TBL YQZINDUA KAMPENI YA 'CASTLE LITE UNLOCKS' JIJINI DAR ES SALAAM
HIVI NDIVYO INTERNETI INAVYO ATHIRI MAISHA YAKO YA KILA SIKU




TAMKO LA WAZIRI UMMY MWALIMU KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI
KILA MTANZANIA AHAKIKISHE ANALINDA MUUNGANO
Na. Immaculate Makilika, MAELEZO -DODOMA
Kila mtanzania ametakiwa kuhakikisha anafanya jitihada za kuimarisha na kulinda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa miaka 53 iliyopita.
Akizungumza leo wakati akihutubia wananchi katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano katika uwanja wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa ni muhimu watanzania wakalinda Muungano kwa vile una manufaa kwa nchi zote mbili.
“Kila mtanzania ahakikishe anafanya jitihada za kuimarisha na kulinda Muungano wetu, kwa vile Muungano na amani iliyopo nchini ndio chachu ya maendeleo yetu” alisema Rais Magufuli. Rais Magufuli alisisitiza kuwa “Muungano ndio silaha yetu, ni nguvu yetu, mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda Muungano kwa nguvu zote na yeyote atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye” alisema Rais Magufuli.
Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika miaka 53 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni pamoja na kuunganisha mataifa mawili na kuunda taifa moja lenye nguvu. Rais Magufuli alisema mafanikio mengine ni pamoja na kuwa ni kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini, nchi kavu na reli, kukabiliana na matatizo ya umaskini, ukosefu wa ajira na kukua kwa uhusiano wa diplomasia kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali ambapo yamepelekea mafanikio katika nyanja za kiuchumi, kisiasa, na jamii.
Aidha, hii ni mara ya kwanza kwa sherehe za Maadhimisho ya Muungano kufanyika mkoani Dodoma ambapo, Rais Magufuli alisema kuwa Serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kujenga miundombinu ili kufikia azma yake ya kuhamishia makao yake makuu mjini Dodoma ifikapo mwaka 2020.
“Niwahakikishie wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi nyuma tena,ambapo awamu ya kwanza ya watumishi wa Serikali takribani 3,000 kwa ngazi za Mawaziri,Naibu Waziri,Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu wameshahamia Dodoma, kama tulivyoahidi kufikia mwaka 2020, Serikali yote itakuwa imehamia hapa”, alisisitiza Rais Magufuli.
Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano zenye kauli mbiu isemayo “Miaka 53 ya Muungano, tuulinde na kuimarisha, tupige vita dawa za kulevya na kufanyakazi kwa bidii”, zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano ambapo ni Mama Maria Nyerere na Mama Shadya Karume.
IVORY YAPANIA KUPAA ANGA ZA MUZIKI WA DANSI



SSRA YASHIRIKI MAONESHO YAUSALAMA MAHALI PA KAZI MKOANI K'NJARO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama akiatoa maelekezo wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwenye Maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa kazi (OSHA) yanayoendelea mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama, akimkabidhi cheti cha Ushiriki Kaimu Meneja wa Rasilimali watu na Utawala wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Bi. Amina Ally wakati wa kilele cha maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yanayoendelea Mjini Moshi, mkoani, Kilimanjaro.
Afisa Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), akigawa vipeperushi kwa wananchi waliotembelea banda la SSRA wakati wa Maonesho ya OSHA yanayondelea Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Afisa Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Ally Masaninga akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la SSRA, wakati wa Maonesho ya OSHA yanayondelea Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Maafisa wa SSRA, wakitoa ufafanuzi juu ya Masuala yanayohusu Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wadau waliotembelea banda la mamlaka hiyo, wakati wa Maonesho ya OSHA, yanayoendelea Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Wananchi wakisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa SSRA, wakati wa maonesho ya OSHA, yanayofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Wadau waliotembelea banda la SSRA, wakijipatia vipeperushi wakati wa maonesho ya Maadhmisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yanayofanyika Mkoani Kilimanjaro.
MKUU WA MKOA WA PWANIMHANDISI NDIKIRO AISHUKURU TANESCO KWA MSAADA WA USAFI
![]() |
Wafanyakazi wa TANESCO wakifagia mazingira kuzunguka kituo hicho |
DKT. MWANYEMBE AHWATAKA VIJANA KUTENGA MUDA WA KUJISOMEA
Mwandishi wa vitabu Ritha Tarimo akiongea na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha 'Colour of Life'. |
NEC YATANGAZA NAFASI YA WAZI KITI CHA MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA DR. ELLY MARKO
TAASISI YA KILIMANJARO DIALOGUE WAADHIMISHA SIKU YA UHURU WA HABARI DUNIANI
Mdhamini wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. Kutoka kulia ni Rais wa taasisi hiyo, Ali Akkiz na Mshauri wa masuala ya Habari, Felix Kaiza.
Mshauri wa Masula ya Habari, Felix Kaiza akielezea umuhimu wa wamiliki wa vyombo vya habari kuweka utaratibu wa mafunzo ya ndani (In House Training) kwa waandishi wa habari ili kuinua weledi pia alishauri kuwepo na Exchange Program kati ya vyombo vya habari nchini na nje ya nchini jambo ambalo huwaongezea uwezo wanahabari.
Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten, Esther Zaramula akielezea kwenye mjadala huo jinsi alivyonufaika na mpango wa kubadilishana uzoefu
Habib Miradji akisisitiza jambo wakati wa mjadala huo ambapo alifafanua zaidi umuhimu wa wanahabari kuandika habari kwa kufuata maadili na kusimamia kwenye ukweli.
Pia katika kongamano hilo waliwaasa wanahabari kutojiingiza katika mkumbo wa kuingizwa mifukoni mwa wanasiasa na matajiri kwa kuandika habari za kuwasifia wao badala ya maslahi ya wananchi.
Mwandishi wa habari, Ezekiel Kamwaga akielezea umuhimu wa wanahabari kujiendeleza kielimu pamoja na vyombo vya habari kubadilika kwa kwendana na kasi ya mabadiliko ya kizazi hiki cha maendeleo ya teknolojia ya habari.
Rais wa taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Ali Akkiz aktoa shukrani kwa wanahabari walioshiriki kwenye mjadala huo uliofanikiwa.
UFAFANUZI KUHUSJ UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA IKIMWI
Kumekuwepo na taarifa iliyoandikwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za Clouds Media Group za Facebook na Instagram ikimnukuu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Grace Magembe akisema kuwa ‘‘Upimaji wa VVU nyumba kwa nyumba sasa rasmi, mchakato unaendelea na zoezi litaanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu“.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa mara nyingine, inapenda kutoa ufafanuzi kwamba UKIMWI haupimwi nyumba kwa nyumba bali inafanya utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania ambapo UKIMWI ni ugonjwa mmojawapo unaopimwa katika utafiti huu.
Aidha, utafiti huu unafanyika kwenye kaya chache ambazo zimechaguliwa kitaalam nchi nzima ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine ambazo hazihusiki moja kwa moja.
Utafiti huu unajumuisha kaya zipatazo 16,000 ambazo ni sampuli iliyochaguliwa kisayansi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na unahusisha watu wazima wasiopungua 40,000 na watoto takribani 8,000. Kwa Dar es Salaam, utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI utahusisha kaya zisizozidi 1,000 kati ya kaya 1,000,000 na unatarajia kuanza tarehe 31 Mei, 2017 na kuendelea kwa wiki zisizozidi tatu (3).
Mbali na upimaji wa UKIMWI, utafiti huu pia unapima kiwango cha maambukizi ya Kaswende, Homa ya ini (Hepatitis B), uwepo wa viashiria vya usugu wa dawa, maambukizi mapya ya VVU, kiwango cha VVU mwilini kwa watu wanaoishi na VVU (Viral load), wastani wa maambukizi ya VVU kwa watu wa rika zote pamoja na wingi wa chembechembe za kinga mwilini (CD4 T-cell count). Aidha, kupima ni hiari na watakaogundulika kuwa na maambukizi, watapata rufaa ya kwenda kupatiwa matibabu bure katika vituo vya kutolea huduma za afya. Ifahamike kwamba, utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016/17 unafanyika nchini kwa mara ya nne (4) ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003, wa pili mwaka 2007 na wa tatu mwaka 2011.
Hivyo, NBS inapenda kuwatoa hofu Wananchi kuwa, kufanyika kwa utafiti huu sio jambo jipya na Watanzania ambao wamekuwa wakipitiwa na utafiti huu, wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa zaidi ya asilimia 90 na mpaka sasa utafiti huu umeshafanyika katika mikoa 17 ya Tanzania Bara na kwa upande wa Tanzania Zanzibar, utafiti huu umekamilika katika maeneo yote yaliyochaguliwa.
Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania unaendelea kufanyika nchini, ukisimamiwa na NBS kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya kwa Tanzania Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS), Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC). Imetolewa na: Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
WAANDISHI WATAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO VIZURI
Na Nuru Juma & Husna Saidi- MAELEZO
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za uandishi katika kuandika habari zitakazoleta umoja,mshikamano na maendeleo na siyo uchochezi ili kujenga jamii bora.
Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison George Mwakyembe kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani. Dkt. Mwakyembe aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo siku hiyo huwa maalum kwa wadau wa tasnia hiyo kukutana na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwa ni njia ya kujenga jukwaa la ushirikiano.
“Uhuru wa habari una ukomo wake hivyo ni muhimu kwa vyombo vya habari hapa nchini kuajiri watu wenye taaluma hiyo kwa kuachana na makanjanja ili viheshimike kwa kutoa taarifa zenye kuzingatia maadili ya uandishi”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Alifafanua kuwa katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kalamu ya mwandishi wa habari itetee ukweli na si mambo ya haramu kwa sababu ya siasa au rushwa ambayo huwa kichocheo cha uvunjifu wa amani.
Aidha aliitaka Idara ya Habari (MAELEZO) kuwa na utaratibu wa kukutana na wahariri kila mwezi ili kuweza kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia nzima ya habari nchini. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi alisema uandishi wa habari si biashara ya kawaida bali ni kazi yenye kuhitaji uweledi mkubwa hivyo waandishi wanatakiwa kufuata taratibu na sheria za uandishi.
SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI SUALA LA VYETI FEKI
WAZIRI LUKUVI AMTUMBUA OFISA MIPANGO MIJI LINDI
WAZIRI MWAKYEMBE AMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUTUMIA LUGHA YA KISWAHILI KAMA UTAMBULISHO WA KITAIFA
NKAMIA AKIMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KUWA KIONGOZI MZURI
ATCL KUPATA NDEGE MPYA JULAI MWAKA HUU
Na Vicent Tiganya Tabora
Serikali imesema kuwa mwezi Julai mwaka huu (2017)itanunua ndege nyingine mpya aina ya Dash 8-Q 400 kwa ajili kuliimarisha Shirika la Ndege la Tanzania ili liliweze kutoa kutoa huduma za usafiri wa anga katika maeneo mengi ndani na nje ya nchi.
Hatua hiyo itaiweza ATCL kufikisha ndege nne (4) ambapo itaiwezesha kuongeza safari zake kwa kuhudumia masoko yake ya ndani na miji ya nchi jirani kama vile Kenya, Uganda, Burundi , Rwanda, Malawi, Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC).
Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilano Mhandisi Edwin Ngonyani wakati wa uzinduzi wa Safiri za Ndege za Shirika la ATCL mkoani Tabora.
Alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa hadi kufikia Julai mwakani (2018)Shirika la Ndege hapa nchini linakuwa na uwezo wa kumiliki Ndege sita zenye uwezo wa kubeba abira kwa kiwango tofauti tofauti na kusafiri mikoa mingi hapa nchi na nje ya Tanzania.
Naibu Waziri huyo alisema kuwa hadi hivi sasa , serikali imeshanunua ndege mbili aina ya Bombardier Dash 8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja.
Alisema kuwa hatua inayofuata ni ununuzi wa ndege nyingine tatu aina ya Bombardier Dash 8-Q400 ambayo itakuwa na uwezo kubeba abiria 76, CS 300 mbili zitakazobeba abiria 132 kila moja na Boeing 787 (Dreanliner ) itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 262.
Aidha Ngonyani alisema kuwa lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuhakikisha inaimarisha viwanja vya ndege kwa kukarabati miundombinu na kuboresha mifumo mbalimbali ya huduma za usafiri wa anga.
Alisema kuwa hatua hiyo inaenda sanjari uimarishaji wa Shirika la Ndege hapa nchini na ujenzi wa viwanja vipya vya ndege katika mikoa ambayo haina viwanja hivyo kwa sasa.
Ngonyani alisema kuwa Serikali kupitia Shirika lake imekusudia kuhakikisha kuwa mikoa yote hapa nchini inaunganisha na usafiri wa anga.
Alitoa wito kwa kwa wananchi kutumia usafiri wa anga hasa wa Shirika hilo kama huduma ya kawaida na ya kuongeza fursa ya kibiashara kwa ajili kuimarisha kipato kuanzia ngazi ya familia hadi taifa.
Ngonyani aliwaomba wakazi wa Tabora na maeneo mengine hapa nchini kutumia huduma za usafiri wa anga katika kutanua wigo wa biashara zao na kuhamasisha utalii na kuimarisa sekta ya kilimo cha kisasa hapa nchini.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho alisema kuwa Shirika la Ndege hapa nchini linatoa huduma nafuu ukilinganisha na mashirika mengine yanayotoa huduma hiyo hapa nchini.
Alisema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia usafiri huo na kutokuwa wa watu wachache kama yalivyo mashirika mengine hapa nchini. Dkt. Chamuriho alisema kuwa Shirika hilo linatoza gharama nafuu ukilinganisha na Kampuni nyingine zinazotoa huduma za usafiri wa anga hapa nchini.
Alisema kuwa hivi sasa kutoka Dar es salaam kwenda Tabora kwa safari mmoja ni shilingi 330,000 na kutoka Tabora kwenda Dodoma ni shilingi 250,000 Dkt. Chamuriho aliongeza kuwa safari ya kwenda na kurudi kutoka Dar es salaam kwenda Tabora kwa safari mmoja ni shilingi 499,000 na kutoka Tabora kwenda Dodoma ni shilingi 380,000.
Wabunge wa Mkoa wa Tabora na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemshuru Rais Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahidi yake kwa vitendo kwa kuanza kiliimarisha upya Sherika la Ndege hapa nchini.
Waliomba Serikali kupitia Shirika la ATCL kuendelea kupunza nauli za usafiri wa ndege ili wananchi wengi waweze kutumia usafiri wa anga hasa kupitia Shirika lao.
Wamesema kuwa haitakuwa na maana kama nauli zitakuwa juu na wananchi kuona usafiri wa anga ni watu matajiri tu.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ametoa wito kwa wawekeza popote ndani na nje ya nchi kwenda mkoani humo kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo kufuatia kuimarika kwa miundo mbinu mbalimbali ikiwemo usafiri wa anga, barabara na mawasiliano ya simu.
Alisema kuwa Tabora inayoa ardhi nzuri inayokubali ufugaji na ukilima wa mazao mbalimbali kama vile tumbaku, mahindi, alizeti mbunga, karanga miazi, mihogo na mengine mengine hatu inayowezo kuwawezesha kufunga viwanda vidogo na vikubwa. Kwa mujibu wa ratiba ya safari za ndege za Shirika hilo mkoani Tabora zitakuwa Jumatau, Jumatano Ijumaa na Jumapili.
BURIANI MWANAHABARI REVOCATUS BULIZYA
RC GAMBO AWALILIA WATOTO 32 WALIOFARIKI KWA AJALI KARATU
Pichani wanafunzi wakisubiri basi kabla ya kuanza safari ambapo walikutwa na mauti
Mwanafunzi mmoja aliyenusurika kwenye ajali hiyo jina halikufahamika.
Mzazi wa mmoja wa marehemu akilia kwa uchungu.
Baadhi ya watu wakishuhudia basi hilo likiwa limetumbukia kwenye bonde,pia wakitoa msaada,
Baadhi ya miili ya wanafunzi hao walifariki kwenye ajali hiyo.
Hili ni kati ya mabasi ya shule hiyo ya Lucky Vincent lililokuwa kwenye msafara huo.
Blog hii inatoa mkono wa pole kwa wazazi wote wa marehemu waliopiteza watoto wao, Mungu azilaze roho zote mahala pema peponi Amin.