Quantcast
Channel: BONGOWEEKEND
Viewing all 1915 articles
Browse latest View live

TFF YAMFUNGUA PINGU HAJI MANARA NA WENZAKE

$
0
0

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefuta adhabu dhidi ya wanafamilia wanne waliofungiwa kushiriki masuala la soka kwa mwaka mmoja.

Wanafamilia hao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa, James Mwakwinya; Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Blassy Kiondo; Kaimu Katibu wake, Ayoub Nyaulingo pamoja na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.

Haji Manara alitiwa hatiani Aprili 23, mwaka huu kwa makosa ya lugha chafu na za chuki kwa viongozi wa TFF na kupotosha umma dhidi ya kadi njano ya mchezaji Mohammed Fakhi wa Kagera Sugar ambako alifungiwa kushiriki masuala ya mpira kwa mwaka mmoja na faini ya Sh milioni tisa.

Viongozi wa RUREFA walifungiwa kwa mwaka mmoja na faini ya Sh. milioni mbili kwa kila mmoja kwa makosa ya kukiuka maagizo ya viongozi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyotaka wasitishe mchakato wa uchaguzi mkoa kwa kuwa kulikuwa na rufaa iliyokatwa TFF.

Akizungumza na Wanahabari leo Julai 17, 2017 Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas, alisema viongozi hao wamesamehewa adhabu zao kwa kuwa waliomba kupitiwa upya kwa mashauri yao na kamati imeona ni bora kuwaachia huru ili kuendeleza masuala ya soka.

“Wapo wengi waliofungiwa wengine maisha na wengine adhabu fupi, msamaha huu ni kwa wale ambao wameomba tu kupitiwa upya kwa adhabu zao, pia milango ipo wazi kwa wengine ambao wanataka kupitiwa kwa mashauri yao, lakini si kwa wale waliopanga matokeo uwanjani,” alisema Tarimba.

Kadhalika, Tarimba aliwaomba viongozi wa TFF kuandaa semina ya Maofisa Habari na Viongozi wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ili kuepuka maneno machafu ambayo yanasababisha wao kufungiwa.

“Inaonekana viongozi na Maofisa Habari hawana maneno mazuri ya kuongea na wadau wa soka na ndio maana matatizo ya kufungiwa yanajitokeza mara kwa mara, naamini wakipata semina hiyo itawasaidia kujirekebisha na kupunguza kesi kama hizo,” alisema Tarimba.

Kwa niaba ya TFF, Ofisa Habari wa Shirikisho, Alfred Lucas, wameyapokea mapendekezo hayo kutoka kwa Tarimba na kwamba tutafanyia kazi ili kurekebisha makosa hayo kwa manufaa ya soka la Tanzania.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


BANK OF AFRICA YAKABIDHI RASMI MTAMBO WA UJENZI AINA YA GREDA KWA MTEJA WAKE

$
0
0
Naibu Mkurugenzi mtendaji wa BANK OF AFRICA TANZANIA Bw. Wasia Mushi akikabidhi mfano wa funguo kuashiria makabidhiano ya Greda kwa Mteja Bw. T Hitesh Vishram ambae ni Project Supervisor wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Limited, Katikati ni meneja wa masoko, Utafiti na maendeleo wa BANK OF AFRICA TANZANIA Bw. Muganyizi Bisheko.


BANK OF AFRICA hii leo imekabidhi rasmi mtambo wa ujenzi (Greda jipya aina ya JCB) lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300 kwa kampuni ya Dezo Civil Contactors Limited, kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo kandarasi ya ujenzi wa kuta kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi.

Makabidhiano ya mtambo huu ni sehemu ya mpango endelevu wa benki wa kununua na kukodisha mitambo (lease finance), ambayo inawawezesha wateja kujiongeza kiutendaji kwa kupata vifaa vya kisasa bila ya kulazimika kuwa na pesa taslimu za manunuzi ya vifaa hivyo.

Makubaliano haya ya ukodishaji wa mitambo yanaakisi katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi, usafirishaji, teknolojia ya habari na mawasiliano, utalii, madini, mafuta na gesi.

BANK OF AFRICA imebaini huu ni mpango ambao una tija kubwa kwa wajasiriamali wakubwa kwa wadogo, kwa ajili ya kufanikisha uendeshaji wa biashara zao ambao utaongeza uzalishaji na faida kubwa. Mteja kupitia mpango huu anapewa fursa pana ya kufanya chaguo lake bila kikwazo chochote na bila ya uhitaji wa amana ya awali au dhamana nyingine. Marejesho ni malipo ya ukodishaji ya kila mwezi na mteja ana uwezo wa kuchagua kua mmiliki wa mali husika pindi ifikapo mwisho wa mkataba wa ukodishaji.

Benki humsaidia mteja kuhakiki chombo anachotaka kuingianacho mkataba kama kina ubora ili kuweza kuinua uchumi wake na uchumi wataifa kwa ujumla.

BANK OF AFRICA ilianza shughuli zake Juni mwaka 2007, baada ya kuinunua Benki ya Euroafrican ambayo ilianza kazi Tanzania kutokea September 1995.

BANK OF AFRICA inafanya kazi katika mtandao wa benki za biashara katika nchi 18 zikiwamo nchi za Benin, Burkina Faso, Burundi, Cote d”ivoire, Djibouti, DRC, Ethiopia, France, Ghana, Kenya, Madagascar, Mali, Niger, Rwanda, Senegal, Tanzania, Togo na Uganda.

Kundi la Group BANK OF AFRICA lina makao makuu yake jijini Dakar, Senegal ikiwa na mtandao wa watu 500 wale wanaotoa huduma na sapoti kwa ofisi. Kuanzia mwaka 2010, Group BANK OF AFRICA ilimilikiwa kwa wingi wa hisa BMCE Bank, ambayo ni benki ya pili kwa ukubwa nchini Morocco.

BMCE Bank huleta mikakati mizito ya msaada wa uendeshaji katika kuunga mkono shughuli za BANK OF AFRICA Group, vilevile na muunganiko na ukaribu wa kufikia masoko ya kimataifa kutokana na uwepo wake katika nchi za Ulaya na Asia.

KUTANA NA TYRESE 'BANYE' AACHIA WIMBO WAKE BROWN COLOUR

$
0
0


Elias Banyenza nduo jina alilopewa na wazazi wake, lakini unafahamika na wengi kwa jina la Banye. Anapenda kuimba na RnB ndio muziki ana unaoupenda zaidi. Banye alianza kuimba akiwa Sunday Schools na Talent Shows lakini alivutiwa zaidi na Mwanamziki Tyrese tangu alipomuona mara ya kwanza kwenye Tangazo la Coca-Cola la mwaka 1986 na kujaribu kumfuatisha jinsi alivyoimba kila mara lile Tangazo lilipopita. 

Watu wengi wakimuona kwa mara ya kwanza huwa wanahisi kama waliwahi kumuona sehemu nahisi hii ni kwasababu waliwahi kuomuona kwenye sehemu zifuatazo:- Mwaka 2014/2015 alikuwa miongoni mwa wawashiriki 6 (Damian Soul,Grace Matata,Eli Daddy, Rogers Lucas, Myra) waliowakilisha Tanzania kwenye shindano la kuimba la Maisha Superstar nchini Kenya, kipindi hicho cha Tv kilirushwa na Maisha Magic ambapo walienda kushindana na washiriki wengine 12 kutoka nchi tofauti tofauti za Africa Mashariki, walisimamiwa na Shaa, AY(Tanzania), Jose Chameleon, Maurice Kirya (Uganda),Nameless, King Kaka(Kenya) na Music Director alikuwa Eric Wanaina. 

Mwaka 2015/2016, alikuwa kati ya washiriki 5 (Nandy, Jeff, Kechu na Zouccu) waliochagulia kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano makubwa zaidi ya Karaoke kuwahi kutokea Africa, Tecno Own The Stage Lagos nchini Nigeria, kipindi hicho kilirushwa na Africa Magic Showcase ambapo pia alishindana na waimbaji wengine 14 kutoka sehemu mbalimbali za bara la Afrika. Kwenye shindano hili walikuwa chini ya usimamizi wa Yemi Alade, MI, ID Cabasa (Nigeria), Bien Soul/Saut Sol, Anto Neosoul(Kenya) and AY (Tanzania) 
Ndoto yake kubwa alitamani atoke kimuziki kupitia Mashindano ya kuimba, lakini hakuweza kufanya vizuri huko kwa sababu alikuwa anafanya multitasking…ikiwemo Shule,Kazi na Muziki kwa wakati mmoja hivyo kumpelekea kufanya maandalizi ya zima moto.

Ukiachana na Muziki Banye amesoma Masters of Business Administration in Marketing na Bachelor in Mass Communication na kaspecilize kwenye Public Relations and Marketing. Na sasa kaamua kuingia studio na wimbo wake wa kwanza ni huo Brown Colour.

UONGOZI MPYA TAGCO WAKABIDHI USUKANI

$
0
0
 
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, (wapili kulia), akimkabidhi nyaraka za chama, Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Bw. Abdulm Njaidi. (wapili kushoto), ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi majukumu ya kiuongozi jijini Dar es Salaam Julai 20, 2017. Wengine pichani walioshuhudia hafla hiyo ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshughulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, (watatu kushoto), Bw. Gerald Chami, (wakwanza kushoto), ambaye ni Mweka Hazina Msaidizi na Bw.Peter Malinzi, (kulia), Mweka Hazina aliyemaliza muda wake.



NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
UONGOZI mpya wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), umekabidhiwa rasmi usukani wa kuongoza taasisi hiyo muhimu katika mawasiloiano ya serikali nchini.
Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam, Julai 20, 2017 ambapo Mwenyekiti wa TAGCO aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, alimkabidhi “nyenzo” za kufanyia kazi Katibu Mkuu mpya wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi, ambapo shughuli hiyo ilishuhudiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshuhulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, Mweka Hazina wa chama  hicho aliyemaliza muda wake, Bw. Peter Malinzi, Mweka Hazina Msaidizi Mteule, Bw.Gerald Chami.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekliti aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy alisema, “tunawakabidhi TAGCO, hiki ni chombo muhimu sana kwa mawasiliano ya serikali, hivyo hakikisheni mnakiongoza vyema ili maelengo kusudiwa yafikiwe,”.alisema Bw. Mungy.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi alisema, “Tunashukuru kwa kukabidhiwa usukani wa TAGCO, tunajua hiki chombo ni muhimu sana katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa taarifa sahihi za shughuli za Serikali yao inazofanya, tutatekeleza majukumu yetu kwa umakini na uaminifu mkubwa, tunaomba ushirikiano kutoka kwa uongozi uliopita na wanachama wote wa TAGCO na watendaji wote serikalini,”. Alisema Bw. Njaidi wakati akitoa neon la shukrani.
Viongozi wengine wapya wa TAGCO ni Bw. Pascal Shelutete (Mwenyekiti), Bi. Sarah Kibonde Msika (Makamu Mwenyekiti), Bi. Tabu Shaibu (Mweka Hazina), Bi. Gaudensia Simwanza (Katibu Msaidizi), Bw. Owen Mwandubya (Katibu Mwenezi) na Bw. Mpokigwa Mwakasipo (Katibu Mwenezi Msaidizi).
TAGCO nichama kinachowa kutanisha pamoja Maafisa Mawasiliano wa Taasisi mbambali za umma, serikali na Halmashauri zote hapa nchini, lengo likiwa ni kupena ujuzi na uwezo wa kuhakikisha taarifa za serikali zinawafikia wananchi kwa usahihi na kwa wakati.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, (wapili kulia), akimkabidhi nyaraka za chama, Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Bw. Abdulm Njaidi. (wapili kushoto), ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi majukumu ya kiuongozi jijini Dar es Salaam Julai 20, 2017. Wengine pichani walioshuhudia hafla hiyo ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshughulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, (watatu kushoto), Bw. Gerald Chami, (wakwanza kushoto), ambaye ni Mweka Hazina Msaidizi na Bw.Peter Malinzi, (kulia), Mweka Hazina aliyemaliza muda wake.



NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
UONGOZI mpya wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), umekabidhiwa rasmi usukani wa kuongoza taasisi hiyo muhimu katika mawasiloiano ya serikali nchini.

Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam, Julai 20, 2017 ambapo Mwenyekiti wa TAGCO aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, alimkabidhi “nyenzo” za kufanyia kazi Katibu Mkuu mpya wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi, ambapo shughuli hiyo ilishuhudiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshuhulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, Mweka Hazina wa chama  hicho aliyemaliza muda wake, Bw. Peter Malinzi, Mweka Hazina Msaidizi Mteule, Bw.Gerald Chami.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekliti aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy alisema, “tunawakabidhi TAGCO, hiki ni chombo muhimu sana kwa mawasiliano ya serikali, hivyo hakikisheni mnakiongoza vyema ili maelengo kusudiwa yafikiwe,”.alisema Bw. Mungy.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi alisema, “Tunashukuru kwa kukabidhiwa usukani wa TAGCO, tunajua hiki chombo ni muhimu sana katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa taarifa sahihi za shughuli za Serikali yao inazofanya, tutatekeleza majukumu yetu kwa umakini na uaminifu mkubwa, tunaomba ushirikiano kutoka kwa uongozi uliopita na wanachama wote wa TAGCO na watendaji wote serikalini,”. Alisema Bw. Njaidi wakati akitoa neon la shukrani.

Viongozi wengine wapya wa TAGCO ni Bw. Pascal Shelutete (Mwenyekiti), Bi. Sarah Kibonde Msika (Makamu Mwenyekiti), Bi. Tabu Shaibu (Mweka Hazina), Bi. Gaudensia Simwanza (Katibu Msaidizi), Bw. Owen Mwandubya (Katibu Mwenezi) na Bw. Mpokigwa Mwakasipo 
(Katibu Mwenezi Msaidizi).

TAGCO nichama kinachowa kutanisha pamoja Maafisa Mawasiliano wa Taasisi mbambali za umma, serikali na Halmashauri zote hapa nchini, lengo likiwa ni kupena ujuzi na uwezo wa kuhakikisha taarifa za serikali zinawafikia wananchi kwa usahihi na kwa wakati.

WAZIRI MAGHEMBE APOKEA MABILIONEA 28 SERENGETI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea 26 kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wa mapokezi yao jana kwa ajili ya ziara yao ya siku tatu nchini Tanzania.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi (katikati waliosimama) akizungumza na Mabilionea hao. Kulia kwake ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe .
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Mabilionea hao jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Alan Kijazi.

Kiongozi wa msafara wa Mabilionea hao, Perry Amber akizungumza wakati wa mapokezi hayo jana katika moja ya hoteli ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
Mabilionea hao kutoka taasisi ya Young Presidents Organisation (YPO) wakimsikiliza Waziri Maghembe.
................................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amewapokea Mabilionea 26 wa taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika Hifadhi ya Taifa  Serengeti kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.

Mabilionea hao ambao wanatoka katika mabara yote duniani wapo nchini Tanzania kama sehemu ya ziara yao katika nchi 8 duniani ikiwemo Uingereza, Rwanda, Maldives, Nepal, Bhutan na Rajastan.

Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake,  Prof. Maghembe aliwakaribisha Tanzania na kwenye Maajabu ya Dunia yanayobebwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Alisisitiza "hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivores) na wale wanaokula nyama (canivores) kama Serengeti". 

Prof. Maghembe aliwaeleza Wageni wake kuwa kuhifadhi ni gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia. Hivyo akawaomba wageni hao wawe mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo lenye  amani na vivutio vyenye ubora wa pekee. Hatua hiyo italeta watalii wengi na kuiongezea Tanzania mapato.

Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi unaokua kwa wastani wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.

(SOURCE: WWW.WIZARAYAMALIASILINAUTALII.BLOGSPOT.COM)

NAIBU WAZIRI DKT. KIGWANGALLA ATOA NENO KWA MAAFISA MAENDELEO NCHINI

NGO ZATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

IGP SIRO ALIPONGEZA JESHI LA POLISI SINGIDA

$
0
0

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akipiga saluti wakati wa paredi ya Polisi iliyoandaliwa lililoandaliwa kwa ajili yake kulikagua mapema leo kwenye viwanja vya kambi ya FFU mjini hapa.

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua baadhi ya askari wa jeshi la polisi mjini Singida leo piga saluti wakati wa paredi ya polisi iliyoandaliwa lililoandaliwa kwa ajili yake kulikagua. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada kukagua askari Polisi waliokuwa kwenye paredi kwenye viwanja vya kambi ya FFU mjini hapa.

Na Gasper Andrew

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amelipongeza jeshi la polisi Mkoani Singida kwa juhudi zake za kupunguza matukio ya uhalifu yakiwemo ya utekeji wa magari kwa kiwango kikumbwa.

IGP Siro ametoa pongezi hizo leo asubuhi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kweye viwanja vya kambi ya kikosi cha kuzuia fujo (FFU) mjini hapa.
Amesema matukio ya uhalifu mbalimbali mkoani Singida yamekupungua kwa kiwango kikubwa kwa sasa, ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

“Hatua hii inachangia uwepo wa amani na utulivu kwa wananchi wa mkoa wa Singida hivyo kutoa fursa kuweza kujiletea maendeleo yao ya mkoa na taifa kwa ujumla” amesema.

IGP Siro amesema mafanikio hayo yamechangiwa na wananchi kwa kiwanngo kikubwa kwa kutoa ushuirikiano kwa jeshi la Polisi.

Akifafanua amesema wananchi wamekuwa wakitoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa jeshi la polisi pindi wanapobaini dalili ama matukio ya kihalifu.

“Kwa sasa kwa kweli wananchi hata ninyi waandishi wa habari mnatupa ushirikiano mzuri sana
 Ushirikiano huu unachangia kazi zetu kuwa nyepesi na za mafanikio makubwa.
Sasa hivi kule Kibiti mkoani Pwani, wananchi wanatusaidia mno taarifa zinazohusu mauaji ya watu wasiokuwa na hatia”, amefafanua zaidi.

IGP Siro amesema kwa sasa Tanzania inaonewa wivu na nchi jirani kwa namna tulivyo dhibiti matukio ya kihalifu na kupelekea nchi kuendelea kudumisha amani na utulivu.

Wakati huo huo, Mkuu huyo wa jeshi la polisi ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi waendelee kushirikiana na jeshi hilo, kufichua baadhi ya watu wanaojihusisha na matukio mbalimbali ya kihalifu ili waweze kuchukulia hatua stahiki.

MABONDIA IDD MKWELA VICENT MBILINYI SELEMANI SIMBA NA ROLEN JAPHERT WAENDELEA KUNOLEWA NA SUPER D COACH UHURU GYM

$
0
0


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwiu nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimnowa bondia Idd Mkwela anaeijandaa na mpambano wake wa Agost 12 katika ukumbi wa Manyara Park uliopo Manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwiu nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimnowa bondia Idd Mkwela anaeijandaa na mpambano wake wa Agost 12 katika ukumbi wa Manyara Park uliopo Manzese Dar Es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS



Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Vicent Mbilinyi jinsi ya kupiga ngumi za mkunjo wa chini 'upcut' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Super D Uhuru GYM kariakoo Shule ya Uhuru Dar es alaam Picha na SUPER D BOXING NEWS


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wa pili kutoka kulia akiwa na mabondia Selemani Simba Vicent Mbilinyi na Idd Mkwela Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Idd Mkela na Rolen Japhert wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mazoezi yanayoiendelea katika kambi ya Super D Coach Uhuru GYM Shule ya Uhuru Kariakoo Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS


KAMBI YA SUPER D COACH UHURU GYM KARIAKOO 

BONDIA IDD MKWELA



SELEMAN SIMBA

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimnowa bondia Selemani Simba wakati wa mazoezi yanayo endelea katika kambi ya Super D Uhuru DGYM Kariakoo Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS

KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' KUSHOTO AKIWA NA MABONDIA SELEMANI SIMBA, VICENT MBILINYI NA IDD MKWELA BAADA YA MAZOEZI



ROLEN JAPHERT

SIMBA CHAWENE SEKTA YA KILIMO BADO NI MUHIMILI WA UCHUMI TANZANI

$
0
0
Na Mathias Canal, Lindi

Sekta ya Kilimo imetajwa kuwa bado ni muhimili wa uchumi wa Tanzania kwa kuwa inatoa ajira kwa asilimia  65.5  ya Watanzania na kuchangia zaidi ya asilimia 100 ya chakula hapa nchi katika miaka yenye mvua ya kutosha. 

Hayo yameelezwa na Waziriwa nchi ofisi ya Rais,tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, kwa mwaka huu wa 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, tarehe 1/8/2017.

Alisema Kaulimbiu ya Nane Nane mwaka huu inasema “Zalisha kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati”. Kaulimbiu hii inahamasisha Wakulima, Wafugaji na Wafugaji kuongeza uzalishaji na tija katika mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Mhe Simbachawene alisema kuwamwaka 2015, Sekta ya Kilimo ilichangia asilimia 29 ya pato la Taifa, na mwaka 2016 ilichangia asilimia 29.1. Hivyo, ni dhahiri kuwa mchango mkubwa katika pato la Taifa ulitokana na Sekta ya Kilimo ukifuatiwa na Sekta nyingine za kiuchumi. 

Alisema Kutokana na umuhimu huo, Serikali inaeendelea kutekeleza mikakati ya kuongeza kasi ya kukuza kilimo, mifugo na uvuvi ili kuchochea na kufikia uchumi wa viwanda sawasawa na Azma ya Serikali ya Awamu ya Tano. 

Alisema kuwaUzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2016 uliongezeka kufikia kiwango cha utoshelevu wa asilimia 123 ikiwa ni zaidi ya kiwango cha asilimia 120 cha mwaka 2015.  

Hali hiyo, imechangiwa na ongezeko la asilimia 6.7 la uzalishaji wa mazao ya nafaka yakiwemo mahindi na mchele. Usalama wa chakula pia unachangiwa kwa kiasi kikubwa na mazao yasiyo nafaka kama vile mihogo, viazi, ndizi na mazao ya jamii ya mikunde ambayo kwa ujumla kulikuwa na ongezeko la uzalishaji wa asilimia 1.5

Pamoja na kiwango cha kuridhisha cha uzalishaji wa mazao ya chakula, Mhe Simbachawene alisema kuwa hali mbaya ya hewa iliyojitokeza mwisho wa mwaka 2016 na mwanzoni mwa mwaka 2017 ilisababisha kupanda kwa bei za chakula katika maeneo mbalimbali ya nchi. 

Hata hivyo Katika kukabiliana na hali ya ukame uliotokana na uhaba wa mvua za vuli na kuchelewa kuanza kwa mvua za masika katika baadhi ya maeneo, hatua sitahiki zilichukuliwa. 

Amezitaja Baadhi ya hatua hizo kuwa  ni pamoja na kusambaza mbegu bora zinazokomaa kwa muda mfupi, zikiwemo mahindi, mtama na mpunga huku vipando vikiwemo pingili za mihogo na viazi vitamu vilisambazwa.

"Nchi yetu imebahatika kuwa na idadi kubwa ya mifugo ikiwemo ngómbe, kondoo, mbuzi, kuku wa asili na kuku wa kisasa. Pamoja na kuwa na idadi kubwa ya mifugo, viwango vya ulaji wa mazao ya mifugo hususani nyama, maziwa na mayai bado viko chini. Katika mwaka 2016, mifugo inayouzwa katika minada iliongezeka ukilinganisha na mwaka 2015 na hivyo kupata mapato yanayotokana na ng’ombe shilingi trilioni 1.34, mbuzi na kondoo shilingi trilioni 1.02" Alisema Mhe Simbachawene

Aliongeza kuwa Mapato yanayotokana na mauzo ya ngozi yalifikia shilingi bilioni 34.7 kwa ngozi ya ngómbe, shilingi bilioni 6.2 kwa ngozi ya mbuzi na kondoo. Mapato yanayotokana na uzalishaji wa malisho katika mashamba ya Serikali yalifikia shilingi bilioni 1.14. Aidha, mapato yanayotokana na uzalishaji wa mbegu za malisho bora ya nyasi  yalifikia shilingi milioni 55.8 na jamii ya mikunde shilini milioni 11.


Waziriwa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) akizungumza na Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
(Picha Zote na Mathias Canal) 
Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakimsikiliza kwa makiniWaziriwa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Waziriwa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB), Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb), na Mkuu wa mkoa wa MtwaraMhe Halima Dendego wakitazama namna ya uzalishaji samaki katika banda la JKT wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Waziriwa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (MB) akizungumza na Wadau wa kilimo hususani Wakulima, Wafugaji, sambamba na Wananchi wote kwa ujumla wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb) akizungumza kwa niaba ya Waziri waKilimo Mifugo na Uvuvi Mhe Dkt Charles Tizeba wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Mkuu wa mkoa wa MtwaraMhe Halima Dendego akitoa salamu za mkoa wa Lindi na Mtwara wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.

Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe William Tate Ole Nasha (Mb) akisisitiza jambo alipozuru katika ukumbi wa JKTwakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.
Waziriwa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe George Simbachawene (Mb) akionyesha moja ya mazao yanayozalishwa katika banda la JKT wakati wa  maadhimisho ya sikukuu ya wakulima - Nanenane, mwaka 2017 katika viwanja vya maonesho ya kilimo ya Ngongo Mkoa wa lindi, leo tarehe 1/8/2017.


MAONI YA WAKUU VYUO VYA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII

UMOJA WA ULAYA KUOKOA WASICHANA WASICHANA 3,738 KUKEKETWA NA NDOA ZA UTOTONI

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Jumla ya wasichana 3,738 wa Mikoa ya Mara na Geita wanategemea kunufaika na mradi wa Kuzuia Ndoa za Utotoni na Ukeketaji unaofadhiliwa na Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) na kuratibiwa na shirika la Plan International kwa kushirikiana na mashirika ya CDF, NELICO pamoja na Molly”s Network.


Takwimu hizo zimetajwa leo na Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Plan Tanzania, Gwynneth Wong wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika katika ukumbi wa ofisi za Umoja wa Ulaya Jijini Dar es Salaam. Bi. Gwynneth amesema kuwa mradi huo ni moja kati ya miradi inayoratibiwa na shirika hilo ikisaidiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha haki za wasichana zinalindwa na hakuna msichana atakaeachwa nyuma kwenye nyanja za maendeleo hali itakayopeleka wasichana kuwa na haki sawa na wavulana.

“Tumeona kuna haja ya kuweka mradi mwingine utakaodumu kwa miaka mitatu wa uzuiaji wa mimba za utotoni na ukeketaji kwa mikoa ya Mara na Geita kwani mikoa hiyo imeonekana kuongoza kwa matatizo hayo hivyo tunaushkuru Umoja wa Nchi za Ulaya kwa kutoa jumla ya shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kuendeshea mradi huu,”alisema Bi. Gwynneth.

Bi. Gwynneth ameongeza kuwa takwimu za mwaka 2016 za Utafiti wa Demographia na Afya unaonyesha kuwa ndoa za utotoni mkoani Mara ni asilimia 55 na kwa Geita ni asilimia 37 na ukeketaji kwa Mkoa wa Mara ni asilimia 32 kwa asilimia za kitaifa hivyo ni lazima kuanza na maeneo yaliyoathirika zaidi.


Kwa upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya, Roeland Van de Geer amesema kuwa umoja huo unatambua nafasi ya msichana katika jamii na nafasi ya baadhi ya mashirika yanayoshirikiana na Serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo kwa kuhakikisha haki sawa kwa wote.


“Sisi tunatoa fedha lakini nyie ndio watendaji hivyo tunawashukuru sana, lakini pia tunatakiwa tutambue kuwa maendeleo ya kudumu hayawezi kupatikana kwa kuwaacha wanawake nyuma kwa maana hiyo tunatakiwa tufanye juhudi za kuhakikisha tunaenda pamoja,” aliongeza Balozi Roeland Van de Geer.


Pia, Balozi huyo ameyashukuru baadhi ya mashirika yanayojitolea kufanya kazi ya kuhakikisha haki za msingi za binadamu zinalindwa na kuheshimiwa na ametoa wito kwa mashirika mengine kuendelea kusaidia maendeleo ya wasichana kwa sababu haki zao ndizo zinazovunjwa zaidi.


Mradi huo una malengo ya kuhakikisha wasichana wanaweza kuelewa haki zao na kuweza kutoa mawazo yao kwa jamii, kuhakikisha Serikali inasaidia wasichana kumaliza tatizo la ndoa za utotoni na ukeketaji.Kwa Mkoa wa Mara mradi utatekelezwa katika Wilaya ya Tarime ambapo utagusa jumla ya Kata tano na Geita mradi utagusa Kata 4.

STAR MEDIA YADHAMINI LIKI YA KIKAPU MKOA WA DAR ES SALAA

$
0
0



02/ 08// 2017

CHAMA Cha  Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA ) leo  kimemtambulisha  mdhamini  wa Ligi yake inayoendelea  ambaye ni Kampuni ya Star Media  atakaye dhamini gharama  zote  za uendeshaji wa Ligi hiyo inayoelekea ukingoni.

Akizungumza  katika mkutano na waandishi wa habari Mwenyekiti wa BD  Bwana  Ukeri Onesmo  mesema  wamefurahishwa na  udhamini  huo huku wakiwa na imani kwamba utaleta hamasa kwa wachezaji kwa ujumla.

Amesema  hivi sasa  BD wameweka mikakati ya  kuendesha  mchezo huo  kibiashara kwa kushurikiana na Taasisi mbalimbali huku lengo kuu likiwa kurudisha hadhi ya mchezo huo iliyopotea.

Ligi hiyo inatarajiwa kuingia kwenye hatua ya  mtoano  huku timu zitakazotinga  hatua ya fainali  itakayorindima Agosti 9   Mwaka huu Uwanja wa Ndani wa Taifa.



MAKONDA , RUGE, ALL STARS WANOGESHA SHEREHE ZA UWEKAJI JIWE LA MSINGI BOMBA LA MAFUTA CHONGOLIANI TANGA

$
0
0
 Wasanii nyota wa muziki wa kizazi kipya wanaounda kundi la Tanzania All Stars wakijiandaa kupanda jukwaani kutumbuiza kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Wasanii nyota wa filamu wa Bongo Movie wakiwa  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wamalize tofauti zao na kuweka maslahi ya nchi mbele wakati alipohutubia kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Baada ya kupatanishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba walishuka jukwaani bega kwa bega huku wakitabasamu.
 Kisha wakaelekea kwenye jukwaa la wasanii wa Tanzania All Stars
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martine Shigella  akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Naibu Waziri Mkuu wa Uganda Dkt Ali Kirunda Kivenjija akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba wakiwa jukwaani bega kwa bega huku wakiimba na Tanzania All Stars. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.  Ashatu Kijaji wakiwatuza Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakisubiri  kuwapa mikono wasanii wa Tanzania All Stars kwa kutumbuiza vyema  kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba la mafuta ghafi toka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Chongolieni kilicho nje kidogo mwa jiji la Tanga siku ya Jumamosi Agosti 5, 2016










































MABONDIA BAINA MAZOLA NA FRANSIC MIYEYUSHO KUZIPIGA AGOST 26 KINONDONI

$
0
0




Image may contain: 3 people
BONDIA BAINA MAZOLA 'SIMBA MAZOLA' KUSHOTO NA FRANSIC MIYEYUSHO 'CHICHI MAWE' KUSHOTO
Mwandishi Wetu
MABONDIA Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' na Baina Mazola 'Simba Mazola' wameingia mkataba wa makubaliano ya kuzipiga siku ya Agost 26 katika ukumbi wa Vijana uliopo Kinondoni Dar es salaam mabondia hawo ambao kila mmoja anatamba kumnyuka mwenzake

katika raundi za awali kwa kila mmoja
mpambano uho umekuwa na mashabiki wengi kila mmoja akijinasibu kumdunda mwenzake pande hizo mbili zinazotaka kujua nani zaidi ya mwenzie ni kambi ya Mazola ambapo anatokea kitongoji cha Mabibo ambapo kuna mabondia wengi upande uho 

uku Miyeyusho akitaka kuonesha ukongwe wake katika masumbwi na kusema yeye ni zaidi ya mabondia wote katika uzito wake

akizungumzia mpambano uho mratibu wa pambano ilo kaizirege jabiri dragon kaizum amesema mbali ya mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine mengi tu yatakayosindikiza siku hiyo

sajo bosco Jr atakumbana na juma rashidi mdobinaIssa Nampepecha ataoneshana umwamba na Abbas Mwamba wakati Karim Ramadhani ataoneshana kazi na Yohana Dhobian na Keisii Amali atakuchiana ngumi na Hashimu Chisola na Said Wigo atazipiga na Chicho Ramadhani

Mapambano haya yote yatasimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC ambayo yenye dhamana ya kuendesha mchezo wa ndondi za kulipwa nchini


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi

MAREFARII WA TPBC WAKUTANA NA MWAKYEMBE

$
0
0


Marefarii na majaji wa mchezo wa masumbwi nchini wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo Herrisson Mwakyembe wakati wa kumpongeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Marefarii na majaji wa mchezo wa masumbwi nchini wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo Herrisson Mwakyembe wakati wa kumpongeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA WAKULIMA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wakulima, wadau wa kilimo na wananchi kwa ujumla wakati wa kufunga maadhimisho ya sikukuu ya wakulima, (Nane nane) ambayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.(Picha zote na Mathias Canal)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kushoto) akijadili jambo na Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Lindi Mhe Salma Kikwete wakati alipotembelea Mabanda ya Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.

Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe Dkt Dk Charles Tizeba akisisitiza jambo kabla ya kufungwa kwa Maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi leo tarehe 8 Agosti 2017.

MGOMBEA KITI CHA URAIS TFF SHIJA ROBERT SHIJA AANIKA MIKAKATI YAKE

$
0
0

MGOMBEA wa nafasi ya Urais Shija Robert Shija mwenye shati jeupe na tai ya bluu, anayefuata kuli ni  Mwanahabari Muandamizi wa Kituo cha Azam TV na kutoka kushoto ni Mwanahabari kutoka gazeti la Nipashe Faustine Felicine na Khadija Kalili wa ITV ,Radio One jana Agosti 8 mwaka huu alianza  kampeni zake huku akitanabaisha mikakati yake endapo atafanikiwa kuingia madarakani .

Shija alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari  amesema soka ndiyo mchezo unaokusanya wapenzi wengi kuliko mchezo wowote nchini na Afrika Mashariki na Kati kwa ujumla na wadhamini wengi wangependa kutumia fursa hii kuwafikia wadau wao.
Alisema endapo ataingia madarakani ataweka mfumo rasmi wa kuendesha soka ili wadhamini waweze kuvutiwa kufanya uwekezaji katika soka.

Amesema akiwa madarakani ataanzisha kampeni ya kutoa elimu ya kutosha na kutoa kushawishi kwa wazazi kuwekeza na kuruhusu watoto wao wenye vipaji waingie kwenye michezo kwani ukweli ni kwamba mtoto mwenye kipaji anaweza kupata mafanikio katika maisha kwani kichezo inalipa kuliko kazi nyingine za kuajiriwa.

 Aidha amesema kuwa katika utendaji wake atahakikisha familia ya kichezo inaendeshwa kwa uadilufu na kuheshimu uhuru na mipaka ya kitaasisi bila kuingiliana kimaamuzi huku akisisitiza kuwa katika uongozi wake hautavumilia vitendo vya aina yoyote vya rushwa na ufisadi.

SIKU YA VIJANA DUNIANI KUFANYIKA MKOANII DODOMA: JENISTER MHAGAMA

SERIKALI YAFUTA UMILIKI WA VIWANDA AMBAVYO HAVIJAENDELEZWA

Viewing all 1915 articles
Browse latest View live