Quantcast
Channel: BONGOWEEKEND
Viewing all 1915 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSANI AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAAM

$
0
0
 Watoto wakikimbia walipokuwa wakiandamana kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kinyerezi, ambapo yalifanyika kimkoa wilayani Ilala, Dar es Salaam leo.Maadhimisho hayo yaliongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Maandamano yalielekea kwenye viwanja hivyo
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwashukuru na kuwapatia vyeti wauguzi wa kujitolea  walioshiriki kampeni kupima magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa watoto na vijana  wakati wa T
 WATOTO WAKIPIMWA UREFU
 Maandamano
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwasalimia watoto pacha Brighton na Bright Shirima alipokuwa akikagua mabanda ya tiba kwenye Tamasha la Uelimishaji na Upimaji Afya na Kinga dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoto na vijana wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika
 Kikundi cha hamasa cha Ilala kikihamasisha wakati wa maadhimisho hayo
 Brass Band ya Polisi ikiongoza maandamano 
 Makamu wa Rais Samia akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangala
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akihutubia 

 Kikundi cha ngoma cha Shule ya Msingi Umoja kikitumbuiza kwa ngoma ya kibati wakati wa maadhimisho hayo

 Kikundi cha Umoja kikitumbuiza kwa ngoma ya Makhirikhiri


 Makamu wa Rais, Samia akimkabidhi cheti cha shukrani DkNg'wege aliyekuwa mmoja wa madaktari walioshiriki kupma afya za watoto na vijana wakati wa maadhimisho hayo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akihutubia katika maadhimisho hayo.Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigangwala na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kote nchi kuwafichua watu wanaonyanyasa na kudhalilisha watoto kijinsia ili waweze kukamatwa na kuchukua hatua za kisheria kama hatua ya kukomesha vitendo hivyo ambayo vimeanza kushamiri katika baadhi ya jamii nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya kuhitimisha kampeni ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo ilitoa huduma bure za vipimo na matibabu kwa watoto na vijana zaidi ya 1500 kampeni ambayo iliambatana na maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika viwanja vya Shule ya msingi Kinyerezi mkoani Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema kuwa watenda maovu hao lazima vifichuliwe na wananchi, walezi pamoja na wazazi kwa kuwa watu wanaofanya vitendo hivyo vya udhalilishaji wa watoto wapo miongoni mwa jamii.

Katika kukabiliana na hali hiyo, Makamu wa Rais ameviagiza vyombo vya dola kutofumbua macho vitendo hivyo bali pindi wanapopata taarifa za matukio ya udhalilishaji wa watoto wachukue hatua za haraka za kuwakamata na kuwachukulia hatua stahiki watu wanaofanya vitendo hivyo vibaya.

Makamu wa Rais pia ametoa wito maalum kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kote nchini waache kuwaficha watu wanaotendea vitendo hivyo vibaya bali wawapatie taarifa walimu wao na polisi ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kwa kufanya hivyo watoto watakuwa salama katika mazingira ya nyumbani na wakiwa mashuleni kwani watu wabaya wanaofanya vitendo hivyo watawajibishwa kulingana na matendo maovu waliyokuwa wanawafanyia watoto hao.

“Mtoto anaweza kufaidika na fursa sawa iwapo tu atalindwa kwa kuwezeshwa kuwa afya bora”, Amesisitiza Makamu wa Rais.

Kuhusu kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameendelea kuua watu kwa kasi katika nchi zinazoendelea Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania.

Amesema ipo haja ya kuimarisha juhudi za kukabiliana na tatizo hilo kwa ushirikiano wa wadau wote kwani janga hilo linagharimu taifa na wananchi wake wakiwemo watu wazima, watoto na vijana.

“Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yasipodhibitiwa yatapunguza uzalishaji mali,ufanisi mahali pa kazi na hata shughuli za ulinzi na usalama nchini mwetu na hivyo pato la taifa litapungua na taifa kuwa watu maskini kutokana na magonjwa hayo”, Alifafanua Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kuwa katika kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza Serikali imeweza kupanua maeneo ya kutolea huduma kwa wagonjwa wa saratani nchini kwa kujenga jengo jipya katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na kuongeza majengo mapya ya huduma za saratani kwenye Hospitali za Rufaa ya kanda ya Bugando mkoani Mwanza.

Amesema Serikali pia imejenga Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambayo ni taasisi ya mfano ya kutibu maradhi ya moyo ambapo kutokana na kujengwa kwa taasisi hiyo Serikali imefanikiwa kuokoa mabilioni ya fedha ambayo yangetumika kuwagharamia wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamisi Kingwangala amemhakikishia Makamu wa Raia kuwa Wizara hiyo itaendelea kuweka mipango na mikakati imara ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza nchini.

Dkt Kingwangala ameomba wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kidini na wadau wengine kushirikiana na Wizara ya Afya katika kuongeza kasi ya kukabiliana na magonjwa hayo ili yasiendelee kuteketeza maisha ya watu nchini

NISHUSHE DAR LIVE IDD, WASANII WATAKAOLIAMSHA DUDE IDD MOSI

$
0
0
Mashabiki wakiwa ndani ya Dar Live.

Siku zikiwa zinahesabika kuelekea Usiku wa Nishushe Dar Live utakaofanyika Sikukuu ya Idd Mosi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo MbagalaZakhem jijini Dar, wakali kibao watakaoliamsha dude siku hiyo wamefungukia makamuzi watakayotoa. Katika usiku huo, pazia la burudani litafunguliwa rasmi mapema kuanzia saa 8:00 asubuhi ambapo burudani ya watoto itatolewa chini ya kundi la sarakasi na kudensi la Wakali Dancers pamoja na Kundi la Muziki wa Asili la Makhirikhiri kutoka Tanzania. Wakizungumza na Mikito Nusunusu kwa nyakati tofauti, wakali hao watakaoongozwa na R.O.M.A Mkatoliki walisema kuwa wataliamsha dude mwanzo mwisho sambamba na kutoa sapraizi kibao jukwaani. ROMA“Kwa muda mrefu sijafanya shoo tangu nipate matatizo hapa kati. Mara ya mwisho nilifanya shoo Dar Live nikiwa na Darassa ilikuwa Usiku wa Michano (Mkesha wa Mwaka Mpya) na waliofika waliona na ambao hawakufika walisimuliwa. Safari hii nisingependa ikupite hii. Nimepona na nipo fiti hivyo mje kwa wingi kushuhudia shoo yangu ya kwanza tangu mwaka huu uanze nikikinukisha kwa ngoma kali kuanzia Viva Roma Viva, K, Ivan, Kaa Tayari na nyingine kibao.” Darasa Mara ya mwisho kutinga Dar Live ilikuwa Mkesha wa Mwaka Mpya.
[/caption] DARASA“Mara ya mwisho kutinga Dar Live ilikuwa Mkesha wa Mwaka Mpya nikiwa na ngoma ya Taifa ya Muziki. Safari hii nakanyaga tena jukwaa hilo Idd Mosi nikiwa na ngoma nyingine ambayo nayo ni habari nyingine ya Hasara Roho. Sina maneno mengi; ‘Dunia iweke tuzo za wachukiaji, Bongo kuna watu wana vipaji, Utarusha madongo kwenye maji, Bora upige michongo utanipa midadi.’  
Mr Blue akiwapagawisha mashabiki wake.MR BLUE“Sikukuu hii ya Idd Mosi sehemu pekee ya kijanja ni Dar Live tu! Nitaliamsha dude na ngoma zangu zote kali kama Pesa, Mboga Saba, Baki Na Mimi na nyingine kibao. Muhimu mashabiki wajitokeze kumuona Byser mpya najua mnajua muziki wangu jukwaani upoje. Haina kukata pumzi hiyo!” STAMINA“Sina maneno mengi ila jukwaa linaongea. Battle za jukwaani kama kawa, mashabiki wajiandae kumsikia na kumuona Stamina akiwa na ngoma kibao mpya ikiwemo Love Me na siku hiyo ni mperampera mwanzo mwisho hadi kuchee.”
Snura Akifanya yake ndani ya Dar Live na wacheza shoo wake.[/caption] SNURA“Nina zawadi kibao za kuwapa mashabiki wangu Sikukuu ya Idd Mosi Dar Live. Mbali na kuwaimbia nitawaonesha live staili ya kucheza nyimbo zangu zote kuanzia Ushaharibu, Majanga, Chura, Najidabua, Shindu hadi wa sasa huu wa Nionee Wivu nilioimba na Yamoto Band.” BAMBO“Nitaliamsha kuanzia asubuhi mpaka mida ya jogoo akitoka bandani. Mkongwe niliyebaki katika uchekeshaji Bongo nitakuwepo kufanya yangu kwa watoto na wakubwa wote watakaofika Sikukuu ya Idd Mosi Dar Live.” ZANZIBAR STARS Mmoja wa wanaounda Kundi la Zanzibar Stars, Sabaha Mchacho alisema; “Zanzibar Stars itazaliwa upyaaa Idd Mosi Dar Live. Wapenda Muziki wa Mwambao hii si ya kukosa kwani tumewaandalia vibao vipya kabisaa kutoka kwa wakali wengi wakiwemo Bi. Mwanahawa, Jokha Kassim, Mosi Suleiman na Zubeda Mlamali MTONYO JE? Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo aliweka wazi kuwa licha ya uwepo wa wakali wengi, kiingilio kwa siku hiyo upande wa shoo ya kibabe itakayoanza saa 8:00 usiku kitakuwa kiduchu yaani shilingi 7,000 huku watoto kikiwa shilingi 3,000 tu na bonasi ndani yake ya kuteleza bure, kubembea bure, kupanda ndege bure, kuogelea bure na vingine vingi bureee. (STORI: MIKITO NUSUNUSU, RISASI JUMAMOSI)

NAFASI ZA KAZI ZATANGAZWA PPF

KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MAWIO KWA MUDA WA MIEZI 24

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROF. JUMANNE MAGHEMBE AMUAGA BALOZI WA UJERUMANI NCHINI ALIYEMALIZA MUDA WAKE

$
0
0
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Waziri Maghembe alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano na misaada mbalimbali aliyoitoa, yeye binafsi na nchi yake katika kusaidia kuendeleza sekta ya uhifadhi nchini.
Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (katikati) akifurahia zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori alivyopewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki.
 Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous mkoani Morogoro.
Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kulia) akimkabidhi Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe zawadi ya picha ya kumbukumbu ambayo ilipigwa wakati wawili hao wakitua kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Matambwe, Selous, Kwa mujibu wa balozi huyo siku hiyo haikuwa rahisi kwa ndege hiyo kutua kwa kuwa mvua zilikuwa zinanyesha. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)
 Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Juni, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Waziri Maghembe alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano na misaada mbalimbali aliyoitoa, yeye binafsi na nchi yake katika kusaidia kuendeleza sekta ya uhifadhi nchini.
Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (katikati) akifurahia zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori alivyopewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 juni, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.  Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 juni, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki.
 Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous mkoani Morogoro.
Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kulia) akimkabidhi Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe zawadi ya picha ya kumbukumbu ambayo ilipigwa wakati wawili hao wakitua kwa ndege katika uwanja wa ndege wa Matambwe, Selous, Kwa mujibu wa balozi huyo siku hiyo haikuwa rahisi kwa ndege hiyo kutua kwa kuwa mvua zilikuwa zinanyesha.
 (PICHA NA HAMZA TEMBA - WMU)

JPM AZINDUA MRADI WA KUUNGANISHA MATREKTA URSUS

VIPIMO BINAFSI VYA VIRUSI VYA UGONJWA UKIMWI KUFANYIWA UTAFITI NCHINI

MWANISPAA YA UBUNGO YAADHIMISHA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0
 Afisa Utumishi Mkuu Ally Juma Ally (Kushoto) akisikiliza maswali mbalimbali ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo wakati wa kikao cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. Kushoto kwake ni Yamo Wambura



 Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Mariam Maliwa akifatilia kwa karibu Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma


Afisa Utumishi Manispaa ya Ubungo Ndg Alute Joseph akitoa ufafanuzi wa kanuni za maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma

Leo June 20, 2017 watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wameanza kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano mkubwa uliohudhuriwa na watumishi wote wa makao makuu katika ukumbi wa Manispaa hiyo mkutano ambao umeongozwa na Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa hiyo Ndg Ally Juma Ally kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo.

Akiongea katika kikao hicho mara baada ya kufungua kikao Afisa Utumishi  mkuu aliwajulisha kuanza rasmi kwa wiki ya utumishi na kutoa utaratibu wa jinsi Halmashauri itakavyotimiza maadhimisho hayo ambapo alisema kuwa kwa wiki hii ya maadhimisho muda wa kutoka kazini utaongezeka kwa saa moja badala ya kutoka saa tisa na nusu mchana itakuwa ni saa kumi  na nusu, hali kadhalika alisisitiza mambo ya kuzingatia katika wiki hii na hata baada ya maadhimisho no pamoja na Kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni taratibu na miongozo mbalimbali ya utumishi wa umma, Kufanya kazi zetu kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, na Kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa bila ya viashiria vya kupokea rushwa au hongo katika kutoa huduma katika ofisi za serikali au umma.

Mengine ni Kuongeza Ari na kujituma katika kutekeleza majukumu yetu, Kufanya kazi kwa maarifa na kuwasikiliza wanaanchi wanapofika kupata huduma katika ofisi za umma/serikali na Kuweka vizuri kumbukumbu za wananchi watakaohudumiwa kwa kipindi hiki ili kuzitolea taarifa kwenye mamlaka husika.

Pia wamesisitizwa kutoa Huduma bora, Utii kwa serikali, Kuongeza bidii ya kazi, Kutoa huduma bila upendeleo, Kufanya kazi kwa Uadilifu, Uwajibikaji kwa Umma, Kuheshimu sheria na taratibu za kazi, na Matumizi sahihi ya Taarifa.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO


MKUU WAWILAYA UBUNGO KISARE MAKORI AFUNGUA MAFUNZO KWA WENYEVITI WATENDAJI WA KATA NA MITAA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielezea lengo la mafunzo muda mchache kabla ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Ubungo sambamba na Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati wa kufungua mafunzo ya siku nne ya kuwajenega uwezo Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaakwa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg Jmaes Mkumbo akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Mkuu wa Idara ya Mipango na Uchumi Manispaa ya Ubungo Ndg Yamo Wambura (Kulia) sambamba na Hosia Kivulenge wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati akifungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma Ally akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati akifungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Ubungo sambamba na Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati wa kufungua mafunzo ya siku nne ya kuwajenega uwezo Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaakwa.
Baadhi ya Watendaji wa Kata wakishangilia jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielezea lengo la mafunzo muda mchache kabla ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akifatilia kikao kabla ya kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori leo June 21, 2017 amefungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo kuhusu Mwongozo mpya wa mapokezi na Matumizi ya fedha za LGDG (Local Government Development Grant), Mpango wa fursa na vikwazo kwa maendeleo (O and OD-Oportunity and Obstacle to Development), Rushwa mahala Pa kazi, Ulinzi na Usalama, Na sheria ya Ardhi.

Mafunzo hayo pia yatahusisha masuala ya Utawala bora, Majukumu ya Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa, Pia kujifunza kuhusu historia na uhalali wa serikali za Mitaa, Sheria za uendeshaji wa Mamlaka za serikali za Mitaa, Muundo, Madaraka na Majukumu ya serikali za Mitaa, Mamlaka za serikali za Mitaa, Maadili ya viongozi wa Umma na Ulinzi na usalama katika maeneo ya kazi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe Makori alisema kuwa mafunzo hayo yanayotolewa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa mafunzo ulioidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Alimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yatatoa fursa kwa Wenyeviti na Watendaji wa Kata na Mitaa kuimarika katika nidhamu ya utendaji hususani kutekeleza mambo yaliyoainishwa kutekelezwa katika maeneo yao kwa maslahi ya wananchi.

Alisema kuwa mafunzo hayo yatatoa ufanisi wa uelewa mipaka na mamlaka katika utendaji jambo ambalo litawasaidia kuepuka migongano ya kimaslahi katika utekelezaji wa shughuli za uwakilishi wa wananchi pamoja na kusimamia utekelezaji wa shughuli za Halmashauri.

Aliongeza kuwa mada zote ziatakazotolewa itakuwa ni chachu ya kufungua ukurasa mpya kwa kuzingatia misingi ya utawala bora kwa kufuata miiko ya uongozi na kuongeza uadilifu katika utendaji kazi wa kila siku ili kufikia malengo yaliyoidhinishwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa lengo la mafunzo hayo yanayotolewa kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji Kata na Mitaa katika Manispaa ya Ubungo ni kuwajengea uwezo katika kutatua matatizo ya wananchi, kuwasilisha mawazo yao katika vikao vya kisheria, kuchambua sera na mikakati ya kutekeleza mipango mbalimbali, kutafuta ufumbuzi wa changamoto za wananchi katika maeneo yetu ya kusimamia majukumu yetu kikamilifu.

MD Kayombo alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuinua kiwango cha utendaji kazi kwa kuongeza stadi na maarifa ya uongozi ambayo yatachangia kuongeza tija na ufanisi katika shughuli zao ikiwa ni pamoja na kuondoa migogoro ya kila siku baina ya Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaa.


MWISHO
x
KAWAIDA...! MKUU WA WILAYA YA UBUNGO MHE KISARE MAKORI AFUNGUA MAFUNZO KWA WENYEVITI, NA WATENDAJI KATA NA MITAA Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielezea lengo la mafunzo muda mchache kabla ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Ubungo sambamba na Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati wa kufungua mafunzo ya siku nne ya kuwajenega uwezo Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaakwa. Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg Jmaes Mkumbo akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo Mkuu wa Idara ya Mipango na Uchumi Manispaa ya Ubungo Ndg Yamo Wambura (Kulia) sambamba na Hosia Kivulenge wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati akifungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma Ally akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati akifungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Ubungo sambamba na Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaa wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati wa kufungua mafunzo ya siku nne ya kuwajenega uwezo Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaakwa. Baadhi ya Watendaji wa Kata wakishangilia jambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielezea lengo la mafunzo muda mchache kabla ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kufungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akifatilia kikao kabla ya kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo Na Mathias Canal, Dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori leo June 21, 2017 amefungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo kuhusu Mwongozo mpya wa mapokezi na Matumizi ya fedha za LGDG (Local Government Development Grant), Mpango wa fursa na vikwazo kwa maendeleo (O and OD-Oportunity and Obstacle to Development), Rushwa mahala Pa kazi, Ulinzi na Usalama, Na sheria ya Ardhi. Mafunzo hayo pia yatahusisha masuala ya Utawala bora, Majukumu ya Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa, Pia kujifunza kuhusu historia na uhalali wa serikali za Mitaa, Sheria za uendeshaji wa Mamlaka za serikali za Mitaa, Muundo, Madaraka na Majukumu ya serikali za Mitaa, Mamlaka za serikali za Mitaa, Maadili ya viongozi wa Umma na Ulinzi na usalama katika maeneo ya kazi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mhe Makori alisema kuwa mafunzo hayo yanayotolewa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa mafunzo ulioidhinishwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Alimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yatatoa fursa kwa Wenyeviti na Watendaji wa Kata na Mitaa kuimarika katika nidhamu ya utendaji hususani kutekeleza mambo yaliyoainishwa kutekelezwa katika maeneo yao kwa maslahi ya wananchi. Alisema kuwa mafunzo hayo yatatoa ufanisi wa uelewa mipaka na mamlaka katika utendaji jambo ambalo litawasaidia kuepuka migongano ya kimaslahi katika utekelezaji wa shughuli za uwakilishi wa wananchi pamoja na kusimamia utekelezaji wa shughuli za Halmashauri. Aliongeza kuwa mada zote ziatakazotolewa itakuwa ni chachu ya kufungua ukurasa mpya kwa kuzingatia misingi ya utawala bora kwa kufuata miiko ya uongozi na kuongeza uadilifu katika utendaji kazi wa kila siku ili kufikia malengo yaliyoidhinishwa. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa lengo la mafunzo hayo yanayotolewa kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji Kata na Mitaa katika Manispaa ya Ubungo ni kuwajengea uwezo katika kutatua matatizo ya wananchi, kuwasilisha mawazo yao katika vikao vya kisheria, kuchambua sera na mikakati ya kutekeleza mipango mbalimbali, kutafuta ufumbuzi wa changamoto za wananchi katika maeneo yetu ya kusimamia majukumu yetu kikamilifu. MD Kayombo alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuinua kiwango cha utendaji kazi kwa kuongeza stadi na maarifa ya uongozi ambayo yatachangia kuongeza tija na ufanisi katika shughuli zao ikiwa ni pamoja na kuondoa migogoro ya kila siku baina ya Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata na Mitaa. MWISHO

WAZIRI MWAKYEMBE MSIMAMO WA MWALIMU ULIOKOA MENGI NCHI HII

STAMI A ,DARASSA KULIPELEKA JIJI DAR LIVE IDD MOSI

$
0
0
M
Rapper wa Morogoro, Stamina akifanya yake stejini. SIKU zikiwa zinahesabika kufi kiaSikukuu ya Idd Mosi, wakali kibao wa michano wakiongozwa na R.O.M.A Mkatoliki,Stamina,Darassa, Moni na wengineo wanatarajia kulipeleka jiji ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar na kufanya makamuzi ya kihistoria katika bonge la shoo lijulikanalo kama Nishushe Dar Live. Akizungumza na Uwazi Showbiz, Mratibu na Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mara ya mwisho kwa R.O.M.A kufanya shoo ilikuwa Dar Live na safari hii anarudi akiwa mpya ndani ya uwanja huo akiwa na sapraizi kibao katika shoo kabambe inayotambulika kama Nishushe Dar Live. “Tunajua kiu ya mashabiki wengi kumuona live R.O.M.A akikamua jukwaani na safari hii tena tumewaletea mtu wenu. Ni wakati kwa shabiki yeyote mpenda burudani kujitokeza na kukata kiu kwa shoo ya kihistoria ambayo ataliamsha dude msilolitegemea. “Kama mtakumbuka shoo yake hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya alikuwa katika michano mikali na msanii Darassa na mliona shughuli yake.
  Msanii wa Bongo Fleva, Darassa.

Safari hii anashuka kuchukua kijiji chake na kuondoka nacho,” alisema Mbizo. MSIKIE R.O.M.A MWENYEWE“Sijawahi kuwaangusha mashabiki wangu tangu nimeanza muziki. Siku zote ni mzee wa kuondoka na kijiji. Nitadondosha ngoma zangu zote kali kama Viva Roma Viva, K, Ivan, Kaa Tayari na nyingine kibao kikubwa njoo wewe na yule tujumuike pamoja na kumshuhudia R.O.M.A mpya nikiwa na ngoma mpya kwa mara ya kwanza tangu mwaka uanze,” alisema R.O.M.A. MR. BLUE YUMO! Mbizo aliongeza kuwa mbali na uwepo wa R.O.M.A siku hiyo jukwaa litapambwa na wakali wengine kibao wakiongozwa na Mr.Blue. “Wote tunamjua Mr. Blue anayebamba na nyimbo kibao kama vile Pesa, Mboga Saba na Baki Na Mimi. Mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia amshaamsha ambalo halijawahi kutokea popote.”  
Roma Mkatoliki akikinukishaSTAMINA WA MICHANO Darassa Kuhusiana na mkali mwingine wa michano, Stamina, Mbizo alisema kuwa safari hii Dar Live imejiandaa kutoa burudani kwa mashabiki wake wote kwa kuangalia wanataka nini na kwa kipindi gani hivyo katika sikukuu hii Stamina atawapa kinachostahili. “Stamina ni mmoja kati ya wakali wa michano wabishi na kila wakitoa ngoma huwa gumzo. Alishawahi kufanya michano na R.O.M.A katika shoo moja lakini hii ya safari hii itakuwa zaidi ya chana nikuchane kila mmoja akitambaa na biti la mwenzake,” alibonyeza Mbizo. Snura wa Chura Mbizo alimuongelea pia mkali wa nyimbo za mduara, Snura a.k.a Mamaa Chura au Mamaa Majanga kuwa atakuwa miongoni mwa wakata kiu kwa mashabiki wote watakaojitokeza Dar Live. “Chura zitakuwa za kumwaga na siku hiyo atakayepatia kucheza chura atapewa zawadi nono kutoka kwa Snura.”Msanii wa Bongo Fleva, Snura.[/caption] ZANZIBAR STARS KUIBUKA Baada ya kupotea kwa muda, kundi kongwe la Muziki wa Mwambao, Zanzibar Stars litaibuka kwa mara ya kwanza ndani ya Dar Live likiwa na vichwa hatari kama Bi. Mwanahawa, Sabaha Mchacho, Jokha Kassim, Mosi Suleiman, Ally Jay, Zubeda Mlamali na wengine kibao. 

 SHOO YA WATOTO SASA! 

 Mbizo aliongeza kuwa, mbali na shoo hizo pia pazia la burudani litafunguliwa Sikukuu ya Idd Mosi mapema kuanzia saa 2:00 asubuhi kwa kundi la sarakasi lisilo na mpinzani Bongo, Wakali Dancers pamoja na Makhirikhiri kutoka Tanzania pamoja na mchekeshaji anayebamba kunako kundi la Ze Comedy, Bambo ambao wataliamsha kwa kutoa burudani kwa watoto. “Kutakuwa na michezo mingi ya watoto kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea, kucheza ndani ya ndege na mingine mingi.” 

 MTONYO JE?
 Mbizo alimaliza kwa kutaja kiingilio kwa siku hiyo kuwa, burudani kwa wakubwa itakayoanza saa 2:00 za usiku itakwenda kwa shilingi 7,000 huku watoto ikiwa kiduchu cha shilingi 3,000. STORI: UWAZI SHOWBIZ SIKU

WAZIRI MWAKYEMBE AMTEMBELEA NA KUMJULIA HALI NAHODHA WA SERENGETI BOYS

JESHI LA POLISI LAUA WAHALIFU WANNE MKURANGA

$
0
0
Mkuu wa  Operesheni za Jeshi Polisi Kamishna ( DCP) Liberatus Sabas , akionyesha Bunduki aina ya  SMGzilizopatikana  juzi usiku wakati wa mapambano ya kurushiana risasi  baina ya wahalifu  na Polisi katika kijiji cha  Pagae Wilayani Kibiti   Mkoani  Pwani. Bunduki 2 aina ya SMG zilipatikana pamoja na Magazine  na Risasi 17.

 (Picha na Hassan Mndeme -Jeshi la Polisi ).

Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua wahalifu wanne wanaosadikiwa kuwa miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji katika mapambano yaliyodumu kwa zaidi ya nusu saa katika kijiji cha Pagae wilayani Kibiti mkoani Pwani.

Akielezea tukio hilo Mkuu wa Oparesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema tukio hilo lilitokea siku ya Alhamisi juni 29 majira ya saa tatu usiku kwenye barabara ya vumbi itokayo Pagae kuelekea Nyambunda ambapo Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita ambapo wahalifu hao baada ya kuona gari la Polisi walikimbilia vichakani na kuanza kuwarushia risasi Polisi.

Sabas alisema baada ya hali hiyo kutokea Askari nao kwa ujasiri walijibu na mapambano hayo yalidumu kwa zaidi ya nusu saa ambapo Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu wanne kwa risasi ambao baadaye walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.

“Katika tukio hilo tumefanikiwa kupata silaha mbili aina ya SMG na magazine mbili pamoja na risasi 17 zilizokuwa zinatumiwa na wahalifu hao na hii ni dalili kuwa tunaendelea vizuri na oparesheni yetu ambayo inashirikisha vyombo vingine vya ulinzi na Usalama katika wilaya hizi tatu za Mkuranga, Kibiti, na Rufiji” Alisema Sabas.

Aidha Sabas ametoa wito kwa wahalifu wengine kuacha mara moja kufanya vitendo hivyo kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kufanya jitihada zote za kuhakikisha kuwa maeneo hayo yanakuwa salama na wananchi wanaishi katika hali ya amani na usalama.

Vilevile amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana wahalifu wengine ili kuhakikisha kuwa kila mmoja anaishi kwa usalama ambapo kwa ambaye atakayetoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa wahalifu hao kiasi cha shilingi milioni kumi kitatolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Simon Sirro.

SHIRIKA LA POSTA LANG'ARA MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli (katikati), akimkabidhi Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa, Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam leo, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. Kulia anayesaidia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijsnge.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli (kulia), akimkabidhi Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa, Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo leo. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa (katikati), akiwa ameishikilia Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road jijini Dar es Salaam pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo, mara baada ya kukabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo leo. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa (wa tatu kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (wa tatu kulia), Tuzo ya Ushindi wa Kwanza kwa Mashirika yatoayo huduma katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, Viwanja vya Sabasaba, mara baada ya kukabidhiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, jijini leo. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deogratius Kwiyukwa (kushoto), akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Dk. Haruni Kondo (kulia), kwenye banda la shirika katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es Salaam leo.

PSPF WAKABIDHI MASHUKA 75 WODI YA WATOTO ZANZIBAR

$
0
0
Maafisa wa Mfuko wa PSPF kulia Faidha Khatau na Hazina Konde wakimkabidhi mashukaka Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Dr Ali Salum Ali anayefutia ni Mkurugenzi Utawala na Uendeshaji Dr. Abubakar Khamis Hamadi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa jengo jipya wa Hospitali ya Watoto Mnazi mmoja PSPF imekabidhi mashuka 75 kwa ajili ya wodi za watoto katika hospitali hiyo Kuu Zanzibar ikiwa ni moja ya kusaidia Jamii.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dr. Ali Salum Ali akipokea mashuka kutoka kwa Maafisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Hazina Konde (katikati) na Afisa Mkuu wa Tawi la Zanzibar PSPF Bi. Faidha Thatau wakikabidhi mashuka hayo kwa ajili ya matumizi ya Wodi ya Watoto katika hospitali ya Taifa ya Mnazi Mmoja Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika majengo mapya wa hospitali hiyo Zanzibar. 
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar Bi Faidha Thatau akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi mashuka kwa Uongozi wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Mfuko wa PSPF hutowa huduma za mafao mbalimbali kwa Wanachama wake Bima ya Afya kwa wateja wao.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar Dr. Ali Salum Ali akitowa shukrani kwa Uongozi wa Mfuko wa PSPF kwa msaada wao huo na kuwataka isiwe mwisho iwe ni endelevu kwa kutoa misaada mbalimbali kwa hospitali hiyo uwezo ukiruhusu.
Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF Bi. Faidha Khatau akigawa vipeperushi vya maelezo ya PSPF kwa viongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja kujuwa huduma zinazotolewa na Mfuko huo. 
Viongozi wa Hospitali ya Mnazi Mmoja wakifuatilia vipeperushi vya Mfuko wa PSPF baada ya kukabidhiwa kupata maelezo ya PSPF, wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mashuka kwa ajili ya Wodi ya Watoto Zanzibar.  
Afisa Mfawidhi Mfuko wa PSPF  Tawi la Zanzibar kulia Bi Faidha Khatau akimkabidhi mashuka Afisa Muunguzi katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Bi. Fatma Ali Mzee na kushoto Afisa Mfawidhi Msaidizi Bi Hazina Konde, wakiwa katika moja ya Wodi ya Watoto katika hospitali mpya ya Watoto Mnazi Mmoja.  
Maafisa Wafawidhi wa PSPF Tawi la Zanzibar wakitandika kitanda katika moja ya vitanda katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar baada ya kukabidhi mashuka hayo 75 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Watoto Zanzibar. 
Maafisa Wafawidhi wa PSPF Tawi la Zanzibar wakitandika kitanda katika moja ya vitanda katika Wodi ya Watoto Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar baada ya kukabidhi mashuka hayo 75 kwa ajili ya hospitali hiyo ya Watoto Zanzibar. 
Maafisa wa Mfuko wa PSPF Tawi la Zanzibar wakitoka katika jengo ya hospitali ya Watoto Mnazi Mmoja baada ya kumalizika kwa hafla ya kukabidhi msaada wa mashuka kwa ajili ya matumizi ya Wodi ya Watoto Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot.com.
Email othmanmaulid@gmail.com
Mobile.0777424152. 

KISARE AZINDUA BARAZA LA BIASHARA WILAYA YA UBUNGO

$
0
0
MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017

Wadau mbalimbali wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori Leo June 30, 2017 wakati wa ufunguzi wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo akimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017

Mwenyekiti wa TCCIA-Ubungo Ndg Clement Bocco akisikiliza hoja za wajumbe kwenye mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017

MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori (Kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo wakati mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017

Mwanasheria wa Manispaa ya Ubungo Ndg Merick Luvinga akifatilia mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017

MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori (Katikati) akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo na Mwingine ni Mwenyekiti wa TCCIA-Ubungo Ndg Clement Bocco, Leo June 30, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akimsikiliza kwa makini MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori kwenye mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017
Kushoto ni Afisa Utumishi Mkuu Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma Ally, Mwingine ni Mchumi Mkuu Manispaa ya Ubungo Ndg Yamo Wambura wakimfatilia kwa makini MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori kwenye mkutano wa wadau wa Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo, Leo June 30, 2017



Na Mathias Canal, Dar es salaam

MKUU wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori leo June 30, 2017 amezindua Baraza la Biashara la Wilaya ya Ubungo.

Akihutubiwa wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye Mkutano huo wa ufunguzi wa Baraza hilo uliofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Ubungo uliopo Kibamba CCM, Mhe Makori alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa Baraza la Biashara la Taifa ni uwezeshaji wa wananchi kiuchumi na serikali kwa kushirikisha wadau mbalimbali.

Katika uzinduzi wa Baraza la Biashara Wilaya ya Ubungo Wadau mbalimbali wameshiriki kutoka Sekta binafsi, Mashirika yasiyo ya kiserikali na watu binafsi kutumia fursa zilizopo katika mazingira yanayowazungumza kwa kuwezeshwa kiuchumi.

Mhe Makori alisema kuwa kupitia Mabaraza ya Wilaya wananchi wataongeza uwezo wao wa ubunifu na uzalishaji na biashara ambapo kwa uwezeshaji huo wananchi watafikia matarajio yao ya kuwa na maisha bora.

Alisema kuwa ili kufikia lengo hilo sera mbalimbali zimetekelezwa ikiwa ni pamoja na kupitishwa kwa sera na sheria namba 16 ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004, Kuundwa kwa baraza la Taifa la uwezeshaji kiuchumi mwaka 2015 na Uanzishwaji na uimarishwaji wa mifuko mbalimbali ya kuwezesha wananchi kiuchumi.

Alisema kuwa kutokana na upya wa Wilaya ya Ubungo ilitakiwa kuunda Baraza lake la Biashara likiwa chini ya Baraza la Mkoa na Taifa.

Mhe Kisare alisema kuwa Kuanzishwa kwa Mabaraza ya biashara ya Wilaya ni kuwa chombo cha mwanzo wa majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, Kuwa chombo cha kuratibu, kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa Programu mbalimbali za maendeleo ya wananchi kiuchumi.

Kuanzishwa kwa mabaraza ya biashara Wilaya itakuwa ni sehemu ya kupeleka mafanikio ya ukuaji uchumi mpana katika ngazi ya chini ya uchumi wa jamii kwa kuwahusisha wananchi katika majadiliano ya kuibua fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuzalisha ajira, kukuza kipato, kuongeza tija na kupunguza umasikini kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Wilaya.

Awali akizungumza kabla ya Kufunguliwa kwa Baraza hilo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa Baraza la Biashara la Wilaya lina wajumbe arobaini kutoka sekta binafsi na ya Umma, kila sekta ikiwa na wajumbe ishirini kutokana na nyadhifa, nafasi na ujuzi.

Kayombo aliongeza kuwa Baadhi ya wajumbe wanapangwa kwenye kamati/vikundi kazi kwa kuzingatia maeneo ya kipaombele yanayopaswa kufanyiwa kazi.

Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa Uzinduzi wa kuanzishwa kwa Baraza hilo ni utekelezaji wa agizo la kuanzishwa mabaraza ya Biashara ya Wilaya lililotolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Taifa Mhe Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano wa tano wa Baraza hilo Disemba 4, 2008 uliofanyika Jijini Dar es salaam ambapo alisisitiza uundwaji huo kusimamiwa na Mabaraza ya Mikoa na Taifa.

IMETOLEWA NA;
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO.


RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA RASMI MAONESHO YA 41 YA SABASABA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akipungia  mkono  wananchi  wakati  akitembekea  mabanda mbalimbali  baada yakufungua  rasmi  maonesho  ya 41 ya Biashara yaKimataifa  katika viwanja  vywa Mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam leo.Rasi  Magufuli ameyafungua rasmi maonyesho hayo  yaliyoanza Juni 28 mwaka huu yameongezewa siku tano zaidi   na kutarajiwa kumalizika Julai 13 mwaka huu.

(PICHA NA IKULU)

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AMUWAKILISHA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT.JOHN POMBE MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA AU

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemwakilisha Rais wa John Pombe Magufuli katika mkutano wa AU katika Makao Makuu ya Umoja huo Addis Ababa- Ethiopia.Mkutano umefunguliwa hii Leo Jijini Addis Ababa- nchini Ethiopia. 


Mkutano huo ukiendelea.

BONDIA IBRAHIMU CLASS ATUA NCHINI NA UBINGWA WA DUNIA

$
0
0


Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akiwasili nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere akiwa na mkanda wa ubingwa wa Dunia alioupata Ujerumani bunaotambuliwa na Global Boxing Council  'GBC' baada ya kumdunda Jose Forero kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS


Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akiwasili nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere akiwa na mkanda wa ubingwa wa Dunia alioupata Ujerumani bunaotambuliwa na Global Boxing Council  'GBC' baada ya kumdunda Jose Forero kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akiwasili nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere akiwa na mkanda wa ubingwa wa Dunia alioupata Ujerumani bunaotambuliwa na Global Boxing Council  'GBC' baada ya kumdunda Jose Forero kwa point kushoto ni bondia shabani kaoneka na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class ambae ni bingwa wa Dunia wa mkanda wa GBC katikati akiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini  Rajabu Mhamila 'Super D' wakati akiwasili na kanda wa ubingwa wa Dunia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius Nyerere na kupokelewa na baadhi na mashabiki pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi nchini  Picha na SUPER D BOXING NEWS 


Bondia Ibrahimu Class ambae ni bingwa wa Dunia wa mkanda wa GBC katikati akiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini  Rajabu Mhamila 'Super D' wakati akiwasili na kanda wa ubingwa wa Dunia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius Nyerere na kupokelewa na baadhi na mashabiki pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi nchini  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class ambae ni bingwa wa Dunia wa mkanda wa GBC katikati akiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini  Rajabu Mhamila 'Super D' wakati akiwasili na kanda wa ubingwa wa Dunia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius Nyerere na kupokelewa na baadhi na mashabiki pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi nchini  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akiwasili nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius nyerere akiwa na mkanda wa ubingwa wa Dunia alioupata Ujerumani bunaotambuliwa na Global Boxing Council  'GBC' baada ya kumdunda Jose Forero kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS

Kocha wa kimataifa wa mchezo w masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiteta jambo na bingwa wa Dunia wa Mchezo wa masumwi nchini Ibrahimu Class 

Bondia Ibrahimu Class ambae ni bingwa wa Dunia wa mkanda wa GBC katikati akiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini  Rajabu Mhamila 'Super D' wakati akiwasili na kanda wa ubingwa wa Dunia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius Nyerere na kupokelewa na baadhi na mashabiki pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi nchini  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class ambae ni bingwa wa Dunia wa mkanda wa GBC katikati akiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini  Rajabu Mhamila 'Super D' wakati akiwasili na kanda wa ubingwa wa Dunia katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius Nyerere na kupokelewa na baadhi na mashabiki pamoja na viongozi wa mchezo wa ngumi nchini  Picha na SUPER D BOXING NEWS
bondia Ibrahimu Class akiwa na ubingwa wake alipowasili


  1. bondia Ibrahimu Class akiwa na ubingwa wake alipowasili

MANISPAA YA UBUNGO KUANZISHA SHULE YA SHERIA

$
0
0
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo  John Lipesi kayombo akielekeza jambo wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na viongozi wengine wa shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na viongozi wengine wa shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwasalimu wanafunzi wa Shule ya Sheria Tanzania wakiwa darasani wakati alipozuru Chuoni hapo wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na viongozi wengine wa shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na viongozi wengine wa shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akisaini kitabu cha wageni wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na viongozi wengine wa shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akisikiliza maelezo mafupi kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo cha sheria Tanzania Dkt Willium Palanjo kuhusu changamoto ya ubovu wa barabara wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akizungumza na Viongozi wa Shule ya sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo akiwa na Viongozi wa Shule ya Sheria Tanzania wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)
Kushoto ni Rais wa serikali ya wanafunzi Shule ya sheria Tanzania Ndg Emmanuel Nyanza, Dkt Clement Mashamba muhadhiri shule ya sheria Tanzanai, na Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi na Zimamoto, wakati wa ziara ya kikazi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo ya kutembelea na kukagua barabara ya Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania)

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi kayombo Tarehe 6 June 2017 amekagua na kujionea hali ya ubovu wa barabara inayotoka Mawasiliano kuelekea Shule ya Sheria (Law school Of Tanzania) iliyopo katika Kata ya Sinza Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kutembelea barabara hiyo katika ziara yake ya kikazi huku akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Idara ya Ujenzi na zima moto Ndg Goodluck Mbanga, Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa matengenezo hayo yataanza hivi karibuni ili kurahisha huduma za kijamii kwa watumiaji wa barabara hiyo wakiwemo wananchi wa Mtaa wa Mawasiliano na Kata ya Sinza sambamba na wanafunzi wa Shule ya Sheria.

MD Kayombo alisema kuwa Fedha za matengenezo ya barabara hutolewa na Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) ambapo lengo kuu ni kuhakikisha kuwa barabara zinapitika muda wote.

Kiwango cha matengenezo kimefikia wastani wa asilimia 90 kwa matengenezo ya aina mbalimbali hususani ya muda maalumu (Periodic maintenance), sehemu korofi (Spot Improvement), matengenezo ya kawaida (Routine maintenance) na ujenzi wa makalavati huku kiwango kikubwa pia kikitolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami.

Mwanzoni mwa mwezi Februari serikali ilizitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanasimamia sheria katika utendaji wao wa kazi pamoja na kufanya kazi kwa uadilifu, kutumia weledi wa taaluma zao katika kusimamia suala la usafi wa mazingira,yakiwemo masuala ya kudhibiti biashara holela, uegeshaji wa magari holela na ujenzi holela.

Mkurugenzi Kayombo alisema kuwa barabara hiyo itakuwa na urefu wa kilomita 1.2 hivyo kuhudumia wananchi wengi ambao wanataabika kwa adha ya ukorofi wa barabara hiyo.

Viewing all 1915 articles
Browse latest View live