Mkurugenzi wa Jamii Forum Maxence Melo pichani juu amepata dhamana leo baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili huku kila mmoja alisaini dhamana ya maneno ya Sh.Mil.5 na kuachiwa huru na Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam Godfrey Mwampamba.
Melo alishikiliwa na Polisi zaidi ya saa 72 kabla ya kupandishwa Mahakamani Ijumaa Desemba 16 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na makosa manne likiwemo la kuzuia upelelezi wa polisi.Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 29 mwaka huu.