Quantcast
Channel: BONGOWEEKEND
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1907

MWILI WA MWANAMUZIKI MASHUHURI MAREHEMU TABIA MWANJELWA KUWASILI NCHINI JUMATATU

$
0
0
Marehemu Tabia  Mwanjelwa pichani  juu katika enzi za uhai wake.

Mwili wa mwanamuziki mkongwe, marehemu  Tabia Shabani Mwanjelwa, aliyefariki dunia Januari 25, 2025, huko Saarbrücken, Ujerumani, alikokuwa akiishi na familia yake, unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatatu, Februari 17, 2025, saa tano asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa binti yake kipenzi, Jane Jackson, mwili wa marehemu utawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam. Baada ya kuwasili, taratibu za mazishi zitaelekezwa Tukuyu, mkoani Mbeya, ambako atapumzishwa katika nyumba yake ya milele.

Marehemu Tabia Mwanjelwa atakumbukwa kwa vibao vyake maarufu kama "Jane Mimi Nahangaika" na "Kweli Maisha ni Safari Ndefu", alizoimba akiwa na bendi ya Maquis du Zaire miaka ya 1980. 

Ingawa aliishi Ujerumani kwa zaidi ya miaka 40, hakuwahi kusahau nyumbani kwani mara kwa mara alitembelea Tanzania, hususan kwao Mbeya, kila alipopata fursa.

Kwa mujibu wa Jane, mama yake alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kooni kwa muda mrefu kabla ya kufariki dunia Januari 25, 2025, saa moja na dakika 10 asubuhi.

Jane, ambaye si mwanamuziki kama kaka yake Moses, amesema ameshangazwa na simu na salamu nyingi alizopokea kutoka kila pembe ya dunia, akisema hakuwahi kutambua kuwa mama yake alikuwa maarufu na mwenye marafiki wengi kiasi hicho.

Mola ailaze pema roho ya marehemu - AMINA


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1907

Trending Articles