Quantcast
Channel: BONGOWEEKEND
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1907

TANZANIA YAPOKEA EURO MILIONI 158.5 KUTOKA UJERUMANI

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelile (kulia) akifurahia jambo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke (kushoto) wakati wa maandalizi ya kusaini mkataba utakaoipatia Tanzania jumla ya Euro milioni 158.5 kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi.
 
Imetolewa na
Msemaji wa Wizara ya Fedha
Bi. Ingiahedi Mduma

 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yasaini mkataba wa jumla ya Euro milioni 158.5 na Serikali ya  Ujerumani wenye lengo la kusaidia Bajeti ya Serikali pamoja na msaada wa kiufundi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servacius Likwelie aliposaini mkataba huo na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke leo jijini Dar es salaam.

Dkt. Likwelile alisema kuwa lengo kuu la fedha hizo zitaelekezwa katika sekta ya Afya, Mazingira, Nishati, Maji na kuimarisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. 

Kwa upande wake Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Egon Kochanke alisema kuwa  nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuwa nchi hizo zimekuwa na uhusiano mzuri wa muda mrefu ambao umekuwa na manufaa na tija kwa wananchi baina ya nchi hizo mbili.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1907

Trending Articles