Quantcast
Channel: BONGOWEEKEND
Viewing all 1915 articles
Browse latest View live

NIMEFANYIWA UPASUAJI MARA TISA LAKINI BADO WATANZANIA NISAIDIENI

$
0
0
 
Habari Ndugu Mtanzania Mzalendo,Kwa majina Naitwa Exaud Mtei,Mwandishi wa Habari nchini Tanzania,kwa Masikitiko makubwa Imebidi niwe Balozi wa Kusambaza Ujumbe huu ambao nimeupata kutoka kwa mwalimu wa shule ya Kawe Ukwamani akinieleza Kuhusu maisha ya mwanafunzi wake wa Kidato cha Nne ambaye anashindwa kundelea na masomo kutokana na Matatizo yanayomkumba-

HUU NI UJUMBE WA MWALIMU HUYO--
HABARI KAKA-Kuna mwanafunzi wangu anaitwa Mariam Ibrahimu Mwema wa shule ya sekondari Kawe ukwamani kidato cha 4 mwenye umri wa miaka 16 tu ana matatizo makubwa ya tumbo. Alifanyiiwa opereshen ya kwanza  akiwa darasa la 3. Baadae  upasuaj uliendelea takriban mara 9.    
                   
Hali yake kiafya imezorota tena baada ya kuimarika katika miezi 2 Iliyopita kufuayia operation aliyofanyiwa pale Muhimbili .Ilikuwa ni operation ya kumi kwa huyu binti mwenye umri chini ya miaka 18                       
Dogo kwa sasa ni wa kutapika tu, tumbo limevimba tena na kitu kiumizacho zaidi ni kuwa FAMILIA YAKE IPO TAABANI KIUCHUMI KWA SASA...!                     Anaumwa kiukweli dogo hata kukaa hawez..!                       

Pleeeeease wadau hebu kila mmoja wetu afikirie nini anachoweza kumfanyia malaika huyu kunusuru kiza  kinene cha mustakabali wake kimaisha. Kiukweli wazazi wake wamefikia hatua ya kutokujua hatma ya mtoto wao kipenzi. 
                      
Wazazi hawana kitu imebaki ni kumtazama tu, mtoto Analia wazazi wanalia basi ni tafrani Inaumiza sana pale Mariam anapokuambia japo kama ingekuwa inawezekana basi yeye akupatie nafsi yake nawe umpatie yako japo kwa masaa 2 ( dakika 120) japo naye apumzike maumivu kwa muda huo.
  
Msaada unaohitajika kwa sasa ni Matibabu ya haraka nje ya nchi kwa mujibu wa maelezo ya madaktari. Na kwa msaada wa madaktari wa Tmj, Sanitas na Shree Hindumabdal hospital tulifanikiwa kupata mawasiliano, hospital na daktari ambaye alitupatia gharama za natibabu ya tatizo la mtoto wetu sambamba na gharama nyingine kuwa ni takriban dola elfu nane ( 8000) za marekani.                
    


Please wadau hata kwa kuwashirikisha watu wengine na taasisi mnazozifahamu tumnusuru huyu MALAIKA...!  SANAHANI KWA MAKALA NDEFU. NI MIMI MWALIMU MLEZI WA MARIAMU IBRAHIMU MWEMA. Kwa mawasiliano zaidi piga namba hii ya mama yake 0685379888 ASANTENI 
                      
Picha nilizoambatanisha ni Picha za Mariamu Ibrahimu Mwema siku chache kabla ya upasuaji kwa mara ya kumi.!

TUUNGANE KUSAMBAZA UJUMBE HUU NA KUMCHANGIA KWA HALI NA MALI KUFANIKISHA SWALA HILI

Kwa mawasiliano Zaidi—

Mama wa Mtoto -0685379888

Mwalimu wa mtoto huyo Kawe Ukwamani- 0683916283

Au ukihitaji Zaidi Kuwasiliana na Msambaza Ujumbe huu ni 0712098645



ASANTEN TUSAIDIANE KUOKOA UHAI WA MTOTO MARIAM.
Mariam Ibrahimu Mwema wa shule ya sekondari Kawe ukwamani akiwa amelala Kitandani,anahitaji msaada wa Watanzania wote kwa sasa.

BONANZA LA KWAYA ZA VIJANA KUTOKA KWAYA MBALIMBALI LAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Kikosi cha kwaya ya Usharika wa Mabibo (waliovaa jezi za Dark Blue) na kwaya ya Usharika wa Kinondoni (waliovaa jezi nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi kuanza
Mpira ukiwa unaendelea ambapo kwaya ya Kinondoni waliibuka kuwa washindi
Baadhi ya wanakwaya pamoja na watumishi wa Sharika mbalimbali za Moravian jijini Dar wakiwa wanatazama Mpira
Mchezo wa Netball ukiendelea ambapo walikuwa wanacheza kwaya ya Usharika wa Mabibo na Uhuru ambapo kwaya ya Mabibo waliibuka washindi.
Kwaya ya Amani kutoka Usharika wa Mabibo wakifurahia ushindi baada ya kuibuka Videdea kwenye mchezo wa netball
Mpambano mwengine uliokuwa wakukata na shoka kati ya Kwaya ya Usharika wa Uhuru na Mabibo ambapo Mabibo waliibuka washindi
Hapa ni mashindano ya kukimbia kwa wanawake
Mashindano ya kukimbia kwa wanaume hapa watu walichomoka balaa
Hapa ilikuwa ni mashindano ya kukimbia na majunia ambapo ngoma ilikuwa nzito kweli lakini walioweza waliibuka kidedea
Hapa ilikuwa sasa kufukuza kuku ambapo baada ya purukushani akapatikana mshindi ambaye ndiye anaonekana hapo akifurahi.
Mshindi wa Kukimbiza Kuku Bw. Lewis kutoka Usharika wa Kinondoni akiwa amekabidhiwa zawadi yake ya Kuku.
Mshindi wa kukimbia na Majunia Bi. Emmy kutoka Usharika wa Uhuru akikabidhiwa nishani yake na katibu wa kwaya ya vijana kutoka usharika wa Mabibo.
Huyu dogo anaitwa Afsa ndiye aliibuka mshindi wa riadha kwa upande wa wanawake
Mshindi kwa kukimbiza upepo kwa upande wa wanaume Adam ajichukua zawadi yake
Washindi wa Mpira wa Miguu kutoka Usharika wa Kinondoni wakikabidhiwa kombe lao
Kwaya ya vijana kutoka Usharika wa Mabibo wakikabidhiwa kombe lao baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa Netball

Picha zote na Fredy Njeje

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUUNGA MATREKTA YA URSUS

SERIKALI KUFUTA TOZO 108 KATIKA KILIMO ,MIFUGO NA UVUVI

SERIKALI YAIHAKIKISHIA SEKTA BINAFSI KUENDELEA KUPATA MIKOPO

ZIFF KUBORESHA SOKO LA FILAMU

$
0
0

ZIFF KUBORESHA SOKO LA FILAMU

Na Husna Saidi MAELEZO

Filamu 23 za Kitanzania zimefanikiwa kushinda kinyang’anyiro cha filamu bora 132 zitakazoonyeshwa katika tamasha la Nchi za Jahazi linalotarajia kufanyika Zanzibar kuanzia tarehe 8-16 Julai Zanzibar.

Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi wa Tamasha hilo Fabrizio Combolo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo ambalo linatarajia kushirika mataifa 70 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Combolo alisema filamu zinazotarajiwa kuonyeshwa katika tamasha hilo ni filamu ndefu, filamu makala, filamu katuni na kwa mara ya kwanza Nchi ya Namibia imeweza kutayarisha filamu pamoja na filamu ya Winnie iliyotayarishwa kutoka Afrika Kusini.

“Kutakuwa na makala kutoka Afrika ya Kusuni yenye jina la Winnie ambayo itazungumzia maisha ya Winnie Mandera na kwa Tanzania kutakuwa na filamu yenye jina la Kiumeni ambayo imeshaanza kuonekana katika majumba ya sinema hapa nchini.

Alisema kutokana na kukua kwa soko la filamu nchini, tamasha hilo kwa mara ya kwanza litaziduliwa na filamu ya Kitanzania ya T-Junction, iliyotayarishwa na Amil Shivji, jambo ambalo ni tofauti na huko nyuma ambapo walikuwa wanazindua na filamu kutoka nje ya nchi.

Aliongeza kuwa tamasha hilo pia litakuwa na filamu ya makala maalum ya maisha ya Mwanamuziki wa Marekani, marehemu Winnie Hauston filamu iliyoandaliwa na Mtunzi Nick Bloomfield. Aidha Tamasha hilo pia litaweza kuonyesha filamu ya makala maalum ya Ujangili iliyorekodiwa hapa nchini ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanyamapori.

Kwa upande wake Afisa Habari na Masoko wa tamasha hilo Lara Preston alisema kuwa kwa mara ya kwanza wameamua kuwa na soko filamu litakalofanyika ndani ya ukumbi huo ili kutoa hamasa ya kukuza tasnia ya filamu katika Afrika Mashariki.

Nae Mwenyekiti wa Mfuko wa Emerson, Said Elg alisema kuwa wapo tayari kushirikiana na ZIFF katika kunyanyua soko la filamu hivyo katika tamasha hilo watatoa tuzo kwa washindi na kwa wanafunzi 15 kutoka vyuo vya filamu watakaofanya vizuri.

Tamasha hilo litahusisha tuzo mbalimbali ambazo ni:-Tuzo za nchi za Jahazi, Tuzo za Sembene Ousmane, Tuzo za filamu bora ya Afrika, Tuzo za Adiaha, Tuzo za filamu bora kwa wanawake, Tuzo za filamu bora ya Kimataifa, Tuzo za Zanzibar Emerson na Tuzo ya video ya mwanamuziki bora wa Afrika Mashariki.

RC MAKONDA AKABIDHIWA MWENGE WA UHURU

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul C. Makonda (Kushoto) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi (Kulia) katika dhifa ya Makabidhiano iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi  iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo  John Lipesi Kayombo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Ndg Stephen Katemba Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni Theresia Mmbando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo  James Mkumbo wakifatilia dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Lipesi Kayombo (Kushoto) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happi wakijadili jambo katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya UbungoJohn Lipesi Kayombo (Kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo  Kisare Makori (Kulia) wakifatilia dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Wananchi waliojitokeza kuulaki Mwenge wa Uhuru katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul C. Makonda (Kushoto) akizungumza jambo na Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Simon Sirro katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi  iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com  Mathias Canal akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Rukia Muwango katika dhifa ya Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Mkoani Lindi iliyofanyika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma. Leo Mei 27, 2017.
Muonekano wa Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam ukitokea Mkoani Lindi.
Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda Leo Me 27, 2017 amekabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi katika dhifa ya makabidhiano iliyofanyika katika eneo la Kongowe Shule ya Msingi Kongowe/Mzinga kata ya Tuangoma na kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke tayari kwa kumulika miradi ya Maendeleo.

Mara baada ya kukagua Miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Temeke Mwenge wa Uhuru utazuru katika Wilaya ya Kigamboni Tarehe 28/05/2017, Siku ya Tarehe 29/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ilala, Tarehe 30/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Kinondoni na Tarehe 31/05/2017 utakimbizwa katika Wilaya ya Ubungo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amesema kuwa Mwenge wa uhuru ni chombo kilichoasisiwa na baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni Tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika hivyo kuzuru katika Mkoa wa Dar es salaam itakuwa ni kichocheo kikubwa katika kuhamasisha Maendeleo, Uzalendo, Umoja , Mshikamano na kudumisha Amani ndani na nje ya Taifa letu.

Mhe Makonda alisema kuwa Mwaka huu utakuwa mwaka wa 24 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zirejeshwe chini ya utaratibu wa usimamizi wa serikali kutokana na mabadiliko ya kidemokrasia baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

Katika mapambano dhidi ya Dawa za kulevya Mhe Makonda alisema kuwa jitihada ya kudhibiti kusambazwa na Matumizi ya Dawa za Kulevya ni kuifanya kuwa ajenda muhimu kiutekelezeji kwa mustakabali wa maisha ya watanzania kwa kuwa Jambo hilo linagusa nguvu kazi ya Taifa.

Rc Makonda amebainisha kuwa jumla ya Miradi 40 itapitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2017 katika Mkoa wa Dar es salaam ikiwa na  thamani ya Shilingi Bilioni 244,392,530,334 ambapo Miradi 12 itazinduliwa, Miradi 15 itawekewa mawe ya Msingi, Miradi miwili itafunguliwa na Miradi 11 itatembelewa.

Mhe Makonda amewapongeza wananchi wa Mkoa wa  Dar es salaam kwa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili huku akitoa wito kwa Wakazi wa Manispaa ya Temeke, Kigamboni, Ilala, Kinondoni na Ubungo kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote utakapozuru kwani pamoja na mambo yote Mwenge wa Uhuru ni urithi na nembo ya umoja katika maendeleo yetu.

Awali akizungumza kabla ya kukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey Zambi amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa weledi wake katika utendaji hususani katika kudumisha amani na kuchagiza ukuzaji wa uchumi wa nchi kwa kutilia msisitizo uwajibikaji serikalini, Kukemea wizi na Ubadhilifu wa Mali za umma sambamba na Mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya.

Mhe Zambi alisema kuwa Wananchi wanapaswa kumuunga mkono Rais Magufuli katika mapambano dhidi ya wizi wa Mali za Watanzania hususani Vita  ya kiuchumi aliyoianza hivi karibuni kwa kuzuia Mchanga wa dhahabu kusafirishwa kwenda nje ya nchi. 

Mhe Zambi ametoa pongezi hizo kutokana na maamuzi yaliyofanywa na Rais Magufuli mara baada ya kupokea Ripoti ya kamati iliyokuwa inachunguza Hatma ya mchanga wa madini iliyoundwa na Rais Magufuli Machi 29 mwaka huu ikiwajumuisha Profesa Abdulkarim Hamisi Mruma (Mwenyekiti), Profesa Justiania Rwezaura Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dokta Yusuph Ngenya, Dokta Joseph Yoweza Phili, Dokta Ambrose Itika, Mohamed Zengo Makongoro na Hery Issa Gombela.

Mwenge wa Uhuru utamaliza mbio zake mkoani Dar es salaam siku ya tarehe 31/05/2017 na kukabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Pwani siku ya tarehe 01/06/2017 katika Uwanja wa kimataifa wa  Mwalimu Julius Nyerere Terminal 1 kwa ajili ya kuelekea Mafia .

UNESCO, GPF WAWAJENGEA UWEZO CHUO CHA MWL. NYERERE

$
0
0
Muandaaji wa Semina hiyo iliyofanyika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere  na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Frank Joash akieleza namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Vijana kutoka Maeneo mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yanazungumziwa wakati wa semina hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Kigamboni
Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Nelson akieleza namna viongozi katika sekta mbalimbali wanavyoweza kusaidia kudumisha amani katika Jamii.
Mshauri wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi   Anthony Luvanda akitoa masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali.
 Mwakilishi kutoka Raleigh Alice Norbert akitoa maelezo namna ya vijana ambavyo wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea katika Asasi mbalimbali za Kiraia pia alielezea fursa zinazotokana na kujitolea
Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana jinsi ya kupata 'Scholarship'  zinazotolewa sehemu mbalimbali, na kuwasihi kuwa wasikate tamaa kwa kuwa kuna nafasi nyingi za kusoma nje ya nchi.
 Charles Ndiku akiwaelekeza vijana namna mbalimbali ambazo zinaweza kuwasaidia kupata ajira,na aliwasisitiza ili waweze ishi kwa amani yawapasa kuishi maisha bora ikiwa ni pamoja na kuwa na kipato endelevu.
Mwenyekiti wa programu kutoka Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam William Peter akieleza namna vijana wanavyoweza kubadili mitazamo na kuwa na mawazo chanya ya maendeleo
 Vijana mbalimbali wakichukua yale yaliyokuwa ya Muhimu
 Vijana wakiwa wananyoosha mikono ishara ya kuonesha kuwa wameelewa vizuri kwa yale yote waliyoyasikiliza
 Vijana wakiwa wanasikiliza kwa Makini.
Semina ikiendelea
Picha ya Pamoja
Picha zote na Fredy Njeje

"Kiongozi bora ni pamoja na yule ambaye anahakikisha kuwa kuna amani katika eneo la kazi na watu anaowaongoza" hayo yalisemwa na bwana Nelson aliyekuwa mwakilishi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) Nchini Tanzania  wakati wa semina ya vijana katika kushiriki programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Global Peace Foundation Tanzania. 

Alisema kuwa kiongozi makini ni yule anayehakikisha kuwa kuna amani katika eneo la kazi na kuwafanya wafanyakazi wake waishi kama familia moja ili kuondoa migogoro mbalimbali ambayo inaweza ikazuirika.

"Amani inatakiwa kudumishwa kuanzia ngazi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla" alisema Nelson na kuongeza kukosekana kwa amani kunaweza kusababisha  maafa kama vifo kwa sababu ya vita pia uchumi kuyumba kutokana na watu kuhofia kufanya shughuli za kimaendeleo kwa sababu ya machafuko.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa uelewa ili wapate kujiunga.

Nae  Bw. Jackson Oganga ambao walishawahi kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili ‘Scholarship” walielezea kwa kina namna walivyo fika huko, changamoto na jinsi zinavyotokea na kuwasihi vijana hao kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi hizo mpaka pale watakapo fanikiwa nao kutimiza ndoto zao za kwenda kusoma nje.

Mwisho Mshauri na mwezeshaji katika mambo mbalimbali ya Bw. Anthony Luvanda aliwasihi vijana kujitambua na kufahamu vipaji vyao na kujua namna ya kutimiza ndoto zao, ambapo aliwaomba pia vijana wasitegemee sana kazi za kuajiliwa bali wawe na mawazo chanya ili kuweza kutimiza malengo yao

Semina hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya vijana 180, kutoka vyuo vikuu vya Mwalimu Nyerere,CBE, TIA, Bagamoyo, Kampala International University  na St. Joseph, wanavyuo waliomaliza pamoja na vijana .

MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI SIMBA

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu rambirambi kwa Rais wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Evans Aveva kutokana kifo cha shabiki wa timu hiyo, Shose Fideline aliyefariki dunia jana mchana Mei 28, 2017 katika ajali ya gari.

Kadhalika, Rais Malinzi ametuma salamu za pole kwa majeruhi katika ajali hiyo akiwamo Nahodha wa Simba, Jonas Mkude na dereva wa gari hilo ambalo lilikuwa safarini kurejea Dar es Salaam kutoka Dodoma. Wanafamilia kadhaa wa mpira wa miguu walikuwa Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita kushuhudia mchezo wa fainali za Kombe la Azam - ASFC (Azam Sports Federation Cup HD 2016/17) uliozikutanisha timu za Simba na Mbao FC ya Mwanza.

Mbao ilifungwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa dakika 120. Gari lililopata ajali ni aina ya Toyota Land Cruiser V8 lilianguka na kuzunguka mara kadhaa na baadaye kutulia katika eneo la Dumila mkoani Morogoro baada ya tairi yake ya nyuma kupasuka hivyo kumshinda dereva na kupoteza mwelekeo kutoka barabara kuu.
“Nakuandikia Rais wa Simba, Evans Aveva, pia ndugu, jamaa na marafiki pamoja na majirani wa marehemu Shose Fideline na wanafamilia wengine wa mpira wa miguu, kwamba nimepokea taarifa za ajali ya gari iliyosababisha kifo cha mmoja wa mashabiki wa timu ya Simba kwa masikitiko makubwa sana.

Wito wangu, nawaomba wanafamilia wote kuwa watulivu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Rais Malinzi.

Msiba wa shabiki huyo wa Simba umetokea wakati Simba imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Azam likihitimisha ushindani wa timu 86 na hivyo kuwa na hati ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF) hapo mwakani. Mwenyezi Mungu ampe mapumziko mema, Shabiki wa Simba, Shose Fideline.

“Pia nawapa pole nyingi sana majeruhi wote katika ajali hiyo akiwamo Jonas Mkude ambaye ni Nahodha wa Simba na Nahodha Msaidizi wa Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’. Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu majeruhi wote wapone haraka ili kujiunga na shughuli zao mbalimbali za ujenzi wa nchi,” amesema Rais Malinzi.

Kadhalika, Rais Malinzi ameipongeza Simba kwa kutwaa ubingwa huo wa ASFC hivyo pamoja na zawadi nyingine kama vile Sh 50 milioni na medali za ubingwa pia Simba imepata tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Shirikisho - michuano inayoandaliwa na CAF.
“Naitakia Simba maandalizi mema ya kushiriki michuano ya kimataifa hapo mwakani,” amesema Rais Malinzi.

TAIFA STARS KUWEKA KAMBI MISRI, MKUDE ABAKI

 Kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti, kinatarajiwa kuondoka kesho Jumanne saa 10.45 jioni kwenda Misri.

Taifa Stars ambayo itakuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kesho saa 7. 45 mchana inakwenda Misri kufanya kambi ya siku nane kujindaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao 20 kutoka hapa Tanzania wataungana na na wengine watatu, Nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Faridi Mussa wanaocheza ughaibuni katika kikosi hicho na kufanya jumla ya wachezaji kuwa 23 nchini Misri.
Nahodha Msaidizi, Jonas Mkude hatakuwako kwenye msafara huo kutokana na ushauri wa madaktari walioelekeza kwamba nyota huyo wa Simba apate mapumziko ya angalau siku nne.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ameridhia na kusema kuwa Mkude ataungana na wenzake Juni 8, mwaka huu timu itakaporejea kutoka Misri.
Mayanga hajajaza nafasi ya Mkude.

 Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon. Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo. Kikosi cha Taifa Stars kinachofundishwa na Kocha Salum Mayanga kinaundwa na makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar). Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Haji Mwinyi (Yanga SC).

Walinzi wa kati Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Agrey Morris (Azam FC) ilihali viungo wa kuzuia ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude kutoka Simba SC ambaye hatasafiri na timu kwa sasa.
Viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na Mzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa pembeni ni Simon Msuva (Yanga SC), Shizza Kichuya (Simba SC) na Farid Mussa (Teneriffe, Hispania). Washambuliaji wapo Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting). Wasaidizi wa Mayanga katika benchi la ufundi ni Novatus Fulgence ambaye ni kocha msaidizi Patrick Mwangata - kocha wa makipa pia yumo Meneja wa timu, Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu, Daktari wa timu ni Richard Yomba na Daktari wa viungo ni Gilbert Kigadya. Timu hiyo iliingia kambini Machi 23, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam kabla ya kesho kwenda Misri na baadaye itarejea Tanzania kucheza na Lesotho, Juni 10, mwaka.


MAREKEBISHO YA KANUNI ZA LIGI KUU YA VODACOM NA LIGI DARAJA LA KWANZA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatangazia klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/18 na zile za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2017/18 kwamba kipindi hiki ni cha kuwasilisha maoni na mapendekezo mbalimbali kuhusu marekebisho ya kanuni za ligi husika.

TFF inaagiza klabu zote - kwa nafasi walizonazo kama wanafamilia ya mpira wa miguu, kuwasilisha mapendekezo na maoni kuhusu marekebisho ya katiba kwa njia ya kuyatuma kupitia anwani za sanduku la Barua 1574, Dar es Salaam au barua pepe tplb.tplb@yahoo.com au yaletwe moja kwa moja ofisi za Bodi ya Ligi au TFF. Maoni hayo tayafanyiwa kazi na Bodi ya Ligi kabla ya kupelekwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji kabla ya kuanza msimu husika wa mashindano baada ya kupita msimu uliopita.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

UMOJA WA ULAYA KUSHINDANISHA VIJANA WA TANZANIA

$
0
0
Kutoka kulia ni Mratibu wa Tamasha la Umoja wa Ulaya Mosse Sakar katikati Ofisa Uhusiano wa Umoja wa Ulaya Sara mbise na Ofisa Mawasiliano na Uhusiano  Bodi ya Filamu nchini Tanzania wakizungumza na waandishi wa habari jana kwenye uzinduzi wa tamasha hilo ambalo  mwaka huu limekuja kivingine kwa kutoa fursa kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 kutunga filamu fupi itakayochezwa kati ya dakika 5 hadi kumi itakayohusu  kuongez3ka kwa idadi ya watu duniani faida na hasara zake kwa kuwa ongezeko hilo inagusa  sehemu nyingi katika maisha ya kila siku pia nia agenda ambayo VIJANA nchini wametakiwa kuchangamkia fursa ya  mashindano yatakayofanyika kwa mara ya kwanza ya uandishi  na uchezaji wa filamu fupi itakayoelezea faida  au hasara ya ukuaji wa idadi ya  watu duniani.

Shindano hilo limepangwa kuwashirikisha vijana  wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 ambao wana njozi za kufanikiwa kwenye tasnia ya filamu  na ambao hawajawahi kufahamika kabisa.

Akizungumza jana na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa shindano hilo uliofanyika kwenye Ofisi za Umoja wa nchi  Ulaya Ofisa habari wake   Susan Mbise alisema  shindano hilo ni la hiari na watakaopenda kushiriki watatakiwa kujaza fomu maalumu.

"Shindano hili limeandaliwa  ili kuwapa wasaa vijana kuweza kuonesha vipaji walivyo navyo ambapo kila mmoja atatakiwa kurekodi filamu kwa lugha ya kiswahili pamoja na 'subtittle'za kiingereza" alisema Mbise.

Aidha aliweka wazi kuwa shindano hili linawahusisha vijana wa nchi nzima na  filamu hiyo itatakiwa kuwa ndani ya muda wa dakika tano au kumi .

 Baada ya hapo filamu 15 bora zitaoneshwa  kwa umma ambao baadaye  zitachaguliwa filamu tano bora huku mshindi wa kwanza akijinyakulia kitita cha  Sh. Mil.7 , mshindi wa pili atapata Sh. Mil.5 na watatu ataondoka na Sh. Mil.3.

Pia kutakuwa na zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kujifunza lugha ya Kifaransa kwenye kituo cha utamaduni cha Ufaransa Jijini Dar es Salaam.

Naye Mratibu wa shindano hilo Kutoka Kampuni ya Anderson Macha Mosse Sakar alisema  zaidi ya miaka 25 Umoja wa Ulaya wamekua wakifanya tamasha hilo halikua lenye mafanikio huku akisisitiza vijana wajitokeze kwa  wingi.

Wakati huohuo Ofisa Mawasiliano  Uhusiano Bodi ya Filamu Abuu Kimario  alisema tamasha hilo limekuja katika wakati muafaka na kupongeza Umoja huo  kuelekeza nguvu kwa vijana wachanga.

"Hivi sasa lugha ya Kiswahili imekua lulu duniani  hivyo vijana  watakaopata  nafasi  ya kushiriki  wataweza kuitangaza vyema  nchi yetu ya Tanzania" alisema Kimario.

Alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa anawaasa vijana  kutumia muda huu kujifunza viwango vya Kimataifa  pamoja na kuzingatia masharti na vigezo.

Fomu zinapatikana kwenye kituo cha utamaduni cha Ufaransa, Brithish Council  washiriki wametakiwa kurudisha fomu  hizo mara  baada ya kuzijaza kabla ya Juni 15 mwaka huu.

UMISSETA MKOA WA DAR ES SALAAM WAPAMBA MOTO

$
0
0
Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalisha Mkoa wa Dar es salaam N Edward Otieno akizungumza wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Lipesi Kayombo akiwasalimu wanamichezo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam  katika Uwanja wa Uhuru.
Baadhi ya wanamichezo kutoka Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam wakifatilia mchezo kati ya Ilala na Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam  katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na mchezaji wa Mpira wa Miguu Manispaa  ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es Salaam katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Lipesi Kayombo (Kushoto), Kaimu Katibu Tawala upande wa Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam Edward Otieno (Katikati) na Afisa Elimu Mkoa wa Dar es salaam Khamisi Lissu wakati wa ufunguzi wa UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam katika Uwanja Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John Lipesi Kayombo akitoa hamasa kwa timu ya UMISSETA Wilaya ya Ubungo wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es salaam  2017 katika Uwanja wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiimba wimbo maalumu wa Michezo ya UMISSETA wakati wa ufunguzi wa  UMISSETA Mkoa wa Dar es Salaam 2017 katika Uwanja wa Uhuru.

Na Mathias Canal

Maandalizi ya ngazi ya Mkoa wa Dar es salaam Kwa Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania yamezidi kupamba moto katika Uwanja wa Uhuru na Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es  Salaam.

Maandalizi hayo kwa ngazi ya Mkoa kwa ajili ya kupata timu ya Mkoa wa Dar es salaam yameanza kwa kushirikisha timumkutoka Manispaa za Mkoa ikiwemo Ilala, Temeke, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo Kwa ngazi ya Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam Kaimu Katibu Tawala  Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam  Edward Otieno amewasihi washiriki kutumia weledi wao wa mafunzo waliyoyapata kuhusu michezo na kuonyesha umahiri wao ili kuchaguliwa katika timu ya Mkoa.

Wanafunzi hao ambao wameweka kambi katika Shule ya Sekondari Jitegemee mpaka Mei 31, 2017 wataanza safari ya kuelekea Jijini Mwanza kwa ajili ya mashindano hayo ngazi ya Taifa yanayotaraji kuanza kufanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba June 6, 2017.

Otieno alisema kuwa vijana hao wanapaswa kutambua kuwa michezo ndio ajira inayolipa zaidi duniani hivyo wanapaswa kudumisha nidhamu kwa kipindi chote cha mashindano.

Aliongeza kuwa wanapaswa kutambua kuwa timu zote za Mkoa wa Dar es Salaam zitakwenda Mwanza kushindana katika michezo hiyo ngazi ya Taifa na si kushiriki pekee.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo  John Lipesi Kayombo aliyezuru katika Uwanja wa Uhuru kujionea timu ya vijana wake kutoka Manispaa ya Ubungo ikichuana vikali na timu ya Manispaa ya Ilala amepongeza juhudi za washiriki wote ambao wameonyesha nidhamu ya hali ya juu.

"Ukiona vijana wana nidhamu kama hivi ni vyena kuwapongeza na kuwatia moyo maana bado wana safari ndefu kimichezo "alisema.

KAMPUNI YA BIMA YA BRITAM TANZANIA YAZINDUA HUDUMA YA BIMA YA AFYA

$
0
0

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Britam-Tanzania, Stephen Lokonyo akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam wiki iliyopita, wakati wa uzinduzi wa bima ya afya hapa nchini. Katikati ni Mkuu wa Bima ya Afya ya kampuni hiyo, Christine Mungi na kulia ni Mkuu wa Fedha na Utawala, Irene Godson.
 (NA MPIGA PICHA WETU)


Na Dotto Mwaibale


Kampuni  ya Bima ya Britam-Tanzania imezindua bima ya afya inayolenga kuhudumia makampuni makubwa, biashara ndogo na za kati (SMEs).

Bima hii inajumuisha gharama za matibabu ya wagonjwa waliolazwa, vipimo vya magonjwa mbalimbali pamoja na majeraha yaliyotokana na ajali kwa waajiriwa wasiopungua 10. Bima hii itagharimu kati ya shilingi milioni 5 mpaka milioni 200.

Akiongea katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo,Steven Lokonyo alisema bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi mpaka hosipitali, ushauri wa daktari, gharama za chumba maalumu cha uangalizi (ICU), mazoezi ya viungo, tiba ya mionzi, pamoja gharama za upasuaji.

Pia bima hii itagharamia kumsafirisha mgonjwa mahututi kwa ndege au gari kwenda hosipitali kupata huduma za matibabu, gharama za uchunguzi za eksirei na uchunguzi wa  kimaabara.  

"Bidhaa hii tunayoileta kwenye soko inakuja kuleta mabadiliko katika sekta ya afya na itaenda mbali kusaidia biashara ndogo na za kati na makampuni makubwa hivyo kukuza ustawi pamoja na uzalishaji wa wafanyakazi wao" alisema Lokonyo.

Lokonyo alibainisha pia kwamba bima hiyo ina faida za nyongeza kama vile tiba ya ugonjwa sugu uliogunduliwa, magonjwa ambayo mtu anayo kabla ya kuanza kutumia bima,UKIMWI na magonjwa mengine kama kisukari, kansa, magonjwa ya figo, ukurutu, maumivu ya viungo, magonjwa ya ini na kadhalika.

Uzinduzi wa bima hiyo umefanyika kwa kuzingatia uhitaji wa soko pia ni mkakati wa kampuni kupanua biashara yake ya bima nchini kwa kuangalia makundi ya watu ambayo yalikuwa hayajafikiwa na huduma za bima.

"Bima hii imeanzinduliwa kwa kuangalia uhitaji wa biashara ndogo na za kati pamoja na makampuni. Kampuni yenye wafanyakazi 10 sasa inaweza kupata huduma ya bima ambayo kila mtu anajua afya ya wafanyakzi ni muhimu kwa biashara yoyoye" aliongeza Lokonyo.

Takwimu za hivi karibuni zimeonyesha kuwa matumizi ya bima nchini Tanzania ni chini ya asilimia moja ya pato la taifa ambacho ni kiwango cha chini ukilinganisha na nchi zilizoendelea na nchi nyingine nyingi za kiafrika. Katika jitihada zake za kufikia watanzania wengi zaidi, Britam inapanua matawi yake nchini ambapo kwa sasa wapo katika mikoa saba ya Dar-es-salaam, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Mtwara, na Arusha.

Kampuni ya bima ya Britam Tanzania amabayo ilijulikana kama kama 'Real Insurance' hapo mwanzo ni kampuni tanzu ya 'Britam Holdings' ambayo inatoa huduma mbalimbali za kifedha katika bima, usimamizi wa mali, na benki.

JUMIA TRAVEL YAZINDUA RIPOTI YA UTALII BARANI AFRICA

$
0
0
JUMIA TRAVEL YAZINDUA RIPOTI YA UTALII BARANI AFRIKA 

Kuzidi kuongezeka kwa watumiaji wa intaneti barani Afrika na kufikia zaidi ya milioni 300 ambayo kiuwiano kwa ueneaji wake ni sawa na 27.7% ni ishara nzuri kwa uchocheaji wa ukuaji wa shughuli za utalii kwa njia ya mtandao.



Hayo yalibainishwa kupitia ‘Ripoti ya Utalii Afrika kwa mwaka 2017’ iliyowasilishwa na Jumia Travel inayojihusisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao, ambapo inaelezea kuwa teknolojia na huduma za simu zimeliingizia bara la Afrika mapato ya ndani kwa 6.7% kwa mwaka 2015 (ambazo ni sawa na dola za kimarekani bilioni 150 kwa thamani ya kiuchumi), na yanatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni 210 (7.6% ya jumla ya pato la ndani la taifa) kufikia mwaka 2020.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuiwasilisha ripoti hiyo, Meneja Mkaazi wa Jumia Travel nchini Tanzania, Bi. Fatema Dharsee amesisitiza kuwa takwimu hizo zinaifanya kampuni kuamini kuwa bara la Afrika lina fursa kubwa katika ukuaji wa sekta ya utalii kwa njia ya mtandao.


“Jumia Travel inaona kuwa ujio wa intaneti na kupokelewa vizuri na waafrika, ni ishara nzuri kwamba sekta ya utalii itakua ukizingatia ina mchango mkubwa kwenye kuchangia pato la taifa. Kwa mfano mpaka kufikia mwishoni wa mwaka 2015, 46% ya idadi ya waafrika (zaidi ya nusu bilioni ukilinganisha na idadi ya waafrika wanaofikia takribani bilioni 1.2) walijiunga na huduma za simu. Hii idadi ni ya kipekee kwani inatarajiwa kufikia milioni 725 mnamo mwaka 2020,” alisema Bi. Dharsee.


“Hayo yote kwa kiasi kikubwa yamechochewa na uapatikanaji wa mtandao wa intaneti wa 4G kwa zaidi ya nusu ya nchi za kiafrika, ambapo mpaka kufikia katikati ya mwaka 2016 takribani nchi 32 zilikuwa zimekwishaunganishwa na mitandao 72 ya LTE (Long-Term Evolution). Hata hivyo, bado tunajikongoja kwa namna tulivyopokea mabadiliko hayo ukilinganisha na sehemu zingine duniani ambapo ueneaji wake kwetu ni sawa na 20% ya idadi ya watu waliofikiwa na mtandao wa 4G,” aliongezea Menaja Mkaazi huyo wa Jumia Travel hapa Tanzania.


Aliendelea kwa kufafanua zaidi kuwa changamoto kubwa inayolikabili bara la Afrika kwa sasa hususani kusini mwa jangwa la Sahara ni ukosefu wa ujuzi kwenye masuala ya kigiditali. Hivyo basi wao wanaona kwamba kuunga mkono jitihada za utoaji elimu ya kidigitali kwa wadau wa utalii kuna umuhimu mkubwa katika kukuza sekta hiyo mtandaoni ndani ya bara la Afrika.


Mbali na uwasilishaji wa ripoti hiyo ya utalii barani Afrika pia kampuni hiyo imesema kuwa kwa sasa inaendesha kampeni inayolenga kuwakomboa waafrika kusafiri ndani na nje ya mipaka yao kwa gharama nafuu.


“Kampeni hii iliyopewa jina la ‘Democratize Travel’ dhumuni letu kubwa ni kuondoa mawazo yaliyojengeka miongoni mwetu haswa linapokuja suala la mchakato mzima kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hii inamaanisha kupunguza gharama hususani za malazi, upatikanaji wa taarifa pamoja na kutoa huduma bora kwa kila mtu. Pia kupitia kampeni hii tunataka kuwaonyesha wateja wetu uzuri uliofichika kuhusu bara la Afrika kwa kuwapatia suluhu ya mahitaji yao yote pindi wanapotaka kusafiri kama vile; hatua au mambo ya kuzingatia, malazi, chakula na shughuli za kufanya mahali waendapo,” alisema Bi. Dharsee.


“Hatutoishia hapo bali tunataka pia kuondoa mitazamo tofauti ya kwamba sehemu za kutembelea zilizopo nchi za Magharibi kama vile Ulaya na Marekani au Dubai ni bora zaidi ya Afrika. Mbali na kuwarahisishia waafrika kusafiri kwenye maeneo waliyopo lakini pia tunawawezesha kuvuka mipaka kwenda sehemu nyingine duniani. Hapa msafiri ataweza kulipia gharama za kusafiri, kwa mfano kwenda jijini London nchini Uingereza, kwa fedha ya nchi yake anayotokea. Hayo yote yanawezekana na yamerahishwa kwani kupitia mtandao wetu mteja ataweza kukatatiketi ya ndege na kufanya huduma ya malazi kwa sehemu anayokwenda kwa wakati mmoja,” alihitimisha  Bi. Dharsee.


Kampuni hiyo imesema mbali na kuelekeza kampeni hiyo kwa wateja wake lakini pia itawashirikisha hoteli washirika katika kuhakikisha wanawafikia wateja na kukua kwa haraka zaidi. Hayo wanayahakikisha kupitia kuwatangaza mtandaoni ili kukuza muonekana na biashara zao, kuwapatia mifumo ya teknolojia inayoendana na soko la Afrika ili kuwarahishia uendeshaji wa biashara zao kama vile Extranet, SMS au barua pepe pamoja na kuchochea utoaji na uboreshaji wa huduma bora ili kuwavutia wateja wengi zaidi.


Akizungumzia namna Jumia Travel inavyorahisisha ufanyikaji wa shughuli za kila siku za hoteli, Kaimu Meneja Mkuu wa Hong Kong Hotel ya jijini Dar es Salaam, Bw. Mganja Suleiman amesema kuwa, “Kujiunga kufanya kazi na mtandao wa Jumia Travel kumetunufaisha kwa kiasi kikubwa sana ukilinganisha na hapo awali. Kwanza kabisa kujulikana na kutangazwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania hivyo kutuongezea soko, kama mjuavyo shughuli za matangazo na kutafuta masoko zinahitaji mfanyabiashara au kampuni iwe na fedha ya kutosha. Lakini kupitia mtandao huu wateja wanaweza kujua huduma tulizonazo bila ya hata kuwasiliana nasi moja kwa moja kwani kila kitu kipo mtandaoni na pia kuacha maoni yao pale wanapovutiwa na namna walivyohudumiwa au kitu gani cha kuboresha.”


“Kwa kiasi kikubwa mtandao huu umekuwa ni chachu kwa hoteli yetu kufanya vizuri na kuendelea kuboresha huduma zetu kwa ubunifu zaidi ili kuweza kumudu suhindani wa kwenye soko. Pia ningependa kutoa pongezi kwa kutuletea teknolojia mpya na za kisasa kabisa ambazo zinarahisisha kazi zetu. Kwa mfano mfumo wao wa Extranet ambao umelenga kuwarahisishia mameneja au wa hoteli au wapokeaji wa maombi ya huduma kutoka kwa wateja kwa njia ya mtandao popote walipo. Mfumo huu unapatikana kwenye kompyuta, tabiti na simu pia, hivyo kupunguza lile adha ya kumlazimu meneja kutoa huduma mpaka awe hotelini. Lakini pia mfumo huu unatupatia sisi fursa ya kujua aina, idadi na hadhi ya wateja wanaotumia huduma zetu hivyo kurahisisha kuwafikia na kuwapatia kile wanachokitaka,” alihitimisha Bw. Suleiman.
BONYEZA ‘LINK’ HAPA CHINI KUISOMA RIPOTI HIYO

HALMASHAURI NCHINI ZAAGIZWA KUWATENGENWZEA WAZEE VITAMBULISHO VYA MATIBABU

MWANAMUZIKI TONGOLANGA AZIKWA NYUMBANI KWAO MCHICHILA TANDAHIMBA

$
0
0

Halila Tongolanga amefariki jana usiku katika hospitali ya Muhimbili. Alikuwa mwanamuziki wa siku nyingi na alifahamika kwanza  kwa wengi baada ya kuanza kusikika kibao chake cha lugha ya Kimakonde cha Kila munu ave na kwao, chenye tafsiri ya ‘Kila mtu ave kwao’ ambacho alikirekodi akiwa bendi ya jeshi ya CTU Monduli, iliyojulikana kama  Les Mwenge. 

Kwa kifupi ni kuwa baada ya hapo aliitwa kujiunga na bendi iliyokuwa mali ya Dr Alex Khalid, iliyokuwa ikiitwa Makondeko Six. Wakati huo Dr Khalid alikuwa na sehemu kubwa ya burudani iliyokuwa pia na ukumbi na ilikuwa inaitwa Makondeko ikawa na bendi ya watu sita hivyo bendi hiyo ikaitwa Makondeko Six. 

 Bendi hii awali ilikuwa ikipiga muziki kwa kufuata nyayo za bendi ya Tatu Nane, lakini Dr Khalid baada ya kuona bendi haina umaarufu kutokana na aina ya muziki iliyokuwa ikipiga, ndipo alipomuita Halila Tongolanga nae akaja na baadhi ya wanamuziki wakajiunga na kuanzisha kundi lililoendelea kutumia jina la Makondeko Six japo wanamuziki walikuwa wengi zaidi ya sita. Na ndipo katika kundi hili lilikuwa na wanamuziki wengine kama Innocent Nganyagwa, Anna mwaole wakaweza kurekodi tena wimbo wa Kila Munu Ave na kwao na kundi kupata umaarufu mkubwa mpaka baada ya kusambaratika kwa Makondeko baada ya kifo cha Dr Alex Khalid, lakini Tongolanga aliendelea kutumia jina la Makondeko.
Baadhi ya wanamuziki waliowahi kufanya kazi na Tongolanga katika kundi la makondeko Six, wakiwa wanasubiri kusafirisha mwili wa mpendwa wao.Toka kushoto, Innocent Nganyagwa, Meneja wa bendi, mpiga solo, Waninga     



              


 Tongolanga amefanya kazi nyingi za muziki ikiwemo kuwa mmoja wa kundi lililoundwa na wanamuziki wengine mahiri kama Moshi William, Muhidin Mwalim, Huluka Uvuruge, Kandaya na wengine lililojulikana kama Bana mwambe, ambapo waliweza kutoka nyimbo nyingi nzuri sana wakati biashara ya kuuza album ilipokuwa ina faida. Tongolanga ameagwa na wapenzi wa muziki ndugu na marafiki, lakini kulikuwa na uhaba mkubwa wa wanamuziki wenzie katika kundi lililokuja kumuaga mwanamuziki huyu. 

Waliojitokeza hasa ni wanamuziki wale tu ambao waliwahi kupiga nae katika kundi la Makondeko na Bana Mwambe na wanamuziki wengine wachache wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki John Kitime, Katibu Mkuu wa Chamudara Hassan Msumari. 

Serikali iliwakilishwa na Katibu Mtendaji wa BASATA  katika jambo moja kubwa lililotokea wakati wa kuaga mwili ni kujitokeza kwa balozi wa Msumbiiji Bi Monica Patricio Clemente aliyefika Muhimbili kuaga mwili wa Tongolanga akiwa amesindikizwa na maafisa wengine, na pia Balozi huo alitoa rambirambi zake kama Balozi na alitoa rambirambi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji. 

Hili lilikumbusha usemi wa wahenga ‘Nabii hathaminiwi kwao.’ Taarifa zilizopatikana pale ni kuwa Tongolanga alikuwa mtu maarufu sana nchini Msumbiji, na aliyekuwa ni msanii muhimu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini humo.
Balozi wa Msumbiji Bi Monica Patricio Clemente akiaga sanduku lililokuwa na mwili wa Halila Tongolanga

Nilipokutana nae kwa mara ya mwisho akiwa kitandani Tongolanda kwa sauti ya uchovu alinambia alikuwa na mengi ya kunambia, wakati tunasubiri taratib kukamilika za kuanza kusafirisha mwili, Innocent Nganyagwa ambaye alikuwa mmoja ya wanamuziki waliotengeneza kundi la Makondeko Six alinambia Tongolanga alikuwa amepanga kufanya onyesho la ‘Usiku wa Makondeko’ na alikuwa na mipango mingine mikubwa ya kufanya kupitia kipaji chake. Pengine ndiyo hayo aliyotaka kunambia Mungu pekee anajua. 

Shukrani za pekee zimfikie Mbunge wa Tandahimba Mheshimiwa Katani Ahmed Katani, kwani kwa juhudi zake Tongolanga alisafirishwa akiwa hai kutoka Ndanda hadi Dar es Salaam kwa matibabu, na pia ndie aliyeusafirisha mwili wa mwanamuziki huyu kwenda Mchichila kwa ajili ya mazishi.
Toka kushoto Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Nyangamale, Balozi wa Msumbiji nchini, Katibu Mtendaji wa BASATA, Mbunge wa Tandahimba Mhe Katani Katani, afisa wa Ubalozi wa Msumbiji

Tongolanga anategemewa kuzikwa kijijini kwao Mchichila  jana  Junanne  Juni 6  2017.

Mungu Amlaze Pema Halila Tongolanga 
Mpiga Kinanda Geophrey Kumburu, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, Katibu Mkuu wa CHAMUDATA Hassan Msumari
John Kitime, wanamuziki wa Makondeko Six, Mngereza, KumburuAdd caption

Sanduku alilolazwa Halila Tongolanga likitayarishwa kuingizwa kwenye gari la kusafirisha kuelekea Mcjichila




Sanduku likiingizwa kwenye gari

Imetayarishwa na John Kitime wa www.tanzaniarhumba.blogspot.com

PROF TIBAIJUKA AONYA UPITOSHAJI WA MITANDAONI

ALIYOZUNGUMZA PROF ELISANTE OLE GABRIEL KATIKA MKUTANO WA SABA WA AFRICAN DIGITAL TV DEVELOPMENT

BULEMBO AFUNGA KAZI WILAYANI MISENYI

$
0
0
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Misenyi, Mabalozi, viongozi wa Jumuia za CCM na watendaji wa Serikali katika Wilaya hiyo Mkoani Kagera.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ukumbini
 Wajumbe wakiwa ukumbini tayari kumsikiliza Alhaj Bulembo
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzana, Wilaya ya Misenyi Rehema Mtawala akimkabidhi zawadi maalum Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo kabla ya kikao kuanza
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akionyesha zawadi hiyo maalum baada ya kukabidhiwa. Zawadi hiyo ina maneno ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Mbunge. 
Mwenyekiti wa CCM wa CCM Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Haji Seruhu akifungua kikao hicho
 Katibu wa CCM Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Mwajuma Mboha, akieleza maneno ya utangulizi katika kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misenyi Haji Seruhu, wakati wanapita taarifa iliyosomwa na Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo
 Wajumbe wakihamasika kwenye kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akitulia kumsikiliza kwa makini mshairi Mansur Athan wakati akighani shairi mwishoni mwa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipokea zawadi ya Mbuzi aliyopewa na Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Misenyi wakati wa kikao hicho leo.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera  Yahya Kateme (kushoto) akibadilishana mawazo na Vijana wa wa CCM nje ya ukumbi baada ya kikao
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ajhaj Abdallah Bulembo akiendelea kuwasikiliza nje ya ukumbi badhi ya wadau waliotaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo baada ya kikao hicho 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akiwafafanulia jambo nje ya ukumbi baadhi ya wadau  
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj abdallah Bulembo akiendelea kuwasikiliza wadau hata baada ya kupanda gari lake tayari kwa kuondoka

Baada ya wadau kuridhika wakamuaga kwa furaha na kumtakia safari njema kwenda Wilaya ya Bukoba mjini
 Safari ya Alhaj Bulembo kutoka Misenyi kwenda Wilaya ya Bukoba mjini ilipitia kwenye daraja hili la Mto Kagera, eneo la Kyaka.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera  Yahya Kateme akizungumza na vijana waendesha bodaboda aliowakuta Bukoba Mjini, baada ya msafara wa Alhaj Abdallah Bulembo kuwasili
 Mwenyekiti huyo wa UVCCM akapiga picha ya pamoja na vijana wa green Guard wa Bukoba mjini
 Baada ya kuwasili tu Bukoba Mjini, Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo alieanda ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu na kuwa na mazungumzo naye kwa muda. Pichani, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo hayo. Wengine kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Lahel Ndegeleki na Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Costansia Buhiye
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimweleza jambo Mkuu huyo wa mkoa kabla ya kuondoka 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia vijana wa green Guard nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimwelekeza jambo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini Yusuf Ngaiza wakati wa kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya hiyo, Mabalozi, viongozi wa Jumuia na Watendaji wa serikali.
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini mkoani Kagera Yusuf Ngaiza akifungua kikao hicho
 Wajumbe wakiwa ukumbini katika kikao hicho
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho Bukoba mjini mkoani Kagera.
                                 PICHA; BASHIR NKOROMO

SHILAWADU NGOMA MPYA YENYE MAHADHI YA MDUARA KUINGIZWA SOKONI

$
0
0


'Shilawadu’ ni ngoma mpya kabisa ya mduara ambayo wiki hii imeachiwa rasmi kutoka kwa msanii anayekuja juu kwa kasi ya ajabu, Shania Kabeya.

Studio ya 442 Music iliyoko Karakata, Kipawa, Jijini Dar es Salaam chini ya Mtayarishaji Tamimu Hamis ‘Mabanga’ ndipo ilipopikwa ngoma hiyo iliyobeba ujumbe mzito juu ya wapenzi wanavyotakiwa kutoyafuatilia maneno ya watu wa pembeni.

Kwa upande wake Shania mwenyewe, hii ndio ngoma yake ya kwanza ambapo hata hivyo yuko mbioni kuandaa kazi nyingine ‘sumu’, anazoamini kuwa zitabamba zaidi na kutokea kufunika nyingine zitakazozikuta. Video ya kibao ‘Shilawadu’ iko jikoni na itatoka mwishoni mwa mwezi huu.

Ikiwa  sambamba na kibao chake kingine kipya cha mduara.

MSANII IRENE VEDA AUKWAA UBALOZI WA BODI YA TAIFA UTALII YA UTALII (TTB)

$
0
0
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) Akimkabidhi mkataba Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda mara baada ya kusaini.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) akimwelekeza Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda sehemu za kusaini mkataba wake wa miaka miwili.
Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda(kushoto) akiendelea kusaini mkataba wake .
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) akimalizia kumwelezea Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda sehemu za mwisho za kusaini katika Mkataba huo.
Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda akimalizia kusaini Mkataba wake ili kuanza rasmi kazi za kupeperusha Bendera ya kutangaza Utalii nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) pamoja na Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda wakionesha Mikataba yao baada ya kumaliza kusaini.
Kuona kazi ambazo ameanza kuzifanya bofya

Instagram: www.instagram.com/twendetukataliitz

 Twitter: www.twitter.com/TukataliiTz 

Facebook: www.facebook.com/TwendeTukataliiTz



Regards Tone Multimedia Company Limited Plot No.223/225 Block 46, Umoja Street Kijitonyama P.O Box 32529 Dar es salaam Tanzania Tel +255 22 2772919 Fax +255 22 2772892 E-Mail blogszamikoa@live.com Facebook: www.facebook.com/blogszamikoa Web: www.blogszamikoa.com
Viewing all 1915 articles
Browse latest View live