Alhaji Mussa Mansoor amesema kwamba amekuzwa katika utaratibu wa kusoma Dua ya kurehemu baba yake Mzazi ,Viongozi mbalimbali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wametamgulia mbele ya haki.
"Jambo hili la kusoma Dua na kutoa sadaka nalifanya kwa zaidi ya miaka 12 sasa"amesema Alhaji Mansoor.
Mansoor amesema hayo leo Februari 28 wakati alipozungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza kusoma Dua iliyofanyika nyumbani kwake Kongowe Kibaha Mkoani Pwani.
"Huwa natoa sadaka ya futuri kwa waumini wa dini zote huku nikielewa kwamba Ramadhani ya kwanza huwa inakuwa ngumu hivyo nimetoa sadaka ya futari ambayo ni kianzio kwa mwezi mtukufu nimetoa sadaka ya futari kwa watu wa imani zote ilimradi amefika hapa basi kila mmoja anapata mzigo wake" amesema Alhaji Mansoor.
Amesema kuwa kwenye Quran tumeusiwa sana suala la kutoa sadaka pia waalimu wetu wanasema kuwa siku nzito kwa mwanaadamu ni siku yake ya kwanza kaburini ambapo mtu huomba kwa Allah arudishwe duniani ili aweze kutoa sadaka hivyo basi wote tudumu kwenye kutoa sadaka hivyo basi Inshaallah Mwenyeezi Mungu atujaalie tuufunge mwezi mtukufu wa Ramadhani salama na tumalize salama,amesema Alhaji Mansoor.