ALIYEKUWA Kada wa Chama na kiongozi aliyeshika nyadhifa mbalimbali Serikalini Mbunge Mstaafu Sumbawanga Paul Petro Kimiti amewataka Wauguzi kote nchini kutoa huduma hiyo kwa wahitaji kwa kumtanguliza Mungu sababu kazi yao inahitaji Imani zaidi.
Kimiti amesema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani ambayo imeadhimishwa Kimkoa Mkoa wa Pwani hivi karibuni
huku akiwasisitiza watoe huduma kwa kuzingatia hofu ya Mungu zaidi ikifuatiwa na maslahi yao.
"Huduma yenu mnaoitoa kwa wagonjwa ni ya kiimani na mnapaswa kuelewa kwamba mfahamu kuwa hii ni ibada na malipo yenu yako kwa mungu " amesema Kimiti.
Aidha amewataka Maofisa Utumishi kushughulikia madai kwa watumishi ambao bado hawajalipwa stahiki zao ili kuwajenga mioyo wauguzi hao waweze kutoa huduma kwa wito kwa wagonjwa Hospitalini.
Kimiti amewapongeza wauguzi wa Mkoa wa Pwani kwa kazi kubwa wanayofanya na kwamba Serikali inatambua changamoto wanazopitia ndiyo maana kwasasa nguvu kubwa imeelekezwa katika kuwasaidia Wauguzi ili waweze kupata haki zao za msingi.
Aidha Chama Cha Wauguzi (TANA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya Chalinze wanatarajia kujenga chuo cha Uuguzi na Ukunga kwa kutumia majengo ya ofisi za awali za Halmashauri hiyo ambapo wameomba kusaidiwa kupata wadau wa kufanya ukarabati na ununuzi wa vifaa ili waweze kukamilisha hatua za kuanzisha chuo hicho.
Katika maadhimisho hayo Wauguzi walikula kiapo Chao huku wakiwasha mishumaa.
" Wauguzi mnaapa kila mwaka kwa ajili kukumbushwa wajibu wenu hivyo mkafanye kazi kwa maadili na kuheshimu kiapo chenu" amesema Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dkt.Kusilie Ukiyo.
"Wauguzi tujiulize kwanini tunaapa kila mwaka katika taaluma zingine huwa hawaapi kila mwaka kama ninyi hivyo endeleeni kukiishi kiapo chenu timizeni wajibu wenu mbele ya Mwenyeezi Mungu " amesema Dkt. Ukio.
Aidha Dkt. Ukio ameahidi kuboresha maadhimisho ya wauguzi katika siku zijazo.
"Dkt.Ukui amesema kuwa ndani ya miaka mitatu kiasi cha Bil.25 zimetumika katika sekta ya afya Mkoa wa Pwani,pia naahidi kuwa tutalifanyia kazi suala la upungufu wa wafanyakazi vifaa tiba na tunawapongeza kwa kufanya kazi bika kukata tamaa na serikali inatambua na kuthamini huduma na kazi yenu kwani bila uuguzi hakuna huduma bora kwa mgonjwa" amesema Dkt. Ukui.
Wakati huohuo Dkt.Ukui amekemea tabia ya wananchi kujichukulia sheria mikononi mwao kwa kuwapa vipigo wauguzi amesema kuanzia sasa sheria itachukua mkondo wake.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wauguzi amewapongeza Wauguzi hao kutokana na huduma wanayoitoa kwa kusema kuwa Wauguzi wengi ndiyo wanaoongoza katika Zahanati nyingi nchini,"ninyi mnafanya kazi kubwa nchini msichoke changamoto zenu za malipo ya kazi za ziada katika kila kituo tutaweka miongozo mizuri" amesema.
Wauguzi hao wametakiwa kupunguza vifo vya mama na mtoto huku akisisitiza wauguzi hao na kusema kuwa huduma za Uuguzi na Ukunga zinasimamiwe na maadili bora ya kitaaluma.
"Mgonjwa au mteja anapofika Kituoni au Hospitali anatajia kupata maneno ya upendo na faraja zingatieni hilo.