Quantcast
Channel: BONGOWEEKEND
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1906

ASKARI WA JIJI LA TANGA WANUSURIKA KIPIGO KUTOKA KWA WASAFIRISHAJI

$
0
0


 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao kulia mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao katikati mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaj Mussa Mbaruku
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mhina Mustapha Selebosiakisisitiza jambo kwa wasafirishaji hao kulia kwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) alhaj Mussa Mbaruku jana amelazimikakuingilia kati na kuwaokoa askari wa Jiji la Tanga waliotaka kupigwana wafanyabiashara wa magari yaendayo Mombasa nchini Kenya kwa madaiya kukamata magari yanayotakiwa kuhamia stendi ya kange na kuwatoza
faini bila ya kuwa na mashine za EFDs.

Askari wa Jiji la Tanga ambao walinusurika kipigo hicho na kumlazimuMbunge huyo kuwaingilia kati na kuwaondoa eneo hilo ni Timime Makasina Emanuel Lyimo ambao walikuwa tayari wamezingizwa na wafanyabiasharahao wakijiandaa kuwatembezea mkongoto.

Magari hayo yalikuwa yamepakiwa kwenye eneo la barabara 10 karibu naAssad Hotel ambapo kumekuwa kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasanchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata moja ya garilinaloelekea mjini Mombasa na kulitaka kulitoza faini.

Baada ya kuwepo na kadhia hiyo ilimlazimu Mbunge huyo ambaye yupomkoani Tanga mapumziko ya mwishoni mwa wiki kabla ya kwenda mkoaniDodoma kuendelea na vikao vya kamati aliamua kufika eneo la tukio nakuwachukua askari hao kwa gari lake na kuwapeleka mpaka kwenye ofisizao zilizopo Kata ya Nguvumali Jijini Tanga.

Akizungumza  na wasafirishaji hao,Mbunge huyo aliwataka kuwawatulivu kwani suala hilo linajadilika na huenda likapatiwa ufumbuzikutokana na vikao vya baraza la madiwani ambavyo vinatarajiwa kuketihivi karibuni mjini hapa.

  Aidha pia Mbunge huyo alishtusha na kitendo cha askari hao kuchukuaushuru bila ya kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyumena utaratibu wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.

Hata hivyo askari, Timime Makasi ambaye ni askari wa Jiji ambayealisema wao wanafanya kazi chini ya Halmashauri ya Jiji hilo nawanatekeleza agizo hilo kama walivyoelekezwa ya kukamata gari zoteambazo zinatakiwa kupaki kwenye stendi kuu ya Kange.

Alisema kufuatia agizo hilo la halmashauri la kuzikamata gari hizo naatakae kwenda kinyume atatakiwa kutozwa faini ya shilingi 50,000 jambolililozua utata baada ya askari hao kuonekana kutokuwa na mashine zakielektroniki.

Aidha pia mmoja wa wamiliki wa magari yanayofanya safari zake za TangaMombasa Mohammed Nassor alisema kuwa swala liliwashitua zaidi nikutokuwepo na mashine hizo za risiti kama Serikali ilivyoelekeza jamboambalo lilitaka kuzua mzozo baina ya wafanyabiashara na askari hao.

Akizungumzia sakata hilo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj MustaphaSelebosi alisema halmashauri ina uhaba wa mashine za EFDs nahawaruhusu askari hao wa Jiji kuchukua ushuru bila kuwepo kwa mashinehizo.

Alisema wanachotakiwa kukifanya askari hao ni kulikamata gari nakulipeleka depo ya Halmashauri ambao ndio kunafanyika taratibu zakutozwa faini kwa mfumo wa mashine za EFDs
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1906

Trending Articles