa jamii kama lililofanya kundi hilo la AFYA YANGU ambapo alitoa ushauri kwa makundi mengine kuiga mfano huo.

Msimamizi Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale alisema kama kundi waliguswa na kusukumwa kusaidia katika eneo hilo kufuatia mafunzo ya afya wanayopata kutoka kwa wataalamu wa afya ambao ni wanachama katika kundi hilo.

"Katika kundi letu tuna madaktari ambao hutupa mafunzo kuhusu masuala mbalimbali ya afya ambapo kupitia mafunzo hayo tukasukumwa kuchangishana na kusaidiwa na wadau wengine na kuona tufanye hiki tulichokifanya" alisema Lulale.

Lulale alisema waliona ni vizuri msaada huo kuupeleka nje ya mkoa wa Dar es Salaam ambako wanaamini kunachangoto kubwa ya vifaa hivyo vya kujifungulia kwa wajawazito.

Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya cha Mlandizi, Sahib Katyene alishukuru kupata msaada huo kutoka katika Group hilo la WhatAssap na kutaka wadau wengine kuiga mfano huo.

Katyene alisema katika kituo hicho cha afya wajawazito 250 hujifungua kwa siku kwa njia ya kawaida huku wanaofanyiwa upasuaji wakiwa kati ya 20 na 25.

Alisema kutokana na hali hiyo licha ya serikali kutoa bure vifaa vya kujifungulia vifaa walivyokabidhiwa na kundi hilo vitasaidia kwa wajawazito wanaofika kujifungua katika kituo hicho.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
Viewing all 1902 articles
Browse latest View live