JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Serikali inapenda kuzitaarifu ofisi za umma na wananchi kwa ujumla kwamba imesitisha matumizi ya picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Serikali ya Awamu ya Tano, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli mpaka hapo itakapotangazwa tena. Awali majira ya saa 6: 00 mchana leo Novemba 6, mwaka huu Serikali ilitangaza kuhusu kuanza rasmi kwa matumizi ya picha ya Rais. Aidha, Serikali imesema kwamba itazitangazia ofisi hizo na umma wa Watanzania kuhusu kuanza tena kwa matumizi ya picha hiyo hapo baadae. Imetolewa na IDARA YA HABARI (MAELEZO). Novemba 6, 2015.
↧