Mkazi wa Iringa Fadhil Mbembe (kulia) aliyeibuka mshindi wa mifuko 200 ya saruji na mkazi wa Njiro Faibe Ng’odi aliyeibuka na mifuko 400 wakiwa katika picha ya pamoja katika hafla hiyo.
DAR ES SALAAM
MKAZI wa Gangilonga Mkoani Iringa Maria Kalinga mwenye um ri wa miaka 35 leo ameibuka kuwa mshindi wa kwanza katika droo ya Jijenge na Twiga Cement huku akishinda zawadi ya mifuko 600 ya Cement.
Akizungumza mara baada ya kupigiwa simu na kupata taarifa za kushinda Maria alisema yeye ni fundi msaidizi wa ujenzi kuwa alikuwa akitetemeka kutokana na kushinda zawadi hiyo.
Nafasi ya pili ilikwenda kwa mkazi wa Kunduchi Cassian Mihoza ambaye ajinyakulia mifuko 400 ya Cement huku nafasi ya tatu ikienda kwa Kennedy Owili mkazi wa Jijini Mwanza ambaye amepata mifuko 200 ya Cement.
Washindi hao wamepatikana katika droo iliyochezeshwa katika Kiwanda hicho cha Twiga Cement kilichopo Wazo Hill Jijini Dar es Salaam.
Wakati huohuo pia ilichezeshwa droo ya mshindi wa mashine ya kisasa ya kufyatulia matofali ambapo Pascal Karani (25) mkazi wa Jijini Arusha mfanyakazi wa kwenye bustani ya maua amenyakua zawadi hiyo.
Droo hii ni ya tatu kuchezeshwa huku washindi wengine wakiwa wameshapatikana.