Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kupambana na Trakoma (ITI) akizungumza na washiriki wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma kuhusu uendelezaji wa juhudi za kuwaelimisha wananchi na kutoa tiba katika maeneo yanakabiliwa na ugonjwa Trakoma kwa nchi washiriki wa mkutano huo kutoka Kenya, Tanzania, Uganda, Ethiopia, Eritrea, Sudani na Sudani Kusini.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Frida Mokiti akichangia wakati wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma jijini Arusha.