Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amewafuturisha watoto yatima 400 wakiwemo wanaoishi kwenye mazingira magumu kutoka Wilaya tofauti za Mkoa wa Pwani kwenye hafla ya Iftar iliyoanyika Ikulu ndogo Kibaha Mkoani Pwani na kuwakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge.
Watoto hao wamefturishwa tarehe 9 Machi 2025 huku Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kunenge amemwakilisha Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika Iftari hhiyo RC Kunenge amesema kuwa Rais Samia amekuwa na utaratibu wa kuandaa Iftar kwa ajili ya watoto yatima katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwamba mwaka huu inafanyika kwamara nne.
"Futari hii imeandaliwa na Rais Dkt.Samia kwa ajili ya watoto yatima na amekua akifanya hivi nchini kote tangu alupoingia madarakani alipenda kujumuika nasi leo lakini kutokana na majukumu yake kuwa mengi imebidi mimi nimuwakilishe "amesema RC Kunenge
Aidha, Kunenge amewaomba watoto hao pamoja na washiriki wengine katika iftari hiyo kuendelea kumuombea Rais ili aweze kuwa na afya njema ya kukulitumikia taifa na watu wake.
Katika hatua nyingine, Kunenge amesema kuwa mwaka 2025 ni mwaka wa uchaguzi hivyo ni vema wananchi wakajitokeza kupiga kura ili kuwachagua viongozi wazuri watakaoongoza nchi sambamba na kuiletea maendeleo.
RC Kunenge ametumia nafasi hiyo kuwaambia wananchi wa Mkoa wa Pwani kuwa Mkoa wa Pwani umepata heshima ya kuwa mwenyeji katika uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru utakao washwa tarehe 2 Aprili 2025 kwenye Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha huku amesisitiza kwa kusema kuwa maandalizi ya uzinduzi wa Mwenge yanaendelea vizuri pia ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika hafla hiyo Kitaifa.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge akisisistiza jambo kwenye hafla ya Iftar iliyofanyika 9 Machi 2025, Ikulu ndogo Kibaha Mkoani Pwani.Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hamis Mtupa amemshukuru Mhe. Rais Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa kuona umuhimu wa kutoa sadaka hiyo adhim kwa watoto hao .
Mtupa amesema kuwa wadau wengine wanapaswa kumuombea Rais Dkt Samia kwa sadaka hiyo aliyoiandaa huku akitoa wito kwa wadau wengine wenye uwezo kufanya ibada hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon akimpakulia ftari mtoto ambaye ni miongoni mwa watoto yatima na wanaoishi katika mqzingira magumu kwenye hafla ya Iftar iliyo andaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge ambapo fedha zimetolewa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.