Quantcast
Channel: BONGOWEEKEND
Viewing all 1929 articles
Browse latest View live

MAELFU WAJITOKEZAZA IBADA YA MSIBA MKUBWA ULIOTUPATA IKIENDELEA

$
0
0
 Miili ikiwa imebebwa na magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania JWTZ kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.

 Picha za wanafunzi 32 ambao wamefariki kwenye ajali iliyotokea Karatu Jumamosi Mei 6 mwaka huu.
 Umati wa wakazi wa Jiji  la Arusha na mikoa ya jirani waliojitokeza kuaga miili ya watoto hao.



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameomba vyombo vya usafiri kubeba abiria kulingana na uwezo wa chombo cha kusafiria.Suluhu aliyasema hayo leo kwenye hafla ya ibada ya mazishi ya miili ya wanafunzi waliofariki Jumamosi Mei 6 mwaka huu kwenye ajali iliyotokea  Karatu Mkoani Arusha.

Suluhu amekazia suala la kuwa makini kwenye vyombo vya usafiri kua makini katika kuahkikisha sheria za usalama barabarani zinazingatiwa  ipasavyo.


Ajali hii i emegusa mioyo ya kila mtanzania ,msiba huu umetupa majonzi mengi huku ukithibitishwa na wingi wenu ambao mmejitokeza. Mungu azilaze pema roho hizi za watoto wetu. Innalillah wainna ilaihRajiun bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.


"Msiba huu umeitingisha Afrika Mashariki  na kati, maisha yetu siyo mengi siku zetu ni chache  hapa duniani Mwenyeezi Mungu amechukua hizi roho,  nchi yetu imekunywa damu nyingi, mungu tunakuomba ukawasaidie madereva ili waweze kuepusha ajali na serikali ikasimamie suala zima za usafiri wenye usalama".
Hayo yalisemwa na Askofu Mwizarubi wa Kanisa la EAGC.

Aidha alisema kuwa kila mwanadamu ana mambo yake ya siri ambayo hutopenda mtu mwingine ayafahamu ana anayejua ni Mwenyeezi Mungu peke yake.

Huku akisema kuwa hakuna mwanadamu anayeijua kesho,"Wenzetu walipanga wakaenda na laiti kama wangelijua hili wasingeenda safari yao  naamini ndugu zetu hawa wamemaliza safari yako kwa amani naamini hivyo sisi tulio hai ndiyo tunapaswa kujifikiria nafsi zetu".

Shughuli hiyo imehudhuriwa na  viongozi mbalimbali akiwemo Kiongozi wa Kambi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendelo CHADEMA pia Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako. Waziri wa Elimu wa Kenya


MFUMUKO WA BEI WA TAIFA MWEZI APRILI HAUJAONGEZEKA UMEBAKI 6.4%

$
0
0
 Mkurugenzi wa Sensa za watu na Takwimu  Ofisi ya Taifa ya Takwimu,(NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam , kuhusu mfumuko wa bei ya taifa kwa mwezi Aprili. Kulia ni Mtakwimu, Hashim Njowele.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

Mfumuko wa bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Sensa za watu na takwimu wa Ofis ya Taifa ya Takwimu,(NBS), Ephraim Kwesigabo, alisema hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha March 2017 imekuwa sawa na kasi ya upandaji  ilivyokuwa mwaka ulioisha.

Kwesigabo, alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.4 mwezi April 2017 kutoka 1o2 mwezi April 2016.

"Mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka umebaki kuwa asilimia 6.4 kama ilivyokuwa mwezi marchi 2017  kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha mwezi Aprili imekuwa sawa na mwezi Marchi 2017,"alisema

Pia alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi 11.8 kutoka asilimia 11.0 ilivyokuwa mwezi Marchi.

Aidha mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Aprili 2017 umeongezeka hadi asilimia 12.0 kutoka asilimia 11.7 mwezi Marchi 2017.

Alisema badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa sisizo za vyakula umepungua kidogo hadi asilimia 3.4 mwezi Aprili kutoka asilimia 3.6 mwezi Ma
chi.

Akizungumzia kuhusu ukuaji wa dhamani ya shilingi, Kwesigabo alisema  uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 91 na senti 71, mwezi Aprili 2017 ikilinganisha na shilingi 92 na senti 21 ilivyokuwa mwezi Marchi 2017.



SHIRIKA LA POSTA LATOA POLE MSIBA WA SHULE YA LUCKY VINCENT

SERIKALI KUFUTA USHURU NA TOZO MBALIMBALI KWA WAKULIMA

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI UJENZI WA KITUO CHA MABASI MBEZI LOUIS

UWEKEZAJI WAONGEZEKA KATIKA SEKTA YA UTALII NCHINI

$
0
0

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema kumekuwa na ongezeka la uwekezaji katika miundombinu na mahitaji yanayochangia ukuaji wa Sekta ya Utalii nchini.

Hayo yamesemwa  jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii  Ramo Makani wakati akijibu Hoja mbalimbali za Wabunge .

“Kumekuwa na Ongezeko la uwekezaji katika ujenzi wa Hoteli na Madaraja mbalimbali,uimarishaji wa vyombo vya usafiri kuelekea ndani ya Hifadhi na Maeneo mengine yenye vivutio na uboreshaji wa vifaa mbalimbali vinavyotumika kuhudumia watalii,mambo ambayo kwa kiwango kikubwa hutekelezwa na Sekta binafsi “Aliongeza Mhe.Makani.

Aidha amesema mafanikio hayo yamewezesha kuongezeka kwa idadi ya watalii ambapo mwaka 2016 idadi hiyo iliongezeka kutoka jumla ya Watalii milioni 1,137,182 kwa mwaka 2015 hadi jumla ya watalii 1,284,279 kwa mwaka 2016 sawa na ongezeko la asilimia 12.9 ambapo ongezeko hilo limeonekana katika Hifadhi za Taifa zinazosimamiwa na TANAPA.

Ameongeza kuwa ili ongezeko ili liwe na tija na endelevu Wizara hiyo imejikita katika kusimamia ubora wa huduma na utoaji huduma,kutangaza zaidi vivutio hususani vivutio vipya na kusambaza shughuli za Utalii nchi nzima hususani ukanda wa kusini.

“Kwa upande wa Serikali ujenzi wa barabara na viwanja vya Ndege,Ununuzi wa ndege mbili na zingine nne zinatarajiwa kuja katika siku za karibuni izi zote ni jitihada zinazochangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa Utalii nchini”alisisitiza Makani.

Pamoja na hayo ametoa wito kwa Sekta Binafsi kuongeza mbinu,bidii na mitaji kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukuza Utalii na Uchumi wa Taifa kwa ujumla.

WAZIRI MWAKYEMBE AWATAKA WASANII KUBORESHA VIPAJI VYAO

FRIENDS OF OCEAN WAUNGA MKONO KAMPENI YA KUTUNZA FUKWE

$
0
0
Wakazi wa Mikocheni  B wanaounda Chama cha Friends of Oceans wakisafisha fukwe ya Escape One katika uzinduzi wa kampeni ya Okoa Bahari ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza  Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya Koncept ,na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita.
Friends of oceans wakiendelea na usafi wa fukwe ya Escape one ikiwa kama uzinduzi wa kuanza usafi huo kwa kila mwezi na pia kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na rasilimali za bahari

 





Usafi ukiendelea katika fukwe ya Escape One ambapo kulikutwa chupa za bia,makopo ya maji, sindano na vingi ambavyo ni hatari kwa afya ya watumiaji wa fukwe hiyo  mapema mwishoni wa wiki iliyopita .
Friends of Ocean wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza usafi katika fukwe ya Escape One Mikocheni B kama uzinduzi wa kampeni ya  OKOA BAHARI yenye lengo ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza  Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT

Mkurungezi Mtendaji wa Koncept Krantz Mwantepele (mwenye tisheti nyekundu) ambao ni waratibu wa kampeni hii ya Okoa Bahati akiwa na wadau wa Friends of Ocean wakati wa  usafi uliofanyika katika fukwe ya Escape One

Muasisi na Kiongozi wa Friends Ocean Boss Brown (mwenye tisheti ya kijani) akifafanua jambo mara baada ya kumaliza usafi katika fukwe ya Escape One ikiwa ni uzinduzi wa kampeni ya Okoa Bahari ambayo  katika uzinduzi wa kampeni ya Okoa Bahari yenye lengo ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza  Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya Koncept.


Mkurungezi Mtendaji wa Koncept Krantz Mwantepele (mwenye tisheti nyekundu) ambao ni waratibu wa kampeni hii ya Okoa Bahari akifafanua jambo kwa wadau wa Friends of ocean mara baada ya kumaliza usafi katika Fukwe za Escape One . Okoa Bahari  yenye lengo ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza  Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa 
Fukwe ya Escape One mara baada ya kusafishwa na wadau wa Friends Of Ocean mwishoni wa wiki iliyopita 


N;B kwa yoyote anayependa kujiunga na Friends of Ocean au kujua kazi zetu wasiliana nasi Simu/Whatsapp 0658123310 /0625566775 Email;krantz.charles@koncept.co.tz


WAZIRI AKIONGELEA UHURU WA HABARI NCHINI

JUHUDI ZASERIKALI KATIKA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI

SERIKALI IMETENGA SHILINGI BILIONI 30 KUKAMILISHA MALIPO YA WAKAZI KIPUNGUNI

AFRIKA KUSINI KUENDELEA KUFUNDIAHA MARUBANI WA YANZANIAA

$
0
0
Na Husna Saidi & Jacquiline Mrisho- MAELEZO Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini imekubali kuendelea kuwafudisha marubani wa Tanzania ikiwa ni sehemu moja wapo ya kukuza maendeleo ya sekta ya uchukuzi na usafiri wa anga pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga ameyabainisha hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu majadiliano ya awali yaliyofanyika kati ya nchi hizo mbili juu ya mikataba mbalimbali inayotegemewa kusainiwa Mei 11 mwaka huu. Balozi Mahiga alisema kuwa katika majadiliano hayo wamejadili mikataba iliyowahi kusainiwa kwa kupima utekelezaji wake pamoja na kujadili mikataba mipya iliyojikita katika sekta mbalimbali za maendeleo zikiwemo za uchukuzi, nishati, elimu pamoja na mawasiliano. “Katika sekta ya uchukuzi tumekubaliana kuboresha barabara, usafiri wa anga pamoja na reli hasa ya TAZARA, sisi tumenunua ndege na tunaendelea kununua zingine zitakazosafiri hadi Afrika ya Kusini hivyo nchi hiyo imekubali kuendelea kuwafundisha marubani wa Tanzania kuendesha na kukarabati ndege hizo,”alisema Balozi Mahiga. Aliongeza kuwa mikataba hiyo inayotarajiwa kusainiwa hapo kesho imelenga maeneo ambayo yatapewa kipaumbele katika ushirikiano huo yakiwemo ya uchumi, biashara na uwekezaji pia mikataba hiyo imewekewa utaratibu wa ufatiliaji na utekelezaji wake. Akiongea kuhusu kulinda uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Afrika Kusini Bi. Maite Nkoana - Mashabane alisema kuwa ni wajibu wa kila mmoja kutafsiri ushirikiano wa kihistoria uliopo baina yetu na kuufikisha kwa kizazi hiki na kijacho kwani kwa kusoma tu historia katika vitabu ni rahisi kwao kusahau hivyo mkutano huo utapelekea kuendeleza na kurithisha uhusiano uliopo baina ya vijana wa nchi hizo mbili. “Tanzania na Afrika Kusini tuna historia kubwa ya kushirikiana katika harakati za kutafuta ukombozi wa nchi zetu lakini haitoshi kuwa na urafiki wa kihistoria tu bali tuwe na urafiki utakaoleta maendeleo katika nchi zetu”, alisema Bi. Maite. Nae Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema kuwa nchi ya Afrika Kusini ni miongoni mwa nchi nne zinazowekeza nchini kwa kiasi kikubwa hivyo tayari wana mikataba mbalimbali ambayo wanaendelea kuiboresha ili kuendelea kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda. “Tumeshaongea na Waziri mwenye dhamana ya viwanda wa Afrika Kusini kwamba kuna ardhi kubwa katika eneo la Kilombero 1 na Kilombero 2 hivyo waongeze nguvu ya kuwekeza katika uzalishaji wa sukari kwenye eneo hilo,”alisema Mwijage.

DC KASESELA AFUNGUA WARSHA YA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO AWAMU YA PILI (ADSP2)

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela akizungumza wakati wa kufungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Meya wa Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni mwenyekiti wa warsha akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela mara baada ya ufunguzi wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Na Mathias Canal, Dar es salaam akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni mwenyekiti wa warsha wakati wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa

Na Mathias Canal, Iringa

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela amefungua warsha ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.

Alisema kuwa ili kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini wataalamu wote nchini wanapaswa kubadilishana ujuzi na kushauriana namna ya kuwa na kilimo chenya tija kuliko kuficha ujuzi walionao kwa muktadha wa maeneo husika pekee waliyopo hivyo ni vyema kutumia ujuzi wao kwa makubaliano na maelekezano kwani jambo hilo litachochea zaidi ukuzaji wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Dc Kasesela ameyasema hayo wakati Akizungumza kwenye ufunguzi wa warsha hiyo inayofanyika katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa, warsha inayowahusisha Makatibu Tawala wasaidizi upande wa uchumi kutoka mkoa wa Iringa na Pwani na Maafisa kilimo wa mikoa, Meya wa Manispaa/Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa halmashauri za Manispaa/wilaya, Wachumi wa Manispaa/Wilaya na Maafisa Kilimo wa Manispaa/Wilaya kutoka Katika Halmashauri za Manispaa na Wilaya kutoka Mkoa wa Pwani na Dar es salaam.

Dc Kasesela ameeleza kuwa Programu hii ya ASDP 2 imeandaliwa baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya ASDP 1 iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2006/2007 hadi 2013/201 huku akiwapongeza waandaaji wa warsha hiyo ambao ni OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kutaraji kutekelezwa na wadau mbalimbali kama vile Wizara za sekta ya kilimo, Wahisani, Sekta binafsi, Taasisi zisizo za kiserikali, Wakulima Wafugaji, na Wavuvi.

Dc Kasesela amesema kuwa Utekelezaji wa ASDP 2 utazingatia malengo ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016-2021), Mkakati wa Taifa wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Dira ya maendeleo ya Tanzania (2025).

Alisema kuwa Programu hiyo imezingatia vipaombele vya vizara ya Kilimo, Ufugaji na uvuvi na imelenga kutatua changamoto na kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo, Kuongeza pato la Taifa, Kuboresha kipato cha wakulima wadogo na usalama wa chakula na lishe nchini.

Sambamba na hayo pia alisema kuwa wadau wote wa ASDP 2 wanapaswa kusimamia na kutekeleza kwa weledi maeneo makuu manne ya utekelezaji wa Programu hiyo ambayo ni Usimamizi wa Matumizi ya maji na ardhi (Sustainable Water and Land use Management),, Kuongeza tija na faida katika kilimo, mifugo na uvuvi (Enhanced Agricultural productivity and profitability).

Maeneo mengine ya kusimamiwa vyema na wadau ni Biashara na Uongezaji wa thamani kwenye mazao (Commercialization and Value Addition, na Viwezeshi vya sekta, Uratibu, Ufuatiliaji, na Tathmini ya sekta (Sector Enablers, Coordination and Monitoring and Evaluation).


WAZIRI MWAKYEMBE APOKEA HUNDI YA SH.BIL.50 YA SPORT PESA KUCHANGIA SERENGETI BOYS

$
0
0

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harisson Mwakyembe (Kushoto) akipokea Hundi ya Shillingi milioni 50 kutoka kwa Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SportPesa Tarimba Abbas( kulia) kwa ajili ya kuisadia timu ya mpira ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) leo Jijini Dar es Salaam, katika ni Mkurugenzi wa Michezo Yussuph Singo.


 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harisson Mwakyembe (Kushoto) akitoa neno la shukrani baada ya kupokea Hundi ya Shillingi Milioni 50 kutoka kwa Kampuni ya SportPesa kwajili ya kuisadia timu ya mpira ya vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni hiyo Tarimba Abbas.

KAMPUNI YA TANCOQL ENERGY YATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI

$
0
0

Meneja Udhibiti Ubora wa Makaa ya Mawe wa Kampuni ya Tancoal Energy Tanzania Limited Bw. Bosco Mabena akielezea moja ya majukumu wayafanyayo katika Kitengo cha Udhibiti Ubora wa makaa ya mawe  yanayochimbwa kutoka mgodi wa makaa hayo uliopo Ngaka, Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma 10 Mei, 2017.


Baadhi ya Malori katika eneo la Kitai Wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma yakiwa yamepakiwa makaa ya mawe yakifungwa maturubai kwa ajili ya kuzuia makaa ya mawe hayo kunyeshewa na mvua ikiwemo kuchafuliwa na aina yoyote ya uchafu wakati wa kuyasafirisha makaa hayo 10 Mei, 2017.


Lori lililopakia makaa ya mawe katika eneo la Kitai Wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma likipimwa uzito kabla ya kwenda kufungwa turubai tayari kwa kuanza safari ya kupeleka makaa hayo kwa mteja wake, 10 Mei, 2017.


Naibu Meneja wa Mgodi wa Kampuni ya Tancoal Energy Limited (wa pili kulia) Bw. Edward Mwanga, Meneja Udhibiti Ubora wa Makaa ya Mawe wa Kampuni ya Tancoal Energy Tanzania Limited Bw. Bosco Mabena (wa pili kushoto), Afisa Mauzo na Usafirishaji wa Kampuni ya Tancoal Energy Tanzania Limited, Bi. Leahkissa Mwangosi pamoja na Meneja Mawasiliano Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) (kulia) wakielekea katika eneo la mzani wa kupimia malori katika eneo la Kitai Wilayani Mbinga, Mkoani Ruvuma 10 Mei, 2017.

SERIKALI YAJA NA FAO LA KUKOSA AJIRA

TRA YATOA MAFUNZO YA ELIMU YA KULIPA KODI KWA WANAHABARI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
TRA YAMZUNGUMZIA MSANII DIAMOND PLATNAMUZ KUHUSU KODI: NI WAKATI WA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI JIJINI LEO Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Mei 13, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi. Angella Msangi na kushoto ni Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Mwangosi Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi NA K-VIS BLOG/Khalfan Said MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa kodi ya shilingi Milioni 400. Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipajin kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam. “Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza “Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo. “Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. Awali akifungua semina hiyo. Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi. Hayo yamesemwa leo Mei 13, 2017 na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Bw. Richard Kayombo(pichani juu), wakati wa ufunguziwa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbin wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. “Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo. Bwana Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chom,bo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za serikali katika kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma. “Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA. Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi Waandishi wa habari wakifuatilia Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (kulia), akiwakaribisha waandioshi wa habatri kwenye semina. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina, Bi. Angella Msangi Bw. Sydney Mkamba, Afisa Kodi Mkuu Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Gabriel Mwangosi. Bw. Emmanuel Herman, kutoka Mwananchi Mwenyekiti wa semina akifuatilia Bw. Obeid Mwangasa Othman Michuzi(kushoto) wa Mtaa kwa Mtaa Blog na Bw. Mushi wa The Habari.com Anna Nkinda(kulia) kutoka JKCI, na Mhariri wa Habari TBC, Anna Kwambaza. Codes;

TRA YAMZUNGUMZIA MSANII DIAMOND PLATNAMUZ KUHUSU KODI: NI WAKATI WA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI JIJINI LEO

 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa  semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Mei 13, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi. Angella Msangi na kushoto ni Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Mwangosi
 Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.
Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipajin kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza
“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo.

“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. Awali akifungua semina hiyo.
Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo Mei 13, 2017 na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Bw. Richard Kayombo(pichani juu), wakati wa ufunguziwa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbin wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

“Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo.

Bwana Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chom,bo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za serikali katika kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma.

“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.
  Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
  Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
 Waandishi wa habari wakifuatilia
 Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (kulia), akiwakaribisha waandioshi wa habatri kwenye semina. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina, Bi. Angella Msangi
Bw. Sydney Mkamba, Afisa Kodi Mkuu
Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Gabriel Mwangosi.
 Bw. Emmanuel Herman, kutoka Mwananchi
 Mwenyekiti wa semina  Angela Msangi akifuatilia jambo.
Mwanahabari Mkongwe  Obeid Mwangasa
 Othman Michuzi(kushoto) wa Mtaa kwa Mtaa Blog na Bw. Mushi wa The Habari.com
Anna Nkinda(kulia) kutoka JKCI, na Mhariri wa Habari TBC, Anna Kwambaza.

TRA YAMZUNGUMZIA MSANII DIAMOND PLATINUMZ KUHUSU KODI

$
0
0


 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA),  Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa  semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Mei 13, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi. Angella Msangi na kushoto ni Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Mwangosi
 Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi

MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.

Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipajin kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza

“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Kayombo.

“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. Awali akifungua semina hiyo.

Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo Mei 13, 2017 na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Bw. Richard Kayombo(pichani juu), wakati wa ufunguziwa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbin wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

“Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema  Kayombo.

Bwana Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chom,bo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za serikali katika kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma.

“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.
  Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
  Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
 Waandishi wa habari wakifuatilia
 Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (kulia), akiwakaribisha waandioshi wa habatri kwenye semina. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina, Bi. Angella Msangi
Bw. Sydney Mkamba, Afisa Kodi Mkuu
Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Gabriel Mwangosi.
 Bw. Emmanuel Herman, kutoka Mwananchi
 Mwenyekiti wa semina akifuatilia
 Bw. Obeid Mwangasa
 Othman Michuzi(kushoto) wa Mtaa kwa Mtaa Blog na Bw. Mushi wa The Habari.com
Anna Nkinda(kulia) kutoka JKCI, na Mhariri wa Habari TBC, Anna Kwambaza.

HIVI NDIVYO VIGEZO VINAVYOTUMIKA KATIKA KUZIPANDISHA HADHI HOTELI

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania

Hivi ushawahi kujiuliza ni kwanini hoteli fulani inatajwa kuwa ni ya nyota tatu, nne au tano? Najua itakuwa ni vigumu kuelewa kama haupo katika tasnia ya masuala ya hoteli au utalii mpaka upatiwe ufafanuzi wa kutosha.

Hivi karibuni Serena Hotel ya jijini Dar es Salaam ilifanikiwa kupewa hadhi ya kuwa hoteli ya nyota tano katika hafla ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe. 

Umuhimu wa kuzipatia hadhi hoteli husaidia sana kuchochea ushindani katika biashara hasa kwa upande wa uboreshaji wa huduma.   

Kupitia makala haya Jumia Travel imekukusanyia vigezo ambavyo mara nyingi huzingatiwa mpaka hoteli kupewa hadhi fulani.  

Nyota moja. Mara nyingi hoteli hizi humilikiwa na watu binafsi katika utoaji wa huduma za malazi kwa wateja. Huwa ni ndogo na za ukubwa wa saizi ya kati zikipatikana katika maeneo ambayo gharama za maisha ni ya kawaida kabisa. 

Kikubwa kinachozingatiwa ni kuweza kukidhi mahitaji ya msingi kwa gharama nafuu. Baadhi ya huduma zinazopatikana ni pamoja na mapokezi, kiti, meza, simu, luninga vyumbani, bafu na usafi wa kila siku. Ni chache zenye migahawa kwa ajili ya  chakula, mbali na hapo huduma na mhudumu kwa vyumbani huwa hakuna. 

Kwa hapa nchini Tanzania nyingi huwa ni nyumba za kulala wageni. Mfano wa hoteli  hizi ni kama vile Perfect Hotel na Sharon House Hotel.   

Nyota mbili. Hoteli za namna hii hazina tofauti sana za nyota moja kwani nazo zinapatikana kwenye maeneo ambayo gharama za maisha ni za kawaida pia. 

Mazingira na vitu vyake kama vile samani ni vya kawaida lakini vikiwa katika hali nzuri na safi. Asilimia kubwa huwa na huduma ya kifungua kinywa lakini si mgahawa. Pia zipo karibu na maeneo ambayo mteja anaweza kupata chakula kwa gharama nafuu. Wateja wanaweza kwenda muda wowote ingawa kuna ukomo ikifika muda fulani kama vile labda kuanzia saa tano usiku. Mfano wa hoteli hizi ni kama vile Golden Coins Hotel  na Four Points Hotel.  

Nyota tatu. Kwa kawaida hoteli za aina hii hutoa huduma ya vyumba vizuri, vikubwa vikiwa na mapambo ya kuvutia. 

Hupatikana katika maeneo makuu ya kibiashara na ya kisasa pamoja na maduka kwa ajili ya mununuzi. Huwa na mgahawa unaotoa huduma ya chakula kuanzia asubuhi mpaka usiku na dawati la mapokezi huwa wazi kwa takribani masaa 14. Mbali na hayo, mteja hufikishiwa huduma mpaka chumbani, maegesho ya magari, huduma ya kubebewa mizigo inapohitajika, sehemu ya kufanyia mazoezi na bwawa la kuogelea pia huwa vinapatikana. Mfano wa hoteli hizi ni kama vile Keys Hotel Moshi na Kilimanjaro Wonders Hotel.     
Nyota nne. Mara nyingi hoteli zenye hadhi hii huwa kubwa. Zina mandhari nzuri kuwavutia wageni, huduma ya mapokezi ambapo lugha zaidi ya moja inazungumzwa na wabeba mizigo kwa ajili ya wateja pia wapo. Hupatikana kwenye maeneo yaliyo 
karibu na hoteli zenye hadhi sawa na zao vilevile karibu na maduka makubwa ya manunuzi, sehemu za chakula na mandhari yenye vivutio vya hali ya juu. 

Huduma ni zenye ubora mkubwa, vyumba vya kisasa na samani za kupendeza. Huwa na mgahawa wenye vyakula zaidi ya aina moja kwa  machaguo ya wateja wa aina tofauti na pia huduma ya mteja kuhudumiwa hata akiwa chumbani kwake hupatikana. 


Hoteli zingine hutoa huduma ya kuwaegeshea magari au matengezo wateja wa pamoja na kuwasaidia na usafiri wa ndani ya eneo alilofikia. Kwa kuongezea, sehemu ya kufanyia mazoezi, bwawa moja la kuogelea au zaidi pia kawaida kupatikana kwenye hoteli za namna hii. Mfano wa hoteli hizi ni kama vile Gold Crest Hotel na Ramada Resort Dar es  
Salaam.     

Nyota tano. Hizi ni hoteli ambazo hutoa huduma za malazi na nyinginezo katika kiwango cha hali ya juu kabisa. Huwa na huduma kwa wateja binafsi zenye ubora wa 
kipekee. 


Ingawa mara nyingi hoteli za namna hii huwa ni ushirikiano wa makampuni makubwa lakini pia baadhi ya watu wachache huweza kutoa huduma sawa au kuzidi ushirika au makampuni 
makubwa. Maeneo zilizopo hutofautiana kutoka maeneo maalum au kuwa katikati au 
kitovu cha jiji kwenye shughuli nyingi za kibiashara. 

Unaweza kukuta hoteli ina migahawa mpaka mitatu na yote ikiwa na vyakula vya aina tofauti. Huduma mpaka vyumbani ni masaa 24 kwa kawaida pamoja na nyinginezo lukuki ambazo mteja 
atazihitaji. Mfano wa hoteli hizi ni kama vile Singita Sasakwa Lodge na Essque Zalu 
Zanzibar.

Kwa ujumla vipo vigezo vingi tu ukiachana na hivyo vichache viliyotajwa hapo juu. 

Mitandao na mashirika kutokea nchi mbalimbali imejaribu kufafanua na kuorodhesha kwa mujibu wa mahali walipo. 
Hivyo basi vigezo ambavyo vinatumika hapa Tanzania vinaweza visitumike au vikawa tofauti na kwingineko.

VIWANJA VINAUZWA BEI PIA VIPO KISEMVULE ,MKURANGA MKOANI PWANJ

$
0
0
 Sehemu ya viwanja hivyo vinavyoonekana nyuma ya Kiwanda cha Saruji cha Rhino kilichopo eneo hilo la Kisemvule.
 Kijana anayesimamia viwanja hivyo akionesha mipaka.
 Viwanja hivyo vikiwa vimepimwa na kuwekewa bicon
Mmoja wa wafanyabiashara alikiangalia viwanja hivyo kwa ajili ya kuvinunua.

VIWANJA VINAUZWA VIMEKWISHA PIMWA  UKUBWA WAKE NI 15X15 BEI NI SHILINGI MILIONI 2 NA NUSU NA VYENYE UKUBWA WA 30X30 NI SH. MILIONI 5 VIPO KIJIJI CHA KISEMVULE KATA YA VIKINDU WILAYA YA MKURANGA MKOANI PWANI JIRANI NA KIWANDA CHA SARUJI CHA RHINO BARABARA KUU YA KWENDA MIKOA YA KUSINI NA VIPO KATIKA MIUNDOMBINU YA BARABARA, MAJI NA UMEME, ANAYEVIHITAJI ANAWEZA KUWASILIANA MOJA KWA MOJA NA MUHUSIKA KWA NAMBA 0756430981.
Viewing all 1929 articles
Browse latest View live