TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YAFAFANUA HATMA YA UBUNGE WA SOFIA SIMBA
RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASASTANDARD GAUGE DAR HADI MOROGORO
Na Immaculate Makilika- MAELEZO
Tanzania inatarajiwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na reli ya kisasa inayotumia umeme na mafuta itakayokuwa na uwezo wa kusafiri masafa marefu kwa mwendokasi wa kilometa 160 kwa saa.
Akizungumza leo katika uwekaji wa jiwe la msingi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hiyo ya leo huko Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alisema kuwa reli hiyo itakuwa ya kisasa zaidi barani Afrika na itasaidia kukuza uchumi wa nchi kwa kuchochea fursa za biashara ndani na nje ya nchi.
Awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli hiyo ambayo itahusisha kipande cha kilomita 300 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro utagharimu jumla ya shilingi trilioni 2.8 na utatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 30.
Dkt Magufuli alitoa mfano wa nchi zenye reli za mwendokasi lakini masafa mafupi barani Afrika kuwa ni Morocco ambayo inasafiri kwa mwendokasi wa kilomita 220 kwa saa na Afrika Kusini inayosafiri mwendokasi 150 kwa saa.
Dkt Magufuli alieleza kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na treni itakayosafiri masafa marefu kwa mwendokasi wa km 160 kwa saa.
Alifananua kuwa mradi huo wa ujenzi wa reli unatekelezwa kwa fedha za Tanzania ambapo tayari serikali imeshawalipa wakandarasi malipo ya awamu ya jumla ya shilingi bilioni 300.
Akizungumzia umuhimu wa ujenzi wa reli hiyo, Rais Magufuli alisema kuwa reli hiyo itasaidia kuongeza kasi ya usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam kwa haraka na kuwafikia wateja ndani ya muda mfupi.
Vilevile, reli hiyo itarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo pamoja na kukuza biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudani ya Kusini.
Sambamba na hayo, Rais Magufuli alisema kuwa ujenzi wa reli hiyo utasaidia kuimarisha sekta nyingine za uchumi ikiwemo utalii, viwanda, kilimo, pamoja na kutoa ajira kwa watanzania ambapo kutakuwa na ajira muda zipatazo 600,000, na ajira za kudumu 30,000.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema kuwa reli hiyo ya kisasa inayojengwa na wakandarasi kutoka muungano wa kampuni mbili za nchi ya Uturuki na Ureno itakuwa na uwezo wa kusafirisha mizigo tani 10,000 kwa mara moja na kutumia saa 2 kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na saa 7 na dakika 40 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
Naye, Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya ujenzi kutoka Uturuki ya Yapi Merkezi Bw. Emre Aykar alisema kuwa reli hiyo itaimarisha zaidi uhusiano wa Uturuki na Tanzania na kuongeza kiwango cha shughuli za biashara nchini.
“Tunaahidi kujitahidi kumaliza mradi kwa wakati na katika kiwango kinachotakiwa” alisema Bwana Aykar.
Reli hiyo ya kisasa inatarajiwa kujengwa pembeni ya reli ya kati ambayo ilijengwa wakati wa utawala wa kikoloni wa Wajerumani na Waingereza miaka 112 iliyopita.
SERIKALI KUFANYA MAREKEBISHO SHERIA YA NDOA YA MWAKA 1971
Na Daudi Manongi-MAELEZO, Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imesema inaendelea na mchakato wa ndani wa kufanyia marekebisho ya kuhuisha na kuimarisha maeneo yaliyo mazuri ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 na kuwasilishwa Bungeni ili kuendana na wakati.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof.Palamagamba Kabudi wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.
“Serikali inaendelea na mchakato huu wa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria hii Bungeni ili iweze kuendana na wakati kwa kuondoa upungufu uliopo kwa maslahi mapana ya nchi yetu”,Aliongeza Mhe.Kabudi.
Amesema kuwa baada ya miaka 20 kupita tangu sharia hiyo ya ndoa itungwe,Serikali kupitia tume ya kurekebisha Sheria iliifanyia mapitio ya sheria hiyo na kubaini maeneo kadhaa yenye udhaifu na hivyo kuhitaji kufanyiwa marekebisho.
Amebainisha kuwa Kutokana na maoni hayo ya tume,mwaka 2008 Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria iliandaa waraka wa baraza la Mawaziri uliokuwa na mapendekezo ya marekebisho ya sharia ya ndoa ya mwaka 1971,hata hivyo desemba 2010 kabla waraka huo kujadiliwa na kuridhiwa na baraza la Mawaziri mchakato wa mabadiliko ya katiba ya jamhuri ya muungano ukaanza na kulilazimu Baraza kusitisha kwa muda mchakato huo.
“Serikali ilikuwa na matarajio kuwa wakati tume ya mabadiliko ya katiba inakusanya maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko ya katiba,wananchi wangetoa maoni kuhusu Sheria ya ndoa pamoja na sheria nyingine zinazofanana na hiyo na hivyo maoni yaliyotolewa wakati wa Sheria ya Ndoa yalikuwa machache sana”Alifafanua Mhe.Kabudi. Sheria ya ndoa mwaka 1971 ni matokeo ya mjadala mpana na shirikishi kupitia waraka wa Serikali namba moja wa mwaka 1969.
TASNIA YA HABATI YAPATA PIGO, ISANGO AMEFARIKI DUNIA LEO
Marehemu Isango atakumbukwa kutokana na mchango wake mkubwa katika uandishi wa habari za siasa na jamii kwa ujumla.Nyota ya fani ya uanahabari ilishamiri alipokuwa ameajiriwa na Kampuni ya Free Media Limited ambao ni Wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima na baadaye alihamia gazeti la Mwana halisi.Mazishi ya Isango yatafanyika Jumamanne Mkoani Singida.
RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI MAUAJI YA ASKARI 8 KIBITI MKOANI PWANI
DAWASA UKINGONI KUKAMILISHA KAZI
![]() |
Mafundi wa TANESCO wakiwa kwenye ukaguzi katika eneo la Chalinze (Sub-station) ambapo laini ya umeme unaoelekea katika mtambo wa Ruvu Juuinapoanzia. |
![]() |
Mtaalam wa Kitengo cha Umeme Mkubwa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Emmanuel Haule (kushoto) akikagua mitambo mipya inayotarajiwa kupokea umeme na kutembeza pampu mpya. |
Hii ni Transfoma mpya iliyopo katika eneo la Mtambo wa Ruvu Juu ambalo kwa sasa linafanya kazi vizuri ya kutoa umeme kwa ajili ya mitambo. |
Mtambo mpya wa kusukuma maji wa Ruvu Juu kama unavyoonekana, mtambo huu unafanya kazi vizuri ya kusukuma maji. |
Hii ni sehemu ya mtambo wa kuwashia na kuongoza mitambo inayofanya kazi ya kusukuma maji eneo la Ruvu Juu kama unavyoonekana. |
Hili ni eneo la mtambo wa maji wa Ruvu Juu ambapo maji husafishwa na kisha kupelekwa katika mtambo mwingine kwa usafishaji zaidi na kisha kusafirishwa kwa wananchi. |
Hili ni jengo la Utawala la Ruvu Juu ambapo shughuli za masuala ya maji zinafanywa na watendaji wake. |
Hili ni eneo la mtambo wa maji wa Ruvu Juu ambapo maji yaliyosafishwa toka mitamboni hupitia ikiwa ni hatua ya mwisho tayari kusafirishwa kwenda kwa wananchi. |
Hili ni bomba kubwa la maji safi la Ruvu Juu ambapo maji yaliyosafishwa toka mitamboni hupitia na kupelekwa sehemu ya kuyasafirisha kwenda kwa wananchi. |
Hili ni eneo la mtambo wa maji wa katika eneo la IN TAKE lililopo katika Mto Ruvu na ndiyo sehemu maji hunyonywa na mitambo na kuyapeleka eneo la Ruvu Juu kwa ajili ya kusafishwa. |
Hii ni sehemu ya mtambo wa kuwashia na kuongoza mitambo inayofanya kazi ya kusukuma maji eneo la IN TAKE lililopo Mto Ruvu. |
Hii ni mitambo ya kusukuma maji iliyopo katika eneo la IN TAKE katika eneo la Mto Ruvu na ndiyo sehemu inayofanya kazi ya kukusanya na kusukuma maji kuelekea Ruvu Juu. |
Hili ni jengo la IN TAKE ambapo ndani ndipo iliposimikwa mitambo inayotumika kusukuma maji kuelekea eneo la Ruvu Juu kwa ajili ya kusafishwa na kusambazwa kwa wananchi. |
Hili ni Transfoma kubwa lenye uwezo wa 45/55 MVA na ndiyo linalotoa umeme kupeleka eneo la Ruvu Juu kwa ajili ya kusukuma maji. |
Article 2
ASKOFU DKT.ALEX MALASUSA AONGOZA IBADA YA IJUMAA KUU KANISA LA KKKT USHARIKA WA AZANIA FRONT JIJINI DAR ES SALAAM
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAANZA KUKUSANYA MAONI KUTOKA KWA WADAU WA UTALII
DUKA LA KISASA LA GSM MALL LAUNGUA MOTO
Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwahishwa hospitali.
Pilikapilika katika lango kuu la kuingilia duka hilo
Mmoja wa majeruhi akitolewa kwenda kwenye gari ili awahishwe hospitali kwa matibabu
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya moto
Na Richard Mwaikenda
DUKA kubwa la GSM Mall ililopo Barabara ya Nyerere eneo la Mtava, Dar es Salaam, linateketea kwa moto hivi sasa.
Kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba duka hilo lilianza kuungua majira ya 8;30,hadi sasa chanzo cha moto huo hakijaweza julikana.
Magari ya zimamoto na uokoaji yamejazana eneo hilo kunusuru mali na maisha ya watu waliokuwemo kwenye jengo hilo lenye ghorofa nne.
Watu wengi wakiwemo wafanyakazi wa duka hilo walionekana kutoka mkuku kuokoa maisha yao.
Duka hilo kubwa la kisasa lenye maduka yenye aina mbalimbali za bidhaa ni moja kati ya maduka makubwa yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Waokoaji waliokuwepo wamepata wakati mgumu kuzima moto kutokana na ndani ya jengo hilo kuwa na giza nene lililotawaliwa na wingu la moshi uliosababishwa na moto huo.
Wamejitahidi kupata mwanga kwa kuwasha taa za magari karibu na lango kuu la kuingilia ndani lakini ilishindikana.
RAIS MAGUFULI AAGIZA TCU KUTOWACHAGULIA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU VYUO
MIILI YA ASKARI NANE WALIOUAWA NA MAJAMBAZI KIBITI YAAGWA RASMI ,WAZIRI MWIGULU ATANGAZA KIAMA KWA WATUHUMIWA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba, akitoa pole kwa wafiwa.
Askari waliopoteza maisha katika tukio hilo la kinyama wametajwa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub
MKURUGENZI JIJI ARUSHA ATOA SEMINA KWA WATUMISHI WAKE
Na Mwandishi Wetu, Arusha
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Juma Kihamia amefanya kikao na watumishi wa serikali katika Kata ya Muriety na Terati na kuzungumza mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuboresha utendaji kazi wao.
Kihamia amesema kuwa lengo hasa la kuonana na watumishi hao ni muendelezo wa ziara yake ya kutembela kila Kata na kuwakumbusha watumishi hao jinsi ya kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya Raisi John Magufuli.
“Siyo kwamba watumishi wangu wa Halmashauri hawafanyi kazi bali ni kuwakumbusha majukumu yao katika kutumikia wananchi hasa katika kasi ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu ambayo inatutaka tuwe karibu zaidi na wananchi wetu na mimi kama mtendaji mkuu lazima nisimamie kikamilifu alisema Kihamia.
Vile vile amesema kuwa watendaji wa serikali wanatakiwa wajitume kwa nguvu zote wasisubiri mpaka viongozi wa juu wafike kwenye maeneo yao na wananchi walalmike wakati kuna kiongozi katika eneo hilo ambaye analipwa na serikali ili kusaidia wananchi.
" Hatutaki mwananchi atoke kwenye Kata mpaka kwa mkuu wa Mkoa au mkuu wa Wilaya wakati kwenda kumlalamikia masuala madogo madogo wakati kuna kiongozi ambaye tumemuweka ili atatue kero akitokea Mtumishi wa hivyo ajue kwamba hatoshi kuongoza wananchi ”alisema Kihamia
Ameongeza kuwa kwasasa anahakikisha Huduma zinaboreshwa katika jiji la Arusha kwa kumjengea mtumishi uzoefu wa kufanya kazi bila kuogopa changamoto zilizopo na kuwa jasiri wakati anaongoza wananchi kwenye maeneo yao.
Hata hivyo amewagiza watumishi hao wa serikali wakiwemo watendaji kutekeleza kwa muda uliowekwa mambo muhimu kama vikundi vya vijana na Wanawake, kuainisha maeneo ya biashara na idadi yake ikiwemo mabango na maduka yote,majengo na miradi viporo pamoja na kuainisha Yale maeneo yote ya wazi.
RAIS MAGUFULI ATOA AJIRA KWA MADAKTARI 258 WALIOOMBA KWENDA KENYA
DAWASCO YAKAMILISHA UPANUZI WA MTAMBO RUVU JUU SASA WAZALISHA MAJI SAFI NA SALAMA LITA1962
Maji yakiingia toka katika mitambo ya kunyonya maji tayari kwa kusafishwa kwa kuweka dawa ndani ya eneo hili na kisha kupelekwa katika mtambo mwingine wa kusafisha maji tayari kwa kusafirishwa. |
Mtambo huu ni sehemu ambapo maji huendelea kusafishwa na kisha kupelekwa katika mtambo maalum wa kukusanya na kusafirisha kwenda kwa wananchi. |
Matanki makubwa ya maji yenye mitambo maalum ya kusafisha maji kama inavyoonekana hapa maji yakiendelea kusafishwa. |
Sehemu hii ni ya mtambo ambapo maji yanawekwa dawa na kisha kupelekwa katika sehemu ya mtambo mwingine kwa ajili ya kusafishwa na kusafirishwa kwa wananchi. |
MSANII WA BONGO FLEVA NILLAN AMPONDA SHILOLE
MSANII wa Bongofleva anayetamba na kibao cha ‘Njenje’ Gilbert Paul maarufu kama ’ Nillan' (pichani kulia) ameponda kitendo kilichofanywa na msanii mkubwa katika tasnia hiyo Zuwena Yusufu ‘Shilole’ cha kuharibu Show iliyotarajiwa kufanyika mkesha wa siku ya mkesha wa Pasaka na hivyo kusababisha hasara kwa Promota.
Nillan aliyetarajiwa kufanya show siku pamoja na msanii mwingine Nuhu Mziwanda alisema kitendo kilichofanywa na Shilole siyo cha kiungwana kutokana na heshima kubwa aliyonayo msanii huyo kwa Taifa hili.
“Ukweli kitendo hicho mimi kama msanii chipukizi kimeniumiza sana, sikutaraji kingeweza kufanywa na msanii mkubwa na maarufu kama Shishi, namuheshimu kama dada yangu lakini kwa hili amejishushia heshima” alisema Nillan.
Show hiyo iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni ya Merry Merry Entertainment, ilishindwa kufanyika baada ya Shilole kuchelewa kufika ukumbini hali iliyosababaisha mashabiki waliofika mahali hapo kulalamika warudishiwe fedha zao na baadae kuondoka.
Akizungumzia baada ya tukio hilo Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Merry Mussa mbali na kulaani kitendo hicho cha Shilole alisema ni lazima sharia itafuata mkondo wake kwa msanii huyo kulipa hasara yote iliyotokana na kitendo alichokifanya.
“Haiwezekani mtu tukubaliane afike ukumbini saa 2 usiku, yeye anakuja muda anaotaka, na hapo hapo hata kushuka kwenye gari hakushuka, hiyo ni dharau na kamwe sikubaliani na kitendo hicho hata kidogo” alisema Merry.
Shilole aliyetarajiwa kutoa burudani siku hiyo ya mkesha wa Pasaka katika ukumbi wa Heinken uliopo Kijichi, aliwasili ukumbini hapo saa 7 za usiku tofauti na makubaliano na Promota aliyeandaa show hiyo.
Hata hivyo alipotafutwa Shilole kuzungumzia suala hilo alidai kufika ukumbini hapo kama taratibu zilivyo za wasanii kufika kwenye show mbalimbali hivyo haoni kama kuna kosa lolote alilifanya kuhusiana na show hiyo.
Kwa upande wake Nuhu Mziwanda aliyewah kuwa mahusiano na msanii huyo alikwenda mbali na kusema kitendo kilichofanywa na mpenzi wake huyo wa zamani ni ushamba na kumtaka kurudisha fedha alizochukua kutoka kwa promota.
Alisema anashangazwa kwanini Shilole alikubali kupokea fedha hizo na kuahidi kufanya show lakini badala yake akaingia mitini na kuibukia ukumbini muda ambayo show ilipaswa iwe mwishoni.
Akizungumzia suala hilo Meneja wa kampuni ya Ochu Entertainment inayomsimamia msanii Nillan, Felix Mkuya alisema kitendo kilichofanywa na Shilole ni cha kushangaza na hakipaswi kufanywa na wasanii wa hapa nchini.
“Imagine watu wametumia gharama kubwa kuandaa ile Show, kila msanii alishapewa hela yake mkononi, sasa kwanini yeye afanye vile, Nuhu Mziwanda alifika ukumbini mapema saa 12 jioni, alikadhalika kwa Nillan…sasa vipi Shilole afanye vile” alihoji Mkuya.
VIJANQ DAR WAANZISHA KLABU ZA KUPINGA MABADILIKO
Na Dotto Mwaibale
WANAWAKE KANISA LA PENTEKOSTE WAOMBA AMANI NCHINI ISUMISHWE
Hapa ni furaha tupu wakati mgeni rasmi akisindikizwa kuingia kanisani |
NGORONGORO KITOVU CHA UTALII KINACHOWAVUTIA WATU MASHUHURI DUNIANI
Inaonekana mwaka 2017 umeanza vizuri katika sekta ya utalii nchini Tanzania kutokana na watu kadhaa mashuhuri kuzuru vivutio vyake. Sehemu ambazo zimeonekana kuwavutia watu wengi zaidi ni hifadhi ya mbuga ya Serengeti na bonde la Ngorongoro.
Alianza mwigizaji maarufu wa filamu kutokea Hollywood nchini Marekani, Will Smith na mkewe Jada Pinkett-Smith. Mwanzoni mwa mwezi Machi walitua nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kujivinjari katika mbuga ya Serengeti. Wakiwa huko familia ya Smith walikutana na msanii mwingine kutokea huko huko Marekani, lakini huyu yeye ni mwanamitindo na mrembo, Chanel Iman.
Haikupita muda mrefu sana tangu watu hao mashuhuri kuwepo nchini, kwani siku chache zilizopita aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Taifa la Israel, Bw. Ehud Barak naye alitembelea mbuga ya Serengeti pamoja na Ngorongoro.
Hii ni ishara nzuri kwa sekta ya utalii nchini ambapo kupitia watu hawa maarufu wengine nao wanapata taarifa na kuhamasika kutembelea pia.
Lakini lazima tujiulize ni kwa nini Ngorongoro huwavutia watu zaidi na kuwafanya kufunga safari kuja Tanzania na sio sehemu zingine? Jumia Travel imekukusanyia vitu ambavyo vinapatikana katika eneo hilo la urithi wa dunia ambalo hakuna mtu atakayesimuliwa na kutotaka kulitembelea:
Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Kama ulikuwa haufahamu bonde la Ngorongoro ni shimo kubwa lililotokana na mlipuko wa volkeno ambalo halijai maji wala kubomoka duniani. Eneo hili ambalo limetangazwa kuwa ni urithi wa dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO); lina urefu wa kilometa 20, kina cha mita 600 na ukubwa wa kilometa za mraba 300.
Vifuatavyo ni vivutio vinavyopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro:
Binadamu na Wanyama kuishi pamoja. Kwa zaidi ya miaka 200 iliyopita watu wa kabila la Wamasai walifika eneo hili na kuishi hapo. Maisha yao ya jadi yamewafanya waweze kuishi pamoja na mifugo yao kwa amani na utulivu kabisa bila ya kuwabugudhi wanyamapori. Mpaka hivi sasa kuna wafugaji wa Kimasai takribani 42,000 wakiishi katika hifadhi pamoja na mifugo yao kama vile ng’ombe, punda, mbuzi na kondoo. Kipindi cha mvua hutoka eneo hili na kuelekea maeneo ya tambarare ambapo kiangazi kikifika hujisogeza maeneo ya karibu ya mlima na misitu iliyopo. Wamasai huruhusiwa kuingiza mifugo yao kwa ajili ya kuilisha na kuinywesha lakini si kufanya shughuli za kilimo; lakini maeneo mengine ya hifadhi wanaruhusiwa kurandaranda.
Bonde la Volkeno na Wanyamapori. Bonde la Ngorongoro lilitokana na mlipuko wa volkeno takribani miaka milioni 3 iliyopita ambapo ni kubwa, lisilobomoka wala kutojaa maji. Lilitangazwa na UNESCO kuwa ni urithi wa dunia mwaka 1979 na ni eneo pekee ambalo binadamu, mifugo na wanyama wanaishi kwa pamoja kwa amani na utulivu kabisa. Unaweza kukuta kuna wakati ng’ombe wa Wamasai wanachunga pamoja na pundamilia katika mbuga za Ngorongoro.
Masalia ya Kale ya Binadamu wa Mwanzo. Ngorongoro ndimo linapopatikana bonde la Olduvai ambalo kwa mujibu wa wanahistoria yanapatikana masalia ya binadamu wa mwanzo kuishi duniani. Hapa ndipo wanaikolojia maarufu Dkt. Louis na mkewe Mary Leakey walipata masalia ya kale likiwemo fuvu la mtu wa kale zaidi, Zinjanthropus, ambaye alipata kuishi miaka milioni 1.75 iliyopita. Utafiti wao uliweza kuvumbua mabadiliko ya taratibu ya ukubwa wa ubongo na zana zao za mawe walizokuwa wanazitumia.
Vivutio vingine. Mbali na vivutio vilivotajwa hapo juu pia kuna vitu vingine chungu nzima vya kuvutia watu wanavyoweza kuvifurahia kuviona.
Ziwa Ndutu na Masek; maziwa haya hujaa kutokana na maji yanayotiririka kutokea milimani, na maji yake hayafai kwa matumizi ya binadamu kutokana na chumvi nyingi iliyonayo.
Oldonyo Lengai; hili ni jina la lugha ya Kimasai likiwa na maana ya ‘Mlima wa Mungu,’ unapatikana nje kidogo ya hifadhi ya Ngorongoro. Ni mlima pekee wenye volkeno hai ambapo ilishawahi kulipuka mwaka 2006 na siku za hivi karibuni mwezi Julai mwaka 2007.
Mchanga Unaohama; safu ya mchanga mweusi umetakana na majivu ya mlima wa volkeno wa Oldonyo Lengai, umekuwa ukisukumwa taratibu kuelekea upande wa Magharibi wa hifadhi kwa kiwango cha mita 17 kwa mwaka. Una kimo cha mita 9 na mzingo wenye urefu wa mita 100, unapatikana Kaskazini mwa bonde la Olduvai.
Bonde la Olkarien; eneo hili nalo ni muhimu katika hifadhi kwani hutoa hifadhi kwa ndege tai aina ya Ruppell Griffon. Msimu mzuri wa kutembelea eneo hili ni miezi ya Machi mpaka Aprili ambapo tai huzaliana. Wanyama huja eneo hili pale panapokuwa na malisho ya kutosha.
Kutazama ndege aina ya Flamingo na wengineo wa kila aina. Ndege aina ya Flamingo wanaonekana sana katika maziwa yanayopatikana ndani ya hifadhi. Mbali na ndege hao pia kuna aina mbalimbali za ndege ambao wanaweza kuonekana katika misimu tofauti ya majira ya mwaka hususani miezi ya mvua.
Safari ya Kuizunguka Hifadhi. Utakuwa hujaifaidi Ngorongoro kama haujavizungukia vivutio mbalimbali vinavyopatikana ndani yake. Kwa kuwatumia waongozaji wa mbuga, hakikisha kwamba unatembelea sehemu kama vile bonde la Olmoti kuelekea nyanda za Embakai, shuka chini kuelekea Bonde la Ufa, pandisha Kaskazini kwenye nyanda za hifadhi ya misitu na kisha eneo la tambarare la Mashariki kuzunga miamba ya Nassera, milima ya Goli na bonde la Olkarien.
Kwa hakika hii ni Edeni ya sasa kama watu wengi wanavyopenda kuiita kutokana na maajabu iliyonayo pamoja na historia ya binadamu wa mwanzo kuishi mule. Sasa kama watu wanasafiri kutoka kila pembe ya dunia kuja kulitembelea eneo hili kwa nini na wewe mtanzania usitenge muda na kupanga kufanya hivyo? Haihitaji kuwa milionea kutembelea eneo hili, kunafikika kwa urahisi na hata malazi ni nafuu pia kwani Jumia Travel wamekurahisishia hilo.